Waziri wa Fedha na Mipango,Dkt.Mwigulu Nchemba amewsilisha hotuba hiyo leo Juni 10, 2021 bungeni jijini Dodoma.
Mheshimiwa Mwingulu amesema kuwa, bajeti ya Serikali kwa mwaka 2021/22 ni ya kwanza katika utekelezaji wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26 wenye dhima ya “Kujenga Uchumi Shindani na Viwanda kwa Maendeleo ya Watu”. Bajeti hii itajielekeza katika utekelezaji wa vipaumbele mbalimbali.
“Vipaumbele vilivyoainishwa katika maeneo matano ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2021/22,Maeneo hayo ni Kuchochea uchumi shindani na shirikishi; kuimarisha uwezo wa uzalishaji viwandani na utoaji huduma ili kuongeza thamani ya mazao ya kilimo; kukuza uwekezaji na biashara; kuchochea maendeleo ya watu; na kuendeleza rasilimali watu.
Waziri Mwigulu ameeleza kuwa ili kuwa na uchumi shindani na shirikishi, Serikali itajielekeza katika kugharamia miradi ambayo itajikita katika: Kujenga jamii yenye uwezo wa kushindana kikanda na kimataifa; kusimamia utulivu wa viashiria vya uchumi kwa ujumla.
Amefafanua kuwa, kuimarisha mazingira ya biashara na uwekezaji,kuchochea uvumbuzi na uhawilishaji wa teknolojia kutoka nje na kuendeleza miundombinu na huduma za reli, barabara za kufungua fursa za kiuchumi, kuunganisha nchi jirani, kupunguza msongamano mijini na barabara za vijijini, madaraja, usafiri wa majini na angani, mageuzi ya TEHAMA pamoja na kutekeleza mradi wa Tanzania ya Kidijitali, nishati, bandari na viwanja vya ndege.
Eneo hili limetengewa jumla ya shilingi trilioni 7.44 ikijumuisha shilingi trilioni 3.13 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya kielelezo.
Pamoja na mambo mengine ameitaja miradi mingine ya kielelezo itakayotekelezwa ni: Kuboresha Shirika la Ndege Tanzania (ATCL); Makaa ya Mawe – Mchuchuma na Chuma – Liganga ikijumuisha ujenzi wa reli ya kiwango cha Kimataifa (Standard Gauge Railway) kutoka Mtwara hadi Mbamba Bay na matawi ya Mchuchuma na Liganga; Bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima (Uganda) hadi Tanga (Tanzania); Mradi wa Kuchakata Gesi Asilia kuwa Kimiminika (LNG) – Lindi; Mradi wa Kufua Umeme wa Maji – Ruhudji MW 358.
“Mradi wa Kufua Umeme wa Maji – Rumakali MW 222; Uchimbaji wa madini ya Nickel; Ujenzi wa Madaraja Makubwa na Barabara za Juu za Daraja la Kigongo – Busisi (Mwanza), Tanzanite (Dar es Salaam) na Interchange ya Kamata (Dar es Salaam); Bandari ya Uvuvi (Mbegani) na Ununuzi wa Meli za Uvuvi; Kiwanda cha Sukari Mkulazi; Utafutaji wa mafuta katika vitalu vya Eyasi Wembere na Mnazi Bay North; Mradi wa Magadi Soda – Engaruka; Kuongeza Rasilimali Watu yenye Ujuzi Adimu na Maalumu (Ujuzi wa Kati na Wabobezi) kwa Maendeleo ya Viwanda na Ustawi wa Jamii; na kuendeleza Kanda Maalumu za Kiuchumi,"amesema.
Amesema kuwa, katika eneo la kuimarisha uwezo wa uzalishaji viwandani na utoaji huduma, msukumo utawekwa kwenye miradi ya viwanda inayolenga kuongeza thamani ya mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi. Katika eneo hili, kipaumbele ni pamoja na Kujenga na kukarabati miundombinu ya umwagiliaji na uhifadhi wa mazao ya kilimo; kuimarisha vituo vya utafiti na huduma za ugani;kuongeza thamani ya mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi; kuhakikisha upatikanaji wa masoko ya ndani na nje ya nchi; kuboresha huduma za uhimilishaji mifugo; na kujenga machinjio ya kisasa na minada ya mifugo.
Mheshimiwa Mwingulu akisoma makadirio hayo ya bajeti akiwa ametumia saa 2:20, ametaja maeneo mbalimbali ambayo bajeti hiyo imegusa ikiwemo maslahi ya watumishi, waendasha bodaboda, mikopo kwa elimu ya juu, kilimo na mengine mengi.
Pia amesema kwamba, anapendekeza Serikali kutenga sh. bilioni 449 kwa ajili ya kuwapandisha vyeo watumishi 92,619.
Vicheko kwa madiwani, maafisa tarafa, watendaji
Waziri Mwigulu amesema, anapendekeza kuanzia mwaka 2021/22, Serikali Kuu ianze kulipa posho za kila mwezi za madiwani moja kwa moja tena kwenye akaunti zao kwa halmashauri zote zenye uwezo mdogo kimapato.
