Amesema, mashindano hayo yayarishwa mibashara kupitia televisheni, akitoa wito kwa makampuni mbalimbali yanayohitaji kutangaza biashara zao ndani na nje ya mipaka ya Tanzania kupitia mashindano hayo.
Mutesi amezitaja nchi washiriki kuwa ni Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Ethiopia, Eritrea, Djibouti na Tanzania.
Nyingine ni Somalia, Madagascar, Malawi, Ushelisheli, Sudan Kusini, Comoro na Mauritius.
Mashindano hayo yalibuniwa na kuanzishwa na Rena Callist yalianza mwaka 1996 na kuwahi kufanyika Burundi kwa udhamini wa Hayati Rais Piere Nkurunzinza.
“Kuanzia sasa mashindano ya Miss East Africa yatakuwa yakifanyika kila mwaka, yatasaidia katika kudumisha umoja wa Afrika Mashariki, kukuza utalii, kutangaza fursa mbalimbali za uwekezaji,”amesema Mutesi.
“Mashindano pia yatatoa elimu na kusaidia katika changamoto mbalimbali hasa zinazowakabili wanawake na watoto wa ukanda huu wa Afrika ya Mashariki,"amesema.