Wanawake 59 wajengewa uelewa kuhusu ukatili wa kijinsia Butiama

NA FRESHA KINASA

Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Butiama mkoani Mara, Josiah Saoke amezindua mafunzo ya siku mbili ya Ukatili wa Kijinsia kwa Wanawake 59 kutoka vijiji vya wilaya hiyo.
Wanawake 59 Kutoka vijiji vya Wilaya ya Butiama wakifuatilia mafunzo kutoka kwa wawezeshaji wa Shirika la Hope for Girls and Women Tanzania. Pia wanawake hao wamepewa simu bure kila mmoja kupambana na ukatili wa kijinsia. (Picha na Diramakini Blog).

Ambapo mafunzo hayo yanaendeshwa na Shirika la Hope for Girls and Women Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la ATFGM Masanga la wilayani Tarime kuanzia leo Juni 17 hadi 18, 2021 kwa lengo la kuwajengea uelewa katika kukabiliana na vitendo vya kikatili katika maeneo yao.
Mkurugenzi wa Shirika la Hope for Girls and Women Tanzania, Rhobi Samwelly akifafanua jambo wakati wa semina iliyoandaliwa na shirika lake kwa kushirikiana na ATFGM Masanga la wilayani Tarime na kufanyikia Nyumba Salama Kiabakari Butiama.

Aidha, wanawake hao 59 kila mmoja amekabidhiwa simu janja bure, ambayo ataitumia kutoa taarifa ya matukio ya kikatili kutoka katika kijiji chake. Ambapo simu hizo zimetolewa na Shirika la Kimataifa la UNFPA zikiwa 210 ambapo kati ya hizo simu 59 kwa ajili ya Shirika la Hope for Girls and Women Tanzania na 151 kwa Shirika la ATFGM Masanga la wilayani Tarime Mkoa wa Mara zote zikiwa na thamani ya shilingi Milioni 21.

Akizungumza leo Juni 17, 2021 wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo yaliyofanyika Kituo cha Nyumba Salama Kiabakari Wilaya ya Butiama, Saoke amewataka wanawake hao kwenda kuitumia elimu hiyo katika kuwaelimisha wengine ambao hawakupata fursa ya kuhudhuria ili kuhakikisha ukatili unapungua kwa kiwango kikubwa ndani ya wilaya hiyo sambamba na kuibua matukio ya kikatili ambayo bado hayaripotiwi katika maeneo yao.
Mkurugenzi wa Shirika la Hope for Girls and Women Tanzania, Rhobi Samwelly akifafanua jambo wakati wa semina iliyoandaliwa na shirika lake kwa kushirikiana na ATFGM Masanga la wilayani Tarime na kufanyikia Nyumba Salama Kiabakari Butiama.
Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Butiama, Josiah Saoke akifafanua jambo wakati wa semina iliyoandaliwa na Shirika la Hope for Girls and Women Tanzania kwa kushirikiana na ATFGM MASANGA la wilayani Tarime.
Amesema, matukio ya ukatili wa kijinsia ya aina mbalimbali bado yapo kwenye jamii, lakini bado hayafichuliwi, hivyo amehimiza wayaripoti katika vyombo vya kisheria na katika shirika kwa njia ya simu janja za kisasa ambazo wamepewa bure. Huku wanaume ambao pia wamekuwa wakifanyiwa ukatili akiwahimiza kujitokeza kuripoti vitendo hivyo bila kuvifumbia macho kwa kuogopa kuchekwa.

"Vitendo vya ukatili wa kijinsia bado vipo katika jamii tunayoishi. Niwaombe ninyi ambao mmepata fursa ya kuhudhuria mafunzo haya mkienda katika maeneo yenu mkawe chachu ya kuleta mabadiliko. Pia kuna simu ambazo zimeunganishiwa na APP Maalum ambayo mtaitumia kuripoti vitendo hivyo, kazitumieni simu hizo kwa manufaa lengo ni kupunguza ukatili ambao hufifisha juhudi za maendeleo kuanzia katika familia,"amesema Saoke.

Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii Wilaya ya Butiama, Johnson Adela amesema kuwa, wanawake ni nyenzo muhimu katika maendeleo hivyo amewahimiza kuwa sehemu muhimu ya kuisaidia Serikali kupambana na ukatili ili kuongeza uzalishaji mali katika familia.
Mkurugenzi wa Shirika la Hope for Girls and Women Tanzania, Rhobi Samwelly amesema kuwa shirika hilo limekuwa likitumia utaratibu wa kuwapa kina mama simu janja bure baada ya kuwapa elimu ya ukatili wa kijinsia kwa lengo la kuimarisha ufanisi katika kumaliza vitendo mbalimbali vya ukatili ikiwemo ukeketaji, ubakaji, vipigo kwa kinamama pamoja na ndoa za utotoni.

Aidha, Rhobi amesema kuwa, shirika hilo limekuwa likiendelea na utaratibu wa utoaji wa elimu kwa makundi mbalimbali kuhusu madhara ya ukatili wa kijinsia, aina za ukatili pamoja na namna ya kuwajengea uelewa wananchi katika kufichua wananojihusisha na vitendo hivyo kauanzia ngazi ya familia na maeneo wanakoishi.
Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Butiama Josiah Saoke akifafanua jambo wakati wa semina iliyoandaliwa na Shirika la Hope for Girls and Women Tanzania kwa kushirikiana na ATFGM MASANGA la wilayani Tarime.
Naye Yustina Marwa Ngega kutoka Kijiji cha Masurura Wilaya ya Butiama amelishukuru Shirika la Hope for Girls and Women Tanzania kupitia Mkurugenzi wake, Rhobi Samwelly kuwezesha mafunzo hayo ambayo amesema yamemuimarisha namna bora ya kuripoti vitendo vya kikatili ambapo awali hakuwa na ujuzi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news