Kwa upande wa halmashauri 16 zenye uwezo mkubwa wa kimapato (Daraja A) amesema zitaendelea kutumia mapato yake ya ndani kulipa posho za madiwani kupitia kwenye akaunti zao.
Waziri Mwigulu amesema, anapendekeza kupunguza adhabu zinazotolewa chini ya Sheria ya Usalama Barabarani SURA 168 kwa makosa ya Pikipiki na Bajaji kutoka sh. 30,000 za sasa hadi shilingi 10,000 kwa kosa moja.
"Ni mfadhaiko kwake na familia nzima. Kwa hatua ya maendeleo ambayo nchi yetu imepata katika sekta mbalimbali hali hii haipendezi na haitakiwi kuendelea. Serikali inakusudia kuchukua hatua za kuhakikisha kuwa inaongeza bajeti ya mikopo ya elimu ya juu ili kuwanufaisha vijana wote wenye sifa za kupata mkopo," amesema Mwigulu.
Sheria ya Petroli, SURA 392
Kwa upande wa sheria hiyo amesema, anapendekeza kufanya marekebisho kwenye Sheria ya Petroli ili kuongeza tozo ya Mafuta ya Taa kutoka sh. 150 hadi sh. 250.
Amesema, lengo la hatua hii ni kupunguza uchakachuaji wa mafuta kufuatia ongezeko la ushuru wa mafuta kwenye dizeli na petroli.
Aidha, Marekebisho hayo yataainishwa katika Muswada wa Sheria ya Fedha ya mwaka 2021 na Matangazo ya Serikali (Government Notices).
Amesema, katika jitihada za kupanua wigo wa vyanzo vya rasilimali fedha, Serikali itaangalia uwezekano wa kutumia Hati Fungani zitakazotolewa na Halmashauri za Manispaa na Majiji kama njia mbadala ya kupata rasilimali fedha kwa ajili ya miradi ya kimkakati.
Amesema hatua hii itapunguza mzigo kwenye Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali hasa kwa Halmashauri zenye miradi ambayo imefanyiwa upembuzi yakinifu na kuwa na uhakika wa uwezo wa miradi hii kujiendesha kwa faida (bankable projects).
"Serikali kwa kushirikiana na Mfuko wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (United National Capital Development Fund - UNCDF) na Mamlaka ya Usimamizi wa Masoko ya Mitaji (Capital Markets and Securities Authority - CMSA) imeanza mchakato wa kuhakikisha kwamba Halmashauri, Manispaa na Majiji yatakayokidhi vigezo na masharti ya matumizi ya Hati Fungani hizi yanaanza kutumia utaratibu huu," amesema.
Kuhusu Zanzibar, Waziri amependekeza kufanya marekebisho ya Sheria ya Kodi ya Ongezeko la
Thamani ili kurudisha utaratibu wa kurejesha VAT kwa bidhaa
zinazonunuliwa Tanzania Bara na kutumika Tanzania Zanzibar. Hii
inatokana na mfumo wa kutoza VAT kwa kiwango cha asilimia sifuri kwa
bidhaa za viwandani pekee kutowanufaisha wafanyabiashara wa Zanzibar
wanaonunua bidhaa na kutozwa VAT Tanzania Bara na kutozwa tena VAT
bidhaa hizo zinapopelekwa Zanzibar.
Aidha, amependekeza marejesho ya
VAT yatakayofanyika kwa bidhaa zinazotoka Tanzania Bara kwenda Zanzibar
yafanyike pia kwa bidhaa zitakazotoka Zanzibar kwenda Tanzania Bara
sambamba na marekebisho ya vifungu husika vya Sheria za VAT kwa pande
zote mbili za muungano. Ili kuwa na ufanisi wa marejesho, maboresho ya
mifumo yatafanyika ili isomane baina ya Tanzania Bara na Zanzibar.
Kutokana na utaratibu huu, kiwango cha asilimia sifuri ya Kodi ya
Ongezeko la Thamani kilichokuwa kinatozwa bidhaa hizo kitasitishwa.
Amesema kuwa, kutokana na hatua
zote za Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa ujumla zinatarajiwa kupunguza
mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 55,499.97.
Kuhusu Sheria ya Kodi ya
Mapato,Waziri amependekeza kufanya marekebisho kwenye Sheria ya Kodi ya
Mapato, Kupunguza kiwango cha chini cha kutoza Kodi ya Mapato
yanayohusiana na ajira kutoka asilimia 9 hadi asilimia 8.
