NA MWANDISHI DIRAMAKINI
Uchaguzi wa Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA) umefanyika huku wakishindwa kupata viongozi wake wa juu.
Viongozi hao ni ngazi ya Mwenyekiti,Mwenyekiti Msaidizi na Katibu Msaidizi baada ya kura zao kuongezeka,tofauti na idadi ya wapiga kura waliokuwepo ukumbini kwa baaadhi ya wagombea wa nafasi hizo. Uchaguzi huo ulifanyika Juni 26,2021mkoani Tanga.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, George Mushimba akitangaza matokeo amesema, Kanuni ya 23 kifungu kidogo cha 1 cha Sheria za Uchaguzi ya TFF,inasema inapotokea tatizo hilo kwenye uchaguzi kura zote zinakuwa batili na nafasi hizo kukosa uwakilishi na uchaguzi utarudiwa mara moja.
Kwenye uchaguzi huo nafasi ya Mwenyekiti,Makamu Mwenyekiti na Katibu Msaidizi zimebaki wazi baada ya kuwa na dosari kwenye akidi ya wapiga kura, kutokana na idadi ya kura kwa wagombea kuzidi hadi kufikia 78.
Katika uchaguzi huo jumla ya wapiga kura walikuwa 73, lakini kura za wagombea wengine zilizidi akidi iliyokuwepo ukumbini,ambapo waliogombea nafasi ya Uenyekiti ni Sara Chao na Amina Karuma,ambaye alipata kura za ndio 53 na kura za hapana 23 na kura zikizoharibika zilikuwa 2 na kufanya jumla ya kura zilizopigwa kwake kuwa 78,ambayo ni tofauti na idadi ya wapiga kura ambayo ni 73.
Sara Chao alipata kura za ndio 31 kura za hapana 40 na kura zilizoharibika ni 3 na kufanya jumla ya kura zilizopigwa kuwa 74 ambayo ni zaidi ya wapiga kura waliokuwepo ukumbini kupiga kura.
Nafasi za makamu Mwenyekiti imeshindikana baada ya idadi ya kura kuzidi ambayo ilikuwa inagombewa na Roselyn Kisiwa aliyepata kura 75 ambayo ni zaidi ya wapiga kura na Beatrice Mgaya kura za ndio 27 na hapana 37 na zilizoharibika ni 3,hapa kura za Roselyn zilizidi hivyo ni batili kwa kuwa imekiuka Kanuni ya 23 kifungu kidogo cha 1 cha Sheria za uchaguzi ya TFF,ambayo inasema inapotokea tatizo kwenye uchaguzi kura zote zinakuwa batili.
Nafasi ya katibu mkuu imekwenda kwa Somoe Robert ambaye amepata kura za hapana 25 na kura za ndio 48 na kufanya kura zake kuwa halali kwa kupigiwa na wajumbe wote 73.
Nafasi ya Katibu Msaidizi ambayo ilikuwa inawaniwa na Veronika Willium imeingia dosari baada ya kura kuzidi,kura za ndio 33 na hapana zikiwa 43, ambapo kura zilizopigwa zimezidi idadi ya wapiga kura.
Nafasi ya Mjumbe wa Mkutano Mkuu ya TFF imeenda kwa, Zena Suleiman ambaye alikuwa akigombea peke yake, ambapo alipigiwa kura za ndio 45 na kura za hapana zikiwa 28.
Kwa upande wa wagombea wa nafasi za ujumbe zilikuwa sita na nafasi zilizokuwa zinatakiwa ni nne na waliofanikiwa kupita ni wenye idadi ya kura nyingi na wagombea walikuwa Jackline Meena 30,Mwanaisha Balisa 30,na waliofanikiwa kuwa wajumbe ni Mwanaheri Kalolo kura 34,Ema John kura 48,Mbinagwe Sungura kura 40,Irene Ishengoma kura 57 na kuwa wajumbe wa kamati ya Utendaji ya TWFA.
Tags
Michezo