TUME:WATUMISHI WA UMMA TEKELEZENI MAJUKUMU YENU KWA KUZINGATIA SHERIA

Na Tume ya Utumishi wa Umma

Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma, Bwana Nyakimura Muhoji amewataka Waajiri, Mamlaka za Ajira, Mamlaka za Nidhamu pamoja na Watumishi wote wa Umma kuhakikisha wakati wote wanatekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu, Miongozo na Maelekezo halali yanayotolewa na Serikali.

Bwana Muhoji amesema hayo katika taarifa aliyoitoa kwa umma kuwa, Tume ya Utumishi wa Umma itasikiliza watumishi wa umma na wadau wake wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoanza kesho Jumatano tarehe 16 hadi 23 Juni, 2021.

"Tume katika maadhimisho ya mwaka huu  imeandaa utaratibu ambapo Maafisa wa Tume watapokea na kusikiliza kero na malalamiko ya watumishi wa umma kuhusu masuala mbalimbali ya kiutumishi.  

"Kuanzia Jumatano tarehe 16 hadi 18 Juni, 2021 Maafisa wa Tume watakuwa Wilayani Kisarawe, Mkoani Pwani na tarehe 21-23 Juni, 2021 watakutana na wadau katika Ofisi ya Tume iliyopo Mtaa wa Luthuli, Jijini Dar es Salaam," amesema Bwana Muhoji. 

Bwana Muhoji ametoa wito kwa watumishi wa umma na wadau waliopo Kisarawe na Dar es Salaam kufika kwa tarehe hizi mahsusi zilizopangwa ili waweze  kuhudumiwa na Maofisa wa Tume kuweza kuzitafutia ufumbuzi  changamoto zinazowakabili kiutendaji.

"Watumishi wa umma na wananchi watakaoshindwa kufika amesema wanaweza kuwasilisha kero na malalamiko yao kwa kutuma barua pepe kwa anuani ya secretary@psc.go.tz au kupiga simu namba 0738 166 70," amesema. 

Kaulimbiu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2021 ni: Kuheshimu tofauti ya nyenzo za kuimarisha misingi ya utawala wa umma ulio adilifu
Kazi kubwa ya Tume ya Utumishi wa Umma ni kufuatilia na kuhakikisha kuwa Rasilimali Watu katika Utumishi wa Umma inasimamiwa na kuendeshwa kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu.




Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma, Bwana Nyakimura Muhoji 

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news