Waziri amesema kuwa, jumla ya Mapato Kiwango cha Kodi sasa
Mapato ya jumla yasiyozidi shilingi 3,240,000/=
Mapato ya Jumla yanayozidi shilingi 3,240,000/= lakini hayazidi
shilingi.6,240,000/=
Mapato ya Jumla yanayozidi shilingi 6,240,000/= lakini hayazidi shilingi 9,120,000/=
Mapato ya Jumla yanayozidi shilingi 9,120,000/= lakini hayazidi shilingi 12,000,000/=
Mapato ya Jumla yanayozidi shilingi 12,000,000/=
Jedwali Na. 1B Viwango vinavyopendezwa
Mapato ya jumla yasiyozidi shilingi 3,240,000/=
Mapato ya Jumla yanayozidi shilingi 3,240,000/= lakini hayazidi shilingi 6,240,000/=
Mapato ya Jumla yanayozidi shilingi 6,240,000/= lakini hayazidi shilingi 9,120,000/=
Mapato ya Jumla yanayozidi shilingi 9,120,000/= lakini hayazidi shilingi 12,000,000/=
Mapato ya Jumla yanayozidi shilingi 12,000,000/=
Hakuna kodi
9% ya kiasi kinachozidi shilingi 3,240,000/=
Shilingi 270,000/= jumlisha 20% ya kiasi kinachozidi shilingi 6,240,000/=
Shilingi 846,000/= jumlisha 25% ya kiasi kinachozidi shilingi 9,120,000/=
Shilingi 1,566,000/= jumlisha 30% ya kiasi kinachozidi shilingi
12,000,000/=
Hakuna kodi
8% ya kiasi kinachozidi shilingi 3,240,000/=
Shilingi 240,000/= jumlisha 20% ya kiasi kinachozidi shilingi 6,240,000/=
Shilingi 816,000/= plus 25% ya kiasi kinachozidi shilingi 9,120,000/=
Shilingi.1,536,000/= plus 30% ya kiasi kinachozidi shilingi
12,000,000/=
Pia amesema kuwa, hatua hiyo
inachukuliwa ikiwa ni dhamira ya Serikali ya muda mrefu kuwapunguzia
mzigo wa Kodi wafanyakazi. Hatua hii inatarajiwa kupunguza mapato kwa
shilingi milioni 14,178.06,kwa Kutoa msamaha wa Kodi ya Mapato kwenye
hatifungani za Serikali. Sheria ya Kodi ya Mapato ilisamehe Kodi ya
Mapato kwenye hatifungani kwa mwaka 2002/03 pekee. Lengo la hatua hii
ni kuhakikisha soko la ndani la hatifungani linaendelea kusaidia
kugharamia miradi ya Serikali.
Amesema kuwa, kumekuwepo na
ukiritimba katika kupokea fedha za kutoka kwa nchi wahisani
zinazokwenda kutekeleza Miradi ya maendeleo. Napendekeza Kurejesha
utaratibu wa Mamlaka ya Waziri mwenye dhamana ya Fedha kutoa msamaha
kwa kutoa tangazo la Serikali (GN) bila sharti la kupata ridhaa ya
Baraza la Mawaziri kwa miradi inayotekelezwa kwa fedha za wafadhili
kupitia mikataba iliyoingiwa baina ya nchi hizo na Serikali yenye
kifungu kinachoruhusu msamaha wa kodi ya mapato.
‘’ Lengo la marekebisho haya ni
kuharakisha utekelezaji wa madi inayofadhiliwa kwa misaada na mikopo
yenye gharama nafuu ambayo utekelezaji wake umekuwa ukichelewa
kusubiri ridhaa ya Baraza la Mawaziri,’’amesema.
Amesema kuwa Kutoza Kodi ya Zuio
kwa kiwango cha asilimia mbili kwenye malipo yanayohusisha mauzo ya
mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi yanapouzwa kwenye kampuni na mashirika
yote yanayojihusisha na usindikaji na ununuzi wa mazao,Kwa sasa,
Taasisi za Serikali pekee kama vile (Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya
Chakula (NFRA) ndizo zinakata kodi hiyo kwa kiwango cha asilimia mbili.
Aidha,amesema kuwa pendekezo hilo
halitahusisha wakulima wadogo na wale wanaouza mazao yao kwenye masoko
ya msingi (AMCOS) na kwenye magulio. Lengo la pendekezo hili ni
kuweka usawa katika utozaji wa kodi kwa Kampuni zote zinazojishughulisha
na mazao ya Kilimo, mifugo na uvuvi.Pendekezo hilo linatarajiwa
kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 43,954.2;
(v) Kufanya maboresho ya Sheria ya
Kodi ya Mapato ili kuwezesha ukokotoaji wa gharama za uchakavu kwa
kiwango maalum cha asimilia tano (5) kwenye gharama za mali za ujenzi
wa bomba la mafuta (EACOP). Lengo la pendekezo hili ni kuwianisha
gharama za uchakavu na muda wa matumizi wa bomba husika kwa kuzingatia
masharti ya mkataba uliosainiwa baina ya Serikali za Uganda na
Tanzania;
(vi) Kuweka utaratibu maalum wa
utozaji kodi kwa wachimbaji wadogo wa madini wenye mauzo ghafi
yasiyozidi shilingi milioni 100 kwa mwaka kama ifuatavyo: –
(a) Kutoza kodi wachimbaji wadogo
wa madini kwa kiwango mfuto cha asilimia 3 kwenye thamani ya mauzo ya
madini pindi yanapopatikana;
(b) Kuweka muda wa ulipaji kodi
kuwa ni wakati wanapouza madini na kulipa mrabaha kwenye Tume ya Madini
au maeneo maalum yaliyoanzishwa chini ya sheria ya madini;
(c) Kuweka wajibu kwa mchimbaji
mdogo wa madini kama mwajiri wa kukata kodi ya mapato ya ajira kutoka
kwa wafanyakazi wake pale tu madini yatakapokuwa yamepatikana na
kuuzwa katika masoko ya madini;
(d) Kuweka muda maalum wa kulipa
kodi ya zuio ya ajira kuwa ni wakati mchimbaji mdogo anapouza madini
na kulipa mrabaha katika masoko ya madini au vituo vingine vya uuzaji
na ununuzi wa madini vinayotambuliwa na Tume ya Madini.
