Na Derick Milton, Simiyu
Mkuu wa mkoa wa Simiyu ametoa muda wa wiki moja kwa Meneja wa wakala wa Barabara (Tanroads) mkoani humo, Mhandisi Albert Kent kufanya mchanganuo wa ushuru na mrabaha ambao unatakiwa kulipwa na mkandarasi CHICCO Kama tozo za kokoto, mawe na mchanga.
Mkandarasi huyo ambaye anatengeneza Barabara ya Mwigumbi - Maswa yenye urefu wa kilometa 50 kwa kiwango cha lami, anadaiwa kugoma kulipa tozo hizo kwa halmashauri ambazo amekuwa akichukua malighafi hizo pamoja na Ofisi ya Madini kama sheria inavyotaka.
Mkuu huyo wa mkoa ametoa maagizo hayo, wakati akikagua Barabara hiyo kutokana na kuanza kuaribika kabla ya kufunguliwa licha ya kukamilika kwa kiwango kikubwa, ambapo eneo kubwa limeanza kuwa na mashino huku sababu kubwa ikielezwa kuwa kujengwa chini ya kiwango.
Kafulila amesema kuwa toka mwaka 2015 mkandarasi huyo ameanza kujenga Barabara hiyo amegoma kulipa ushuru kwa halmashauri ya Maswa, lakini pia mrabaha wa Ofisi ya Madini zaidi ya Milioni 600 huku Taroads wakilalamikiwa kushindwa kutoa ushirikiano ili tozo hio zilipwe.
Kabla ya kutoa maagizo hayo, Mkuu huyo wa Mtaka alimtaka Mkurugenzi wahalmashauri ya Maswa Dkt Fredrick Segamiko kutoa maelezo ya tatizo hilo, ambapo Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa wameangaika Sana kulipwa ushuru huo lakini imeshindikana.
Segamiko amemweleza Mkuu huyo wa mkoa kuwa, Ofisi yake imekuwa ikiomba ushirikiano kutoka Tanroads mkoa, lakini hawapati licha ya kwenda mara kwa mara na kueleza tatizo la mkandarasi huyo kushindwa kulipa ushuru kwa muda mrefu.
Kafulila amemtaja Meneja huyo wa Tanroads ofisini yake kuacha tabia ya kutokutoa ushirikiano kwa mamlaka nyingine za serikali kwani wote wanaitumikia serikali moja hivyo hakuna haja ya kutokufanya kazi kwa pamoja.
"Hadi Jumatatu wiki ijayo nipate mchanganuo huo wa malipo hayo na mkandarasi analipa lini, Tanroads ndiyo wenye jukumu hili hampaswi kulikwepa kwa sababu nyie ndiyo mmewaleta hawa wakandarasi na watakiwa kufuata sheria," amesema Kafulila.
Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa ametoa onyo la mwisho kwa Tanroads juu ya wakandarasi wake kutokulipa tozo hizo za kisheria, ambapo ametaka kila mkandarasi ambaye atapewa kazi anatakiwa kuhakikisha analipa ushuru na mrabaha huo ndani ya muda.
"Tanroads hii iwe mara ya mwisho, leseni mnatoa ninyi alafu wanagoma kulipa kulipa ushuru na mrabaha, na mkiombwa kutoa ushirikiano mnagoma, tafsiri yake ni kuwa Tanroads mnawasaidia wakandarasi kukwepa kodi," amesema Kafulila.
Aidha, Mkuu huyo wa mkoa ametaka kusimamia kwa miradi ya serikali ili isijengwe chini ya kiwango Kama ambavyo imetokea kwenye Barabara hiyo huku akitoa onyo kutojirudia kwa uzembe huo kwenye miradi mingine.
Akizungumzia ubovu wa Barabara hiyo Mhandisi Kent amesema kuwa, mkandarasi ameelekwezwa kurudia matengenezo katika maeneo yote ambayo yameharibika kwa kutumia gharama zake mwenyewe.
Tags
Habari