TANESCO YAWEZESHA MATIBABU MOI

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limechangia kiasi cha Shilingi Milioni Ishirini kwa Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), ili kusaidia na kuwezesha matibabu ya watoto wenye vibiongo katika hospitali hiyo.
Meneja Uhusiano wa Shirika la umeme nchini (Tanesco) Bi Johary Kachwamba wa pili kushoto akimkabidhi mfano wa hundi Naibu Spika Mh Tulia Akson wa pili kulia kama mchango wa shirika hili ili kusaidia matibabu ya watoto wenye vibiongo katika Taasisi ya Mifupa Moi halfa iliyofanyika jana kwenye viwanja vya Chuo cha MUHAS (Muhimbili). (Na Mpiga Picha Wetu).

Akiongea katika Mbio fupi za kuchangia matibabu hayo (Moi marathoni) Juni 27,2021, katika viwanja vya chuo cha udaktari Muhimbili MUHAS, Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Johary Kachwamba amesema kuwa TANESCO imeona umuhimu wa kurudisha kwa jamii sehemu ya kile inachokipata kupitia mauzo ya Umeme kwa kusaidia matibabu ya watoto hao.

"TANESCO imeamua kuangaza maisha ya jamii yetu kwa namna ya tofauti, tunafarijika kwamba matibabu haya yataokao uhai na kurejesha furaha kwa watoto wenye vibiongo," amesema Bi. Kachwamba

Sambamba na kuchangia kiasi hicho, wafanyakazi wa TANESCO pia wameshiriki katika kukimbia mbio hizo katika makundi ya km 5, km 10 na km 21, ambapo mshindi wa tatu mbio za km 5, kwa upande wa Wanaume ni Bw. Sebastian Kwayu, kutoka TANESCO.

Mgeni Rasmi aliepoke hundi kwa niaba ya MOI katika tukio hilo ni, Mhe. Tulia Akson, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo alitoa shukrani kwa wote waliochangia ikiwa ni pamoja na TANESCO.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news