(e) Kuweka kiwango cha kodi cha
mapato ya ajira (PAYE) cha asilimia 0.6 ya thamani ya mauzo ya madini
ambayo italipwa na mwajiri (mchimbaji mdogo wa madini) kwa niaba ya
wafanyakazi wake.
Amesema kuwa Lengo la mapendekezo
hayo ni kurahisisha utozaji na ulipaji wa kodi kutoka kwa wachimbaji
wadogo wa sekta ya madini ili kuongeza mchango wa kodi ya mapato kutoka
kwenye sekta hiyo. Hatua hizi kwa pamoja zinatarajia kuongeza mapato
ya Serikali shillingi
milioni 29,776.14
Kwa upande wa Sheria ya Ushuru wa
Bidhaa, amesema kuwa Kwa mujibu wa kifungu cha 124(2) cha Sheria ya
Ushuru wa Bidhaa, marekebisho ya viwango maalumu vya ushuru wa bidhaa
(specific duty rates) kwa bidhaa zote zisizo za petroli yanaweza
kufanyika kila mwaka ili kuvihuisha na mfumuko wa bei na viashiria
vingine vya uchumi jumla.
Hata hivyo, kutokana na biashara
za bidhaa hizi kuzorota kutokana na athari za kiuchumi
zilizosababishwa na ugonjwa wa Covid-19, amependekeza kutofanya
mabadiliko ya viwango maalumu vya ushuru wa bidhaa kwa bidhaa zote
zisizo za petroli isipokuwa vinywaji vikali na bia zitakazotengenezwa
kwa kutumia shayiri iliyozalishwa hapa nchini.
Amependekeza pia kufanya
marekebisho ya Ushuru wa bidhaa kwenye bidhaa kwa Kupunguza Ushuru wa
Bidhaa kwenye bia zinazotengenezwa kwa kutumia shayiri iliyozalishwa
hapa nchini kutoka shilingi 765 kwa lita za sasa hadi shilingi 620 kwa
lita.
Lengo la mapendekezo hayo ni
kuchochea kilimo cha shayiri hapa nchini kwa Kuanza kutoza Ushuru wa
bidhaa wa asilimia 10 kwenye nyuzi na kamba za plastiki (synthetic
fibres) zinazoingizwa kutoka nje ya nchi au kuzalishwa hapa nchini
zinazotambuliwa kwa heading 55.11 na 56.07 isipokuwa zile zinazotumika
kwenye
Uvuvi (HS Code 5607.50.00).
Marekebisho hayo ni kulinda
mazingira na kuchochea uzalishaji na matumizi ya bidhaa za katani.
Hatua hii inatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa shilingi milioni
2,644
(iii) Kuanzisha tozo ya ushuru wa
bidhaa kwa kiwango cha asilimia 10 kwenye pikipiki zilizotumika kwa
zaidi ya miaka 3 zinazoingizwa nchini zinazotambuliwa kwa HS Code
8711. Lengo la marekebisho haya ni kudhibiti uingizaji wa pikipiki
chakavu na kulinda mazingira. Hatua hii inatarajiwa kuongeza ya mapato
ya Serikali kwa shilingi milioni 263.7.
Hatua za kutoza Ushuru wa Bidhaa
kwenye bidhaa zisizo za petroli kwa ujumla wake zinatarajiwa kuongeza
mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 2,907.7.
Kuhusu Sheria ya Usimamizi wa
Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya mwaka 2004 Waziri huyu
amesema katika Kikao cha Mawaziri wa Fedha wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki cha Maandalizi ya Bajeti kilichofanyika tarehe 7 Mei 2021
mjini Arusha, walipendekeza kufanya marekebisho ya Viwango vya Pamoja
vya Ushuru wa Forodha na Sheria ya Usimamizi wa Forodha ya Jumuiya ya
Afrika Mashariki (EAC Customs Management Act, 2004) kwa mwaka wa fedha
2021/22.
Amesema kuwa Mapendekezo hayo
yanalenga katika Kuboresha Maisha ya Watu Kupitia Maendeleo ya Viwanda
na Kutengeneza Ajira kwa ajili ya Ustawi wa Pamoja wa Watu wa Jumuiya
ya Afrika Mashariki.
Amesema kuwa mapendekezo ya
Mawaziri wa Fedha ya kufanya marekebisho kwenye Viwango vya Pamoja vya
Ushuru wa Forodha yanahusisha hatua mpya na zinazoendelea ambazo
zimekuwa zikitekelezwa katika Mwaka wa Fedha 2020/21.
