NA MWANDISHI DIRAMAKINI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 02 Juni, 2021 amemuapisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Ikulu (Kazi Maalum), Mhe. Kept. Mst. George Huruma Mkuchika aliyemteua tarehe 31 Machi, 2021 na amewaapisha Makatibu Tawala wa Mikoa 11 aliowateua tarehe 29 Mei, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimuapisha Cpt. Mst. George Huruma Mkuchika kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Ikulu (Kazi Maalum) katika hafla ya Uapisho iliyofanyika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma leo.
Hafla ya kuapishwa kwa Makatibu Tawala wa Mikoa hao imefanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa na Naibu Spika Mhe. Tulia Ackson.Makatibu Tawala wa Mikoa walioapishwa ni Mhe. Balozi Batilda Salha Buriani (Shinyanga), Bw. Rodrick Lazaro Mpogolo (Katavi), Bi. Dorothy Aidan Mwaluko (Singida), Dkt. Athumani Juma Kihamia (Arusha), Mhandisi Mwanaisha Rajabu Tumbo (Pwani), Bw. Ngusa Dismas Samike (Mwanza), Bw. Hassan Abasi Rugwa (Dar es Salaam), Dkt. Fatuma Ramadhan Mganga (Dodoma), Bw. Musa Ramadhani Chogero (Geita), Bi. Pili Hassan Mnyema (Tanga) na Bi. Prisca Joseph Kayombo (Simiyu).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimuapisha Balozi Batilda Salha Burian kuwa Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimuapisha Rodrick Lazaro Mpogolo kuwa Katibu Tawala mkoa wa Katavi.
Mhe. Rais Samia ameshuhudia Makatibu Tawala wa Mikoa hao pamoja na Wakuu wa Taasisi 4 aliowateua hivi karibuni wakila kiapo cha uadilifu kwa watumishi wa umma kilichoongozwa na Kamishna wa Maadili Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Sivangilwa Sikalalilwa Mwangesi.
Wakuu wa Taasisi hao ni Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai CP. Camilius Wambura, Mkuu wa Kamisheni ya Fedha na Lojistiki wa Jeshi la Polisi CP. Hamad Khamis Hamad, Afisa Mtendaji Mkuu, Tume ya Ushindani wa Biashara Bw. William Erio na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi Dkt. John Kedi Mduma. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimuapisha Dorothy Aidan Mwaluko kuwa Katibu Tawala Singida. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimuapisha Dkt. Athumani Juma Kihamia kuwa Katibu Tawala mkoa wa Arusha.
Akizunguza katika hafla hiyo, Mhe. Rais Samia amewapongeza viongozi wote walioapishwa na amewataka kwenda kuchapa kazi kwa juhudi, maarifa, kuzingatia sheria na utu ili kutimiza matarajio ya wananchi kwa Serikali yao.
Mhe. Rais Samia amewataka Makatibu Tawala wa Mikoa kutekeleza ipasavyo wajibu wao wa kuwa kiungo kati ya Serikali Kuu na Serikali za Mitaa, kusimamia vizuri rasimali za umma hasa ukusanyaji wa mapato na matumizi yake, kuhakikisha mapato yanayopaswa kuelekezwa katika shughuli za maendeleo na makundi maalumu yanapelekwa kama ilivyopangwa katika halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mwanaasha Rajabu Tumbo kuwa Katibu Tawala mkoa wa Pwani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimuapisha Ngusa Dismas Samike kuwa Katibu Tawala mkoa wa Mwanza. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimuapisha Hassan Abasi Rugwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimuapisha Fatuma Ramadhan Mganga kuwa Katibu Tawala mkoa wa Dodoma.
Ameonya dhidi ya vitendo vya baadhi ya viongozi kudharauliana, kubaguana, kurumbana na kugombana badala ya kushirikiana kusukuma mbele maendeleo ya Mikoa na taasisi wanazoziongoza pamoja na kutatua kero na malalamiko ya wananchi.
Pia, ametaka viongozi hao kwenda kushughulikia migogoro inayowakabili wananchi hususani migogoro ya mirathi ambayo inawaathiri zaidi wanawake, migogoro ya ardhi na ameonya kuwa hatavumilia kuona viongozi hao wanakuwa sehemu ya migogoro kutokana na kujimilikisha ardhi katika maeneo wanayoongoza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimuapisha Musa Ramadhani Chogero kuwa Katibu Tawala mkoa wa Geita, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimuapisha Pili Hassan Mnyema kuwa Katibu Tawala mkoa wa Tanga.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimuapisha Prisca Joseph Kayombo kuwa Katibu Tawala mkoa wa Simiyu. Viongozi mbalimbali walioapishwa pamoja na kuteuliwa katika nafasi mbalimbali wakila Kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi wa Umma mara baada ya tukio la Uapisho katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.(PICHA ZOTE NA IKULU).
Mhe. Rais Samia amewataka Makatibu Tawala wa Mikoa kushughulikia changamoto zinazowakabili watumishi wa umma, kusimamia uchumi vizuri ikiwa ni pamoja na kusimamia uendelezaji wa viwanda, kuvutia wawekezaji, kusimamia vizuri taasisi za Serikali zilizopo katika Mikoa yao, kusimamia kwa ukaribu miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao na kushirikiana na wananchi na Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika utekelezaji wa Ilani iliyoiweka Serikali madarakani.
Aidha, Mhe. Rais Samia amewaonya viongozi hao pamoja na viongozi wengine walioteuliwa katika nyadhifa mbalimbali kuacha vitendo kwenda Majimboni kufanya kampeni za chinichini za kutaka Ubunge na badala yake wawaache Wabunge wa Majimbo hayo kutumikia wananchi kwa amani mpaka wakati wake ukifika.
Tags
Habari