Tigo yapanda miti 500 kuadhimisha Siku ya Mazingira


Mkurugenzi wa Tigo, Simon Karikari akipanda miti katika viwanja vya Half London, Hai mkoani Kilimanjaro wakati wakiadhimisha Siku ya Mazingira Duniani yenye kauli mbiu “Kurejesha Mfumo wa Ikolojia” kwa kupitia mkakati wao wa #TigoGreenForKili ambao wanarejesha mazingira mazuri yanayozunguka Mlima Kilimanjaro kwa kupanda miti 28,000 mwaka huu.
KILIMANJARO YETU: Urithi wetu uko mikononi mwetu, tunapanda miti kuhakikisha theluji ya mlima huu mrefu barani Afrika haipotei kutokana na shughuli na mabadiliko ya tabia nchi.
Jackson Haule ambaye ni Mwakilishi kutoka Baraza la Mazingira nchini (NEMC) akipanda Mti kama mkakati wa kurejesha mazingira salama mkoa wa Kilimanjaro.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Northern Engineering wakipanda Miti kama ishara ya kurejesha hadhi ya Mlima Kilimanjaro na kuifanya Kilimanjaro ya kijani tena.
HATUNA BUDI “Mabadiliko ya tabia ya nchi na shughuli za kibinadamu yameathiri Mazingira ya Mlima Kilimanjaro hivyo hatuna budi kuchukua tahadhari ndio mana kupitia #TigoGreenForKili tutaweza Kurejesha Mfumo wa Ikologia,"anasema Asifiwe James qambaye ni Mkurugenzi @voewofo
LENGO KUU “Dhima ya mwaka huu #SikuYaMazingiraDuniani yenye kauli mbiu Kurejesha Mfumo wa Ikolojia, inaendana na mkakati wetu wenye lengo la kurejesha hadhi ya mlima Mrefu barani Afrika kupitia mkakati wa #TigoGreenForKili kupanda miti 28,000 mwaka huu” Mkurugenzi wa Tigo, Simon Karikari
“Mazingira ni muhimu & ni chanzo cha uhai wetu, hatuna budi kuyatunzq ili yatutunze hasa kupitia mkakati huu ambao @tigo_tanzania wamekuja nao” Jackson Haule- Mwakilishi kutoka NEMC
AHADI YETU KWENU: “Tunawahakikishia kuilinda vyema miti hii 500 tutakayoipanda katika viwanja vya Half London ili kwa pamoja tuweze kuifanya Kilimanjaro iwe ya kijani tena.” Mkurugenzi wa mamlaka ya Mji wa hai, Noel Nnko

Tumeanza rasmi maadhimisho ya siku ya mazingira duniani yenye kauli mbiu “Kurejesha Mfumo wa Ikolojia”. Kupitia mkakati wa #TigoGreenForKili  tumedhamiria kurejesha mazingira mazuri yanayozunguka Ml. Kilimanjaro kwa kupanda miti 28,000 mwaka huu. Kupitia michango mbalimbali kutoka kwa wadau mbalimbali tumeweza na tunaendelea kupanda miti katika maeneo mbalimbali mkoa wa Kilimanjaro.Tunapongeza na kuwashukuru wadau wetu wote walioitikia wito huu
Mkurugenzi wa Tigo, Simon Karikari akipanda miti katika viwanja vya Half London, Hai, Kilimanjaro

Tunaadhimisha Maadhimisho ya siku ya mazingira duniani yenye kauli mbiu “Kurejesha Mfumo wa Ikolojia” kwa kupitia mkakati wetu wa #TigoGreenForKili tunarejesha mazingira mazuri yanayozunguka Ml. Kilimanjaro kwa kupanda miti 28,000 mwaka huu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news