Hatua hizo ni kama Mapendekezo
ya hatua mpya za Viwango vya Ushuru wa Forodha ni Kupunguza Ushuru wa
Forodha kutoka asilimia 25 hadi asilimia 10 kwa mwaka mmoja kwenye
mabasi ya abiria yanayotambulika kwa HS Codes 8702.10.99 na 8702.20.99
yanayoingizwa nchini kwa ajili ya mradi wa mwendokasi. Hatua hii
inalenga kupunguza gharama za uingizaji wa mabasi hayo ili kurahisisha
usafiri kwa wananchi;
(b) Kuongeza Ushuru wa Forodha
kutoka asilimia 10 hadi asilimia 25 kwa mwaka mmoja kwenye nyuzi za
pamba (cotton yarn) zinazotambulika kwa Headings 52.05, 52.06 na
52.07. Lengo la hatua ni kulinda viwanda vinavyozalisha bidhaa hiyo na
kuongeza thamani ya zao la pamba (value addition) nchini;
(c) Kuongeza Ushuru wa Forodha
kutoka asilimia 10 hadi asilimia 25 kwa mwaka mmoja kwenye matairi
mapya ya pikipiki (new pneumatic tyres of rubber) yanayotambulika kwa
HS Code 4011.40.00. Lengo la hatua ni kuongea mapato ya Serikali kwa
kuwa matairi haya ni bidhaa zilizokamilika kwa ajili ya mtumiaji;
(d) Kuongeza Ushuru wa Forodha
kutoka asilimia 25 hadi asilimia 35 kwa mwaka mmoja kwenye siagi ya
karanga (peanut butter) inayotambulika kwa HS Code 2008.11.00. Lengo la
hatua ni kulinda wazalishaji wa bidhaa hiyo nchini;
(e) Kupunguza Ushuru wa Forodha
kutoka asilimia 10 hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye nyaya (wire
of other alloy steel) zinazotambulika kwa HS Codes 7229.20.00 na
7229.90.00. Lengo la hatua hii ni kupunguza gharama kwa
Kuhusu wazalishaji wanaotumia
bidhaa hiyo kama malighafi ni Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka
asilimia 25 hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye milk cans
zinazotambulika kwa HS Codes 7310.10.00 na 7310.29.90. Lengo la hatua
hii ni kutoa unafuu kwenye sekta ya maziwa nchini;
(g) Kupunguza Ushuru wa Forodha
kutoka asilimia 10 hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye LABSA
(Organic surface-active agents – Anionic) inayotambulika kwa HS Code
3402.11.00 kwa utaratibu wa duty remission. Lengo la hatua hii ni kutoa
unafuu kwa wazalishaji wa sabuni za unga na maji nchini;
(h) Kupunguza Ushuru wa Forodha
kutoka asilimia 25 au 10 hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye
malighafi za kuchakata ngozi zinazotambulika kwa HS Code 3208.20.00 na
3210.00.10 kwa utaratibu wa duty remission. Lengo la hatua hii ni
kutoa unafuu kwa wachakataji wa ngozi nchini;
(i) Kupunguza Ushuru wa Forodha
kutoka asilimia 25 au 10 hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye
malighafi za kutengeneza mbolea zinazotambulika kwa HS Codes
2710.99.00, 2528.00.00 na 3505.20.00 kwa utaratibu wa duty remission.
Lengo la hatua hii ni kutoa unafuu kwa wazalishaji wa mbolea nchini;
(j) Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye vifungashio vya tumbaku iliyochakatwa
vinavyotambulika kwa HS Code 5310.10.00 kwa utaratibu wa duty
remission. Lengo la hatua hii ni kutoa unafuu kwa wachakataji wa
tumbaku nchini;
(k) Kupunguza Ushuru wa Forodha
kutoka asilimia 25 hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye vifungashio
vya chai iliyochakatwa vinavyotambulika kwa HS Codes 4819.20.90,
5407.44.00 na 3923.29.00 kwa utaratibu wa duty remission. Lengo la
hatua hii ni kutoa unafuu kwa wachakataji wa chai (tea blenders)
nchini;
(l) Kupunguza Ushuru wa Forodha
kutoka asilimia 25 hadi asilimia 10 kwa mwaka mmoja kwenye malighafi ya
kutengeneza masufuria ya aluminium inayotambulika kwa HS Code
7606.92.00 kwa utaratibu wa duty remission. Lengo la hatua hii ni kutoa
unafuu kwa watengenezaji wa masufuria hayo nchini;
(m) Kupunguza Ushuru wa Forodha
kutoka asilimia 25 hadi asilimia 10 kwa mwaka mmoja kwa waunganishaji
wa pikipiki za matairi matatu bila kujumuisha fremu kwa kuwa
zinatengenezwa hapa nchini (CKD for three-wheel motorcycles excluding
chassis and its components) zinazotambulika kwa HS Code 8704.21.90 kwa
utaratibu wa duty remission. Lengo la hatua hii ni kutoa unafuu kwa
waunganishaji wa pikipiki hizo nchini ili kurahisisha usafirishaji wa
mizigo;
(n) Kupunguza Ushuru wa Forodha
kutoka asilimia 25 au 10 hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye
malighafi za kutengeneza mabomba ya plastiki (glass reinforced plastic
pipes) zinazotambulika kwa HS Codes 3920.61.10, 7019.39.00,
7019.31.00, 6006.90.00, 7019.12.00,
3920.10.10, 4016.93.00, na 3907.91.00 kwa utaratibu wa duty remission.
