Na Mathias Canal, WK
Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda amesema Serikali haitawavumilia wawekezaji waliochukua mikopo ya kimagumashi na kutelekeza mashamba 16 ya maua na mboga mboga wilayani Arumeru mkoani Arusha.
Waziri wa Kilimo, Prof. Adolf Mkenda akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi Kilele ya mazao ya maua na mboga mboga (TAHA), Dkt. Jacqueline Mkindi wakikagua mashamba ya maua na mboga mboga wilayani Arumeru Mkoani Arusha, tarehe 12 Juni 2021. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kiimo).
Waziri Mkenda ameyasema hayo tarehe 12 Juni 2021 wakati alipofanya ziara ya kikazi mkoani humo alipotembelea na kukagua mashamba yenye ukubwa wa Hekari 1950 wilayani Arumeru huku akiongeza kuwa wawekezaji hao walichukua mikopo lakini wameshindwa kurejesha mikopo hiyo na kuisababishia serikali hasara tangu mwaka 2018.
Waziri Mkenda amesema kuwa Mashamba hayo kwa mwaka mmoja yanapoteza zaidi ya fedha za kigeni Dola za Kimarekani Milioni 24 Sawa na ajira 6700 kwa mwaka.
“Serikali itahakikisha mashamba hayo yanarudi katika hali yake ya uzalishaji huku taratibu nyingine za kurejesha mikopo hiyo ikiendelea,"amebainishameProf. Mkenda na kuongeza kuwa,
Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda akikagua miundombinu ya shamba la maua na mboga mboga la Kiliflora wilayani Arumeru Mkoani Arusha, tarehe 12 Juni 2021.
“Mashamba haya ya maua yamefungwa kutokana na wawekezaji waliochukua mikopo ya kimagumashi, mashamba haya yametelekezwa na yanaharibika wakati nchi hii tunahitaji fedha za kigeni na ajira kwa wananchi wetu, hivyo hatutamvumilia wala kumtetea aliyechukua mkopo kimagumashi,"amesema Prof. Mkenda.
Prof. Mkenda ameongeza kuwa ni vigumu kuamini kampuni ambayo ilikuwa ikifanya biashara vizuri ingepewa mkopo halali na kuchukua mkopo wote hatimaye wakashindwa kuendeleza mashamba hayo. “Lazima kuna mchezo ulifanyika baina ya aliyetoa mkopo na aliyepokea mkopo,”amesema Profesa Mkenda.
Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe Jerry Muro pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi Kilele ya mazao ya maua na mboga mboga (TAHA), Dkt. Jacqueline Mkindi akikagua miundombinu ya shamba la maua na mboga mboga la Hortanzia wilayani Arumeru Mkoani Arusha, tarehe 12 Juni 2021.
“Wizara tunaenda kujenga hoja ili haya mashamba yaliyotelekezwa yanarudi katika hali yake ya kawaida ya uzalishaji na kama kuna wawekezaji wengine tuwape wayaendeleze ,” Amesema Prof. Mkenda
Akizungumzia mashamba hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi Kilele ya mazao ya maua na mboga mboga (TAHA), Dkt. Jacqueline Mkindi amesema kuwa utelekezwaji wa mashamba hayo yamepoteza zaidi ya ajira 6700 za Watanzania na kuisababishia Serikali hasara kubwa ya kimapato.
Dkt. Mkindi ameeleza kuwa mashamba hayo yalikuwa yakiuza maua na bidhaa nyingine kwenye masoko ya Kimataifa na kuiomba Serikali kuona namna ya kuyarejesha kufanya kazi mashamba hayo ili yaweze kuongeza pato la Taifa na ajira kwa vijana na Watanzania kwa ujumla.
Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda akiwa ameambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi Kilele ya mazao ya maua na mboga mboga (TAHA), Dkt. Jacqueline Mkindi walipotembelea shamba la maua na mboga mboga la Rijk Zwaan wilayani Arumeru Mkoani Arusha tarehe 12 Juni 2021. Waziri wa Kilimo, Mhe Prof. Adolf Mkenda akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe Jerry Muro pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi Kilele ya mazao ya maua na mboga mboga (TAHA), Dkt. Jacqueline Mkindi akikagua miundombinu ya shamba la maua na mboga mboga la Kiliflora wilayani Arumeru Mkoani Arusha, tarehe 12 Juni 2021.
“Tunamshukuru Waziri kutembelea haya mashamba ambayo yametelekezwa, haya mashamba yalikuwa yanatoa maua ambayo yalikuwa takiuzwa kwenye masoko ya Kimataifa hivyo kufungwa kwa mashamba haya tumepoteza ajira takribani 6700 na kwa mwaka mzima tumepoteza fedha za kigeni wastani wa dola za Kimarekani milioni 24,"amesema Dkt. Mkindi.
Aidha, Dkt. Mkindi aliongeza kuwa, “Tunatamani siku moja kuona haya mashamba yanarudi katika uzalishaji na tuko tayari kutoa ushirikiano kwa serikali kuona ni namna gani ya kufufua haya mashamba na kutoa ajira kwa Watanzania,”
Tags
Habari