Mhandisi wa Mitambo, Vicent Magari kutoka Kampuni ya Gesi (GASCO) ambayo ni Kampuni Tanzu ya Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini ( TPDC) akitoa ufafanuzi kwa baadhi ya wakuu wa Jeshi la Polisi wilaya kutoka mkoani Dar es Salaam, Mkuranga, Rufiji na Kilwa inakopita miundombinu ya gesi asilia baada ya kutembelea BVS1( Block Valve Station) na PRS iliyopo Msijute mkoani Mtwara kwa ajili ya kujifunza na kupata elimu ya miundombinu ya gesi asilia. (Na Mpigapicha Wetu).
Wakuu wa Jeshi la Polisi wa Wilaya za Dar es Salaam,Mkuranga, Rufiji na Kilwa inakopita miundombinu ya gesi asilia leo Tarehe 08/06/2021 wamepata wasaa wa kutembelea BVS1( Block Valve Station) na PRS iliyoko Msijute Mtwara kwa ajili ya kujifunza na kupata elimu ya miundombinu ya gesi asilia.
Vilevile, Wakuu hao wa Polisi waliweza kujionea jinsi miundombinu ya gesi asilia majumbani ilivyounganisha kwenye mojawapo ya nyumba 125 za Bandari Mtwara zinazotumia gesi asilia kama nishati ya kupikia.
Aidha, ziara hiyo ya kujifunza kwa Wakuu hao inaendelea kwa siku tatu mkoani Mtwara kwenye visima vya gesi asilia Mnazibay Msimbati na kituo cha kusafirisha gesi Madimba
Tags
Habari