NA MWANDISHI DIRAMAKINI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema tayari kuna wagonjwa wa virusi vya Corona (Covid-19) ambao wamebainika nchini kwenye wimbi la tatu la ugonjwa huo.
Kutokana na hali hiyo amewataka viongozi wa dini kuwaelekeza waumini wao kuchukua tahadhari dhidi ya Corona.
“Dunia kwa sasa inakabiliwa na janga la Covid-19 na Kanisa tangu mwanzo limekuwa na msimamo thabiti wa kupambana na gonjwa hili, niwaombe Maaskofu na viongozi wengine wa dini endeleeni kuwakumbusha waumini wajikinge na Corona;
Mheshimiwa Rais Samia ameyasema hayo leo Juni 25,2021 wakati akizungumza na Maaskofu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) kwenye makao yao makuu yaliyopo Kurasini mkoani Dar es Salaam.
“Duniani kuna wimbi la tatu la Corona, tumetoka kwenye wimbi la kwanza Tanzania tumeingia, tumekwenda wimbi la pili na sasa wimbi la tatu, ishara ndani ya nchi tayari zinaonekana, tayari tuna wagonjwa ambao wameshaonekana kwenye wimbi hili la tatu.
“Nilipotembelea Mwananyamala Hospitali, kuna wodi Daktari alikuwa ananiingiza akaniambia humo kuna wagonjwa wenye matatizo ya kupumua nikamwambia kuwa muwazi ni COVID-19? akasema ndio, wakati wapiga picha wangu wameshatangulia nikawaambia tokeni haraka, hili jambo bado lipo tuchukue tahadhari ili tuepushe vifo,"amesema.
Tags
Habari