Watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii watembelea mashamba ya Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda


Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Lusius Mwenda akizungumza na baadhi ya watumishi wa Wizara ya Maliasili na utalii kuhusu utaratibu wa ziara ya mafunzo iliyofanyika jana kwenye mashamba ya Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo Pinda (hayupo pichani) yaliyoko Zinje (Zuzu) nje kidogo ya jiji la Dodoma.
Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo Pinda (katikati) akitoa maelezo kuhusu chakula cha samaki kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Allan Kijazi (kulia) na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Ludovick Nduhiye (kushoto) wakati wa ziara ya mafunzo ya watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii iliyofanyika jana katika mashamba yake yaliyoko Zinje (Zuzu) nje kidogo ya jiji la Dodoma.
Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo Pinda (katikati) akionyesha moja ya bwawa la samaki kwa watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii waliotembelea mashamba yake yaliyopo Zinje (Zuzu) nje kidogo ya jiji la Dodoma jana. Kushoto kwake ni Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Allan Kijazi (kulia) na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Ludovick Nduhiye (kulia kwake) wakifuatilia.
Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo Pinda (katikati) akitoa maelezo kuhusu shamba la zabibu kwa watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii (hawapo pichani) waliotembelea mashamba yake yaliyopo Zinje (Zuzu) nje kidogo ya jiji la Dodoma jana. Kulia ni Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Allan Kijazi (kulia) na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Ludovick Nduhiye (kushoto).
Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo Pinda (kulia) akitoa maelezo kuhusu kilimo cha Green House kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Allan Kijazi (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Ludovick Nduhiye (katikati) wakati wa ziara ya mafunzo kwa vitendo ya watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii waliotembelea mashamba yake yaliyopo Zinje (Zuzu) nje kidogo ya jiji la Dodoma jana.(Picha zote na Happiness shayo-WMU).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news