Serikali yadhamiria kupata ufumbuzi wa kudumu uhaba wa watumishi mamlaka za utoaji haki nchini

Na Doreen Aloyce,Diramakini Blog

SERIKALI imesema imeazimia kuendelea kuimarisha taasisi zote za utoaji haki hasa Mahakama pamoja na kutatua changamoto zinazoikabili sekta hiyo hususani uhaba wa watumishi huku ikiwataka Wanasheria wote wa umma nchini kuhakikisha wanafanya mashauriano na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kabla ya kuanza kesi ili kushinda.
Kauli hiyo imetolewa jijini Dodoma na Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Paramagamba Kabudi wakati akifungua mkutano wa kwanza wa Watumishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali na kusema Serikali itahakikisha inazifanyia kazi changamoto zote.

Aidha, amesema katika kufanya mashauri yote kupitia ofisi ya wakili wa Serikali itasaidia wao kujipanga kisheria katika mashauri yao.

Kabudi ameeleza hali hiyo itasaidia Taifa kuondokana na matumizi makubwa ya fedha kwa ajili ya kulipa mawakili wa nje pale Taifa linapofunguliwa kesi nje ya nchi.

“Nipende kuwaeleza hivi sasa tuendelea tu na hiki kipindi cha mpito, lakini baadaye nataka ofisi hii ndiyo iwe inasimamia kesi zote za serikali za ndani na nje tutafanikiwa kama tutaendelea kuimarisha Ofisi hii ya Wakali Mkuu wa Serikali,”amesema.

Hata hivyo amewataka mawakili wa mashirika ya umma ambao wamekuwa wakisimamia kesi mbalimbali kutoa taarifa kwa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali na siyo kusubiri hadi hali inapokuwa mbaya.

Pia Kabudi amesema, ipo haja ya kuwa na taasisi ya mafunzo ya Mawakili wa Ofisi ya Serikali ambayo itatumika kutoa mafunzo ya mara kwa mara ili kuimarisha utendaji kazi wao.

Hata hivyo, ametaka kuona umuhimu wa matumizi ya lugha ya Kiswahili katika mahakama kwakuweka istilahi na misamiati ya kisheria katika suala zima la uendeshaji kesi.

Kwa upande wake Wakili Mkuu wa Serikali,Gabriel Malata ameiomba Serikali kupitia Wizara ya Katiba na Sheria kuwapa mafunzo ili kuwajengea uwezo katika uendeshaji wa madai ya Gesi na Madini katika kuelekea uchumi wa Viwanda kutokana na wanasheria wengi kutokuwa na uelewa wa masuala hayo.

"Changamoto nyingine tulizonazo Ni pamoja na uhaba wa vitendea kazi ikiwemo magari katika ofisi zatu takribani 16, kwani kwa sasa tuna magari 15 ambayo hayakidhi,"amesema.

Sambamba na hilo ameeleza changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa watumishi na vitendea kazi ikiwemo watumishi waliopo ni 143 huku mahitaji yakiwa ni 312.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news