Sura mpya ya Yanga SC hii hapa, Dkt.Mwingulu, Mwambe, Tarimba ndani

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

"Hatutaweza kusema nani atakuwa Mwenyekiti wa Baraza hili wao wenyewe tunawaachia wamchague Mwenyekiti wao;

Menyekiti wa Klabu ya Yanga, Dkt.Mshindo Msolla ameyasema hayo leo Juni 27, 2021 kupitia mkutano wa wanachama unaofanyika Dar es Salaam.

Uongozi wa Yanga umeunda upya Baraza jipya la Wadhamini likiwa na sura mpya tatu kati ya watano ambapo hii inathibitisha rasmi mchakato wa mabadiliko ndani ya Yanga utaendelea kama kawaida baada ya leo kupitishwa na wanachama.
Pia wanachama wa Yanga wamepitisha mabadiliko ya Katiba yatakayowawezesha kufanya marekebisho ya mfumo wa uendeshaji.

Kwa pamoja,wanachama hao wameridhia kwa kura ya ndiyo kuhusiana na mabadiliko hayo, hivyo kuthibitisha kuwa, maazimio yote yamepita kwa asilimia 100.

Akitangaza uamuzi huo Mwenyekiti wa Yanga, Dkt.Mshindo Msolla amesema, wameunda baraza jipya la wadhamini litakaloanza kazi mara moja kama ambavyo katiba yao inaelekeza.

Dkt.Msolla amewataja wajumbe hao kuwa, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Nchemba ambaye ni Waziri wa Fedha na Mipango akiwemo Abbas Tarimba ambaye ni mfanyabiashara na Mbunge wa Kinondoni mkoani Dar es Salaam.

Pia wengine ni Geoffrey Mwambe ambaye ni Waziri wa Uwekezaji,Fatma Karume mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Waziri Ofisi ya Rais Kazi Maalum, Kapteni mstaafu George Huruma Mkuchika.

Baraza hilo, sura mpya tatu za wajumbe ni ya Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Nchemba,Tarimba na Mwambe.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news