NA MWANDISHI DIRAMAKINI
Mhubiri wa Kimataifa kutoka nchini Nigeria, Temitope Balogun Joshua, maarufu kama TB Joshua amefariki Dunia akiwa na umri wa miaka 57.
Amefariki saa chache baada ya kumaliza Huduma ya kichungaji katika Kanisa lake Jijini Lagos.
Ni mwanzilishi wa Kanisa la Synagogue Church of All Nation (SCOAN) na Kituo cha Runinga cha Emmanuel ambacho amekuwa akikitumia katika mahubiri yake na kuwavutia watu wa mataifa mbalimbali.
Kutokana na kile kinachoelezwa kuwa miaka ya 1970 alishindwa kuhitimu elimu ya sekondari kutokana na kuzama zaidi katika kusoma Biblia, mwaka 1990 alimuoa Bi. Evelyn na wote kujaliwa watoto watatu.
Aidha, kwa mujibu wa jarida maarufu la Forbes la Marekani linalotafiti mali walizonazo watu matajiri duniani, mwaka 2011 liliripoti kuwa kwa upande wa masuala ya dini mhubiri huyo alikuwa kiongozi namba 3 kwa utajiri nchini Nigeria, akimiliki dola za Marekani milioni 15.
Hata hivyo, kanisa lake lilikanusha haraka madai hayo na kusema hayana ushahidi.
Kadhalika, Joshua ameondoka duniani huku akiacha upinzani mkubwa dhidi yake kutoka jamii ya makanisa ya Nigeria, ikidaiwa kuwa kiimani hakufungamana na itikadi ya kanisa lolote kama ilivyoada.
Chama cha Makanisa ya Kikristo Nchini Nigeria na Chama cha Wafuasi wa Kipentekoste Nchini Nigeria (The Christian Association of Nigeria and Pentecostal Fellowship Of Nigeria), kwa pamoja hudai kuwa Nabii huyo hakuwa mwanachama wao, na kwamba maudhui katika mafundisho yake yana kasoro.
Mathalani, mmojawapo wa wapinzani wake wakuu ni kiongozi maarufu wa Kikristo, Pasta Chris Okotie, ambaye hukaririwa akimuita kuwa ni "mtoto wa shetani" ('he is a son of the devil').
Hata hivyo, T. B. Joshua alikuwa miongoni mwa wahubiri wenye wafuasi wengi, hususan katika Mabara ya Afrika na Amerika Kusini.
Pia, ni mwenye wafuasi wengi katika mitandao ya kijamii ikiwemo Facebook (wafuasi 3,500,000), na watazamaji takribani 1,000,000 wakiangalia Emmanuel TV kupitia mtandao wa YouTube.
Taarifa iliyotolewa na kanisa lake la Scoan iliyotolewa leo alfajiri inaeleza kwamba TB Joshua alifariki jana Jumamosi Juni 5, 2021 nchini Nigeria muda mfupi baada ya kutoa huduma katika kanisa hilo Jumamosi.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa, Mungu amechukua maisha ya mhudumu wake TB Joshua kulingana na uwezo wake. Amefariki akimuhudumia Mungu.
Taarifa hiyo imetaja sura moja katika biblia inayosema : Mungu muweza hawezi kufanya lolote bila kutoa mipango yake kwa watume wako," Amos 3: 7
"Mungu amemuita nyumbani Nabii TB Joshua kwa mapenzi yake. Nyakati zake za mwisho hapa duniani alizitumia katika huduma ya Mungu. Hiki ndio kitu alichozaliwa kukifanya, alikiishi na kukifia," inaeleza taarifa hiyo.
Hata hivyo, taarifa hiyo haijaeleza chanzo cha kifo chake huku ikiwataka waumini kumwombea mhubiri huyo na kuwapa nafasi wanafamilia kuomboleza kifo cha mpendwa wao.
Siku ya Jumamosi tarahe 5 Juni 2021, mtume TB Joshua alizungumza katika mkutano wa runinga ya Emmanuel.
alisema 'kila jambo na wakati wake, kuna wakati wa kuja hapa kwa maombi na wakati wa kurudi nyumbani baada ya ibada'."
PROPHET TB JOSHUA – JUNE 12th 1963 to JUNE 5th 2021
“Surely the Sovereign LORD does nothing without revealing his plan to his servants the prophets.” – Amos 3:7.
On Saturday 5th June 2021, Prophet TB Joshua spoke during the Emmanuel TV Partners Meeting: “Time for everything – time to come here for prayer and time to return home after the service.”
God has taken His servant Prophet TB Joshua home – as it should be by divine will. His last moments on earth were spent in the service of God. This is what he was born for, lived for and died for.
As Prophet TB Joshua says, “The greatest way to use life is to spend it on something that will outlive it”.
Prophet TB Joshua leaves a legacy of service and sacrifice to God’s Kingdom that is living for generations yet unborn.
"The Synagogue, Church Of All Nations and Emmanuel TV Family appreciate your love, prayers and concern at this time and request a time of privacy for the family,"
Here are Prophet TB Joshua’s last words: “Watch and pray.”
One life for Christ is all we have; one life for Christ is so dear.
Tags
Kimataifa