Na Anneth Kagenda, Diramakini Blog
JAMII imeaswa kuacha mara moja kuweka simu za mkononi kwenye mto na kuzilalia kwa kile kilichodaiwa kuwa wakati mwingine simu hizo zinaweza kuleta madhara baadaye kwani zinakuwa na mionzi japokuwa siyo kwa kiasi kikubwa.
Pia jamii hiyo hiyo imeaswa kuacha kuongea na simu hizo wakati simu ikiwa inalalamika kutokuwa na chaji (Low battery) jambo lililoelezwa kwamba wakati huo simu husika huwa mionzi yake inakuwa na nguvu zaidi.Jifunze, :TAEC mbioni kuanzisha mradi wa teknolojia ya kuhifadhi mazao kwa kutumia teknolojia ya mionzi visiharibike mapema
Hayo yameelezwa mkoani Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na Wawasilishaji wa mada mbalimbali zilizokuwa zinatolewa wakati wa Semina ya Wahariri na waandishi habari wa vyombo mbalimbali iliyoandaliwa na Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC), semina hiyo ililenga kuwaongezea uelewa na udhibiti na matumizi salama ya mionzi nchini.a wiki..
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki (TAEC) Profesa Lazaro Busagala akizungumza katika semina kwa wahariri na waandishi wa habari ili kuwajengea uwezo na udhibiti na matumizi salama ya mionzi nchini pamoja na kuwajengea uelewa kuhusu Jukumu la (TAEC) kwa Taifa na jamii kwa ujumla. Semina hiyo ilifanyika katika ukumbi wa jengo la utawala Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa Ofisi ya Kanda ya Dar es Salaam Tume ya Unguvu za Atomiki (TAEC,) Dkt. Wilbroard Muhogora akiwasilisha mada kuhusu mionzi katika semina ya wahariri na waandishi wa habari katika semina iliyofanyika katika ukumbi uliopo katika jengo la utawala Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mtafiti Mwandamizi Sayansi ya Nyukilia, Alex Pius Muhulo akiwasilisha mada kuhusu mionzi katika matibabu na utafiti wa magonjwa kwa binadamu
"Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) imeona upo umuhimu wa kutoa semina hii hasa kwa kuanza na waandishi na wahariri kwani ndio wamekuwa wakisaidia kufikisha taarifa mbalimbali kwenye jamii," amesema Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo Prof. Lazaro Busagala, na kuongeza;
"Kumekuwapo na changamoto kubwa tuliyonayo ambapo wananchi wengi wamekuwa hawana uelewa mzuri juu ya tume hii pamoja na kazi zake jambo ambalo wakati mwingine wamekuwa wakiihusisha na utengenezaji wa mabomu, jambo ambalo siyo kweli sisi tunahusika na mambo ya mionzi," amesema.
Wawasilishaji waliowasilisha mada mbalimbali kwenye semina hiyo kuhusiana na uelewa, Udhibiti na Matumizi salama ya mionzi Nchini ni Dkt. Wilbroad Muhogora ambaye ni Mkuu wa Ofisi Kanda ya Mashariki TAEC pamoja na Alex Muhulo ambaye ni Mtafiti Mwandamizi Nyuklia Teknolojia wa TAEC.Zinazohusiana, BILIONI 10/- ZATUMIKA KUJENGA MAABARA CHANGAMANO TUME YA NGUVU ZA ATOMIKI TANZANIA
Mada zilizohusu mionzi zilikuwa ni nyingi, lakini baadhi yake zilikuwa ni zile zinazohusu mionzi kwenye simu, vyakula, vyuma chakavu, uelewa juu ya X-ray, aina ya mionzi, vitambuzi vya mionzi pamoja na madhara yatokanayo na mionzi na usalama wa mionzi na pia namna na njia za kujikinga, usalama wa kitaifa na kimataifa.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Profesa William Anangisye akitoa ukaribisho kwa Waziri, Tume ya Nguvu za Atomiki (TAEC)na washiriki wa semina ya kutoa mafunzo kwa wahariri na waandishi wa vyombo vya habari yaliyofanyika UDSM. Alisemakuwa kwa mwaka wa masomo 2020/2021 Chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimedahili wanafunzi 60 wanaosoma kozi inayohusiana na nguvu za atomiki huku kukiwepo na wanafunzi 7 wanaosoma shahada ya umahiri kuhusu masuala ya nguvu za atomiki.Zinazohusiana,Waziri Ndalichako, Prof.Busagala waainisha faida za teknolojia ya nyuklia
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Willium Anangisye na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC,) Prof. Lazaro Busagala, wahariri na waandishi wa habari wa wakiwa katika picha ya pamoja.
Semina hiyo ilifunguliwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako ambaye aliwataka TAEC kuhakikisha inasambaza elimu zaidi kwenye jamii ili iweze kupata elimu na kuelewa ni kwa jinsi gani tume hiyo inafanya kazi.
"Wananchi wengi hawana uelewa na wala hawajui sahihi juu ya nguvu za Atomiki na hili limekuwa likipelekea kuwepo kwa upotoshaji juu ya jambo hilo, hivyo basi jitahidini kuhakikisha elimu inatolewa na kwa usahihi zaidi," amesema Waziri.
Tags
Habari