REA katika semina ya Wabunge wa PAC, mambo mazuri yanakuja

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA, Mhandisi Amos Maganga ameeleza Juni 10, 2021 jijini Dodoma wakati akiwasilisha Mada kuhusu Majukumu ya Wakala huo kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kuwa, wameandaa mikakati kabambe ikiwemo;
Awali, akizungumza katika Semina hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya PAC, Naghenjwa Kaboyoka aliipongeza REA, TANESCO na Wizara ya Nishati kwa ujumla, kwa kazi nzuri inayoendelea kufanyika kuunganisha umeme katika maeneo mbalimbali nchini hususan kwa wananchi walioko vijijini.

Naye Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato, aliwahakikishia Wajumbe wa Kamati hiyo kuwa, Wizara yake itaendelea kufanya kazi kwa bidii katika kuhakikisha watanzania wote wanafikiwa na huduma hiyo muhimu ya umeme.

Aliwaomba Wawakilishi hao wa wananchi kuwa Mabalozi wazuri wa masuala ya nishati katika majimbo yao kwa kuwahamasisha wakazi wa maeneo hayo wanayoyawakilisha kuchangamkia fursa za kuunganisha umeme katika kaya na maeneo yao ya biashara ili kuboresha maisha yao.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali amewashukuru Wabunge hao kwa mwitikio wao katika kushiriki Semina hiyo na kuahidi kuwa Wizara itazingatia michango na maelekezo mbalimbali waliyoyatoa ili kuendelea kuboresha sekta ndogo ya umeme na nishati kwa ujumla.Zinazohusiana na REA soma hapa.


Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news