Mke wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar awapa somo wanawake

Na Mwandishi Diramakini

Mke wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Bi. Zainab Kombo amewataka wanawake kujitambua na kusimamia ndoto zao ili waweze kufikia malengo yao.
Bi. Zainab ameyasema hayo wakati akifungua kongamano la Ustaarabu wa Mwanamke Zanzibar.

Kongamano hilo la tatu Zanzibar lililokusanya wanawake kutoka sekta mbalimbali wakiwemo wajasiriamali, wanafunzi wa vyuo, wafanyabiashara na mama wa nyumbani limefanyika leo Juni 24 katika ukumbi wa Studio ya Rahaleo mjini Zanzibar.

"Mafunzo haya ni muhimu sana katika maendeleo ya mwanamke kuelekea kujikomboa kiuchumi na kuelewa nafasi yake katika jamii,"ameeleza Bi. Zainab.

Aidha, Bi. Zainab amewataka wanawake katika jamii kushirikiana ili kuweza kuzigeuza changamoto zinazowakabili kuwa fursa kwao. "Ni wazi wanawake tunakabiliwa na changamoto nyingi katika jamii, lakini tusipokuwa wamoja na kushirikiana tutajikuta tunakata tamaa mapema nakupoteza fursa adhimu katika jamii zetu", aliongeza.
Mke huyo wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar amewataka waandaaji wa kongamano hilo kufanya tathmini kila baada ya shughuli hiyo ili kujua ni kwa kiasi gani malengo yanafikiwa.

Sambamba na hayo Bi.Zainab ameishukuru serikali ya awamu ya nane kwa kuthamini mchango wa mwanamke kimaendeleo na hatimae kuwa na ustawi mzuri wa familia na taifa kwa ujumla ili kuyafikia Malengo Endelevu ya Dunia (Sustainable Development Goals) bila ya kuathiri ustaarabu wa jamii na kuheshimu mila, silka na utamaduni wa asili wa Wazanzibari.

Akitoa neno la shukrani Bi.Maryam Hamdani, amesema kongamano hili ni fursa adhimu kwa mwanamke wa Kizanzibari kurejesha ustaabu wake.

Sambamba na kuwataka wanawake katika kongamano hilo na jamii kwa ujumla kuzichukua nasaha za Mke wa Makamu wa Kwanza wa Rais, na kuzifanyia kazi kwa maslahi mapana ya kumkomboa mwanamke.

Kongamano hilo limefanyika chini ya kaulimbuiu inayosema "Mwanamke kamata fursa Dunia inakusubiri".

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news