Amesema kuwa Lengo la hatua hii ni
kutoa unafuu kwa watengenezaji wa mabomba hayo nchini ili kupunguza
gharama za uzalishaji na kuwezesha ujenzi wa miundombinu ya maji; na
(o) Nchi Wanachama wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki zimekubaliana kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka
asilimia 10 hadi asilimia 0 kwenye mabati (Flat-rolled products of
other alloy steel, of a width of 600mm or more, not further worked than
hot-rolled, in coils) yanayotambulika kwa HS Code 7225.30.00. Lengo la
hatua hii ni kupunguza gharama kwa wazalishaji wanaotumia bidhaa hiyo
kama malighafi.
(ii) Mapendekezo ya kuendelea na utekelezaji wa Viwango vya Ushuru wa Forodha vya mwaka 2020/21 ni kama ifuatavyo:
(a) Kupunguza Ushuru wa Forodha
hadi asilimia 0 kutoka viwango vya awali vya asilimia 10 na asilimia 25
kwa mwaka mmoja kwenye malighafi zinazotumika katika uzalishaji wa
vifaa maalum vinavyotumika katika kupambana na ugonjwa wa homa kali ya
mapafu (UVIKO-19) vikiwemo Barakoa (Masks), kipukusi
(sanitizer), mashine za kusaidia
kupumua (ventilators), na mavazi maalum ya kujikinga yanayotumiwa na
madaktari na wahudumu wa afya (PPE). Msamaha huu utatolewa kwa utaratibu
wa “duty remission”. Hatua hii inalenga kutoa unafuu wa uzalishaji wa
vifaa hivyo hapa nchini ili kuongeza kasi katika kupambana na ugonjwa
huo;
(b) Kupunguza Ushuru wa Forodha
kutoka asilimia 10 hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye mashine za
kielektroniki zinazotumika kukusanya mapato ya Serikali (Cash
registers, Electronic Fiscal Device (EFD) Machines and Point of Sale
(POS) machines zinazotambulika katika HS Code 8470.50.00 na 8470.90.00.
Lengo la hatua hii ni kuhamasisha matumizi ya vifaa hivi katika
kuhasibu mapato ya Serikali;
(c) Kupunguza Ushuru wa Forodha
kutoka asilimia 25 hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye vifungashio
vinavyotumiwa na wazalishaji wa maziwa kwa joto la juu yanayodumu kwa
muda mrefu (UHT Milk) vinavyotambulika kwa HS codes 4819.50.00. Lengo
la hatua hii ni kutoa unafuu kwa wazalishaji wa maziwa hapa nchini.
Utaratibu wa Duty Remission utakaotumika kutoa unafuu huo;
(d) Kupunguza Ushuru wa Forodha
kutoka kiwango cha asilimia 10 hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye
vifuniko vya chupa za mvinyo (corks and stoppers) vinavyotambulika kwa
HS Codes 4503.10.00 kwa kuzingatia kuwa havizalishwi hapa nchini. Hatua
hii inalenga kuwapunguzia gharama wazalishaji wa mvinyo ili
kuhamasisha na kuendeleza kilimo cha zao la zabibu nchini pamoja na
ajira. Utaratibu wa Duty Remission utakaotumika kutoa unafuu huo;
(e) Kuongeza Ushuru wa Forodha
kutoka asilimia 25 hadi asilimia 35 kwa mwaka mmoja kwenye bidhaa za
marumaru zinazotambulika kwa HS Code 6907.21.00; 6907.22.00; na
6907.23.00 zinazoingizwa kutoka nje. Lengo la hatua hii ni kulinda na
kukuza viwanda vya ndani vinavyozalisha marumaru pamoja na kuongeza
ajira;
(f) Kuongeza Ushuru wa Forodha
kutoka asilimia 25 hadi asilimia 35 kwa mwaka mmoja kwenye chai
inayotambulika kwa HS Code 09.02 inayoagizwa kutoka nje. Lengo la
pendekezo hilo ni kulinda viwanda vya ndani na kuhamasisha kilimo cha
chai hapa nchini pamoja na kuongeza ajira katika sekta ya kilimo;
(g) Kuongeza Ushuru wa Forodha
kutoka asilimia 25 hadi asilimia 35 kwa mwaka mmoja kwenye magunia ya
kitani (sacks and bags of jute or other textile bast fibers of heading
53.03) yanayotambulika kwa HS Code 6305.10.00 yanayoagizwa kutoka nje.
Lengo la hatua hii ni kulinda viwanda vya ndani vinavyotengeneza
magunia ya katani, kukuza na kuendeleza kilimo cha zao la mkonge hapa
nchini pamoja na kuongeza ajira na mapato ya Serikali;
(h) Kuongeza Ushuru wa Forodha
kutoka asilimia 0 hadi asilimia 10 kwa mwaka mmoja kwenye unga wa
kakao unaoingizwa kutoka nje unaotambulika kwa HS Code 1805.00.00.
Lengo ni kuchochea na kuhamasisha kilimo cha zao la kakao nchini pamoja
na kuongeza mapato ya Serikali;
(i) Kupunguza Ushuru wa Forodha
kutoka asilimia 25 hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye vifungashio
vya kuhifadhia kahawa vinavyotumiwa na viwanda vya kusaga kahawa
nchini. Vifungashio vitakavyohusika ni vile vinavyotambulika katika HS
codes 7310.21.00; 6305.10.00; 3923.50.10; 3923.50.90 na 3920.30.90.
Hatua hii inalenga kuongeza thamani kwenye zao la kahawa na kuvipa
unafuu wa gharama viwanda vinavyosaga kahawa hapa nchini. Utaratibu wa
“Duty Remission” utatumika katika kuagiza vifungashio hivyo;
(j) Kupunguza Ushuru wa Forodha
kutoka asilimia 25 hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye vifungashio
vya kuhifadhia korosho. Vifungashio vitakavyohusika ni vile
vinavyotambulika katika HS code
3923.21.00. Hatua hii inalenga kuongeza thamani kwenye zao la korosho
na kuvipa unafuu wa gharama viwanda vinavyochakata korosho hapa
nchini. Aidha utaratibu wa “Duty Remission” utatumika katika kuagiza
vifungashio hivyo;
(k) Kupunguza Ushuru wa Forodha
kutoka asilimia 25 hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye vifungashio
vya kuhifadhia pamba. Vifungashio vitakavyohusika ni vile
vinavyotambulika katika HS codes 3920.30.90; 6305.39.00 na 7217.90.00.
Hatua hii inalenga kuvutia uwekezaji ili kuongeza thamani ya zao la
pamba nchini;
(l) Kupunguza Ushuru wa Forodha
kwa kiwango cha asilimia 0 kwa mwaka mmoja kutoka kiwango cha awali
cha asilimia 25 kwenye malighafi za kutengeneza taulo za watoto (Baby
Diapers) zinazotumbulika kwa HS code 3506.91.00 Hot Melt Adhesive; PE
film HS Code 3920.10.90, Empty bag for Baby Diapers HS Code
6305.33.00, Plastic cask HS Code 3926.90.90; na kiwango cha awali cha
asilimia 10 kwenye Super Absorbent Polymer HS Code 3906.90.00, Wet
strength paper HS Code 4803.00.00, Non-woven HS Code 5603.11.00,
Polyethylene laminated Nonwovens HS Code 5903.90.00, Spandex HS Code
5402.44.00 na Dust free paper HS Code 4803.00.00. Aidha, msamaha huu
utatolewa kwa utaratibu wa “Duty Remission”. Hatua hii inatarajiwa
kutoa unafuu wa gharama za uzalishaji na kuongeza ajira;
(m) Kutoza Ushuru wa Forodha kwa
kiwango cha asilimia 0 kwa mwaka mmoja kutoka kiwango cha awali cha
asilimia 25 kwenye vifaa vinavyotumika katika kukata, kung’arisha na
kuongeza thamani ya madini ya vito vinavyotambulika kwa HS Codes
6804.10.00; 7018.90.00;
7020.00.99; na kiwango cha
awali cha asilimia 10 kwenye HS Codes 3606.90.00; 6813.20.00;
8202.20.00; 8202.99.00; 8203.20.00; 8205.10.00; 8423.89.90;
8513.10.90; na 9002.19.00. Hatua hii inalenga kuchochea uongezaji wa
thamani kwenye madini. Utaratibu wa “Duty Remission” utatumika katika
kuagiza vifaa hivyo;
(n) Kutoza Ushuru wa Forodha kwa
kiwango cha asilimia 10 kwa mwaka mmoja kutoka kiwango cha awali cha
asilimia 25 kwenye makaratasi (HS Code 4805.24.00 na 4805.25.00)
yanayotumika kama malighafi ya kutengeneza vifungashio aina ya maboksi
(corrugated boxes). Utaratibu wa “Duty Remission” utatumika. Lengo la
hatua hii ni kuwapa unafuu wazalishaji wa vifungashio hivyo hapa nchini
ili wananchi waweze kuvipata kwa bei nafuu;
(o) Kutoza Ushuru wa Forodha kwa
kiwango cha asilimia 0 kwa mwaka mmoja kutoka kiwango cha awali cha
asilimia 25 kwenye vifungashio vya mbegu vinavyotambulika katika HS
codes 3923.29.00; 6305.10.00; 4819.40.00; 7310.29.90; 6305.33.00;
6305.20.00; 6304.91.90 na 7607.19.90. Utaratibu utakaotumika kutoa
unafuu huo ni wa “duty remission”. Lengo la hatua hii ni kutoa unafuu
kwa wazalishaji wa mbegu hapa nchini;
(p) Kutoza Ushuru wa Forodha wa
asilimia 35 badala ya asilimia 25 kwa mwaka mmoja kwenye kahawa
inayotambulika kwa Heading 09.01 inayoagizwa kutoka nje ya nchi. Lengo
la pendekezo hili ni kulinda viwanda vya ndani na kuhamasisha kilimo
cha kahawa hapa nchini
pamoja na kuongeza ajira katika sekta ya kilimo;
(q) Kutoza Ushuru wa Forodha wa
asilimia 10 au dola za kimarekani 125 kwa kila tani moja ya ujazo
(Metric ton) kwenye bidhaa za chuma kwa mwaka mmoja kutegemea kiwango
kitakachokuwa kikubwa. Bidhaa hizo ni “Flat – rolled products of iron or
Non-alloy steel na Flat –rolled products of other alloy steel.” Bidhaa
hizi hutambulika katika HS Codes 7209.16.00; 7209.17.00; 7209.18.00;
7209.26.00; 7209.27.00; 7209.28.00; 7209.90.00;
7211.23.00; 7211.90.00; 7225.50.0
na 7226.92.00. Lengo la kuendelea kutoza viwango hivyo ni kulinda
viwanda vya hapa nchini, kukuza ajira pamoja na kudhibiti udanganyifu
wa thamani halisi ya bidhaa hizo kutoka nje;
(r) Kutoza Ushuru wa Forodha wa
asilimia 25 au dola za kimarekani 250 kwa kila tani moja ya ujazo
(metric ton) kwenye bidhaa za mabati zinazotambulika kwa HS codes
7210.41.00; 7210.49.00; 7210.61.00; 7210.69.00; 7210.70.00 na
7210.90.00 kutegemea kiwango kitakachokuwa kikubwa badala ya ushuru wa
asilimia 25 au dola za kimarekani 200 kwa kila tani moja ya ujazo
(metric ton), kwa mwaka mmoja.
Lengo la hatua hii ni kuwalinda wazalishaji wa bidhaa hizo hapa nchini
kutokana na ushindani wa nje;
(s) Kutoza Ushuru wa Forodha wa
asilimia 10 au dola za kimarekani 250 kwa kila tani moja ya ujazo
(Metric ton) kwa mwaka mmoja kutegemea kiwango kitakachokuwa kikubwa
kwenye bidhaa za mabati zinazotambulika katika HS Code 7212.60.00
badala ya ushuru wa asilimia 10 pekee. Lengo la hatua hii ni kulinda
viwanda vya ndani kutokana na udanganyifu wa thamani halisi ya bidhaa
hizo zinapoingizwa kutoka nje (under-invoicing and under valuation), na
kulinda ajira na mapato ya Serikali;
(t) Kutoza Ushuru wa Forodha wa
asilimia 25 au dola za kimarekani 250 kwa kila tani moja ya ujazo
(Metric ton) kwenye bidhaa za mabati kwa mwaka mmoja kutegemea kiwango
kitakachokuwa kikubwa. Ushuru huo unahusu bidhaa zinazotambulika katika
HS Code 7212.30.00; 7212.40.00 na 7212.50,00. Hatua hii ina lengo la
kulinda viwanda vya ndani kutokana na udanganyifu wa thamani halisi ya
bidhaa hizo zinapoingizwa kutoka nje (under invoicing and under
valuation), na kulinda ajira na mapato ya Serikali;
(u) Kutoza Ushuru wa Forodha wa
asilimia 25 au dola za kimarekani 250 badala ya kiwango cha asilimia 25
au dola za kimarekani 200 kwa kila tani moja ya ujazo (metric ton)
kwenye bidhaa za chuma kwa mwaka mmoja kutegemea kiwango kitakachokuwa
kikubwa kwenye nondo kwa mwaka mmoja. (Reinforment bars and hallow
profile). Hatua hii inahusu bidhaa zinazotambulika katika HS codes
7213.10.00; 7213.20.00; 7213.99.00; 7214.10.00; 7214.20.00; 7214.30.00;
7214.90.00; 7214.99.00; 7215.10.00; 7215.50.00; 7215.90.00;
7225.90.00; 7225.92.00; 7225.99.00; 7306.30.00; 7306.50.00; 7306.61.00;
7306.69.00; na 7306.90.00. Lengo la hatua hii ni kulinda viwanda
vinavyozalisha nondo hapa nchini na kuongeza ajira;
(v) Kutoza Ushuru wa Forodha wa
asilimia 35 badala ya asilimia 25 kwa mwaka mmoja kwenye bidhaa za
mboga mboga (horticultural products) zinazotambulika kwa HS codes
0603.11.00; 0603.12.00; 0603.13.00; 0603.14.00; 0603.15.00; 0603.19.00;
0604.20.00; 0604.90.00; 0701.90.00; 0702.00.00; 0703.10.00;
0703.20.00; 0703.90.00; 0706.10.00; 0706.90.00; 0710.10.00;
0710.21.00; 0710.22.00; 0710.30.00; 0714.10.00; 0714.20.00; 0804.30.00;
0804.40.00; 0804.50.00;
0805.10.00; 0805.40.00;
0805.50.00; 0806.10.00; 0807.11.00; 0807.20.00; 0808.10.00;
0808.30.00; 0910.11.00 na 0910.12.00. Lengo la hatua hii ni kulinda
wakulima wa ndani ili kuendeleza kilimo cha matunda, mbogamboga na maua
hapa nchini;
(w) Kutoza ushuru wa forodha kwa
kiwango cha asilimia 10 badala ya asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye
bidhaa za fito za plastiki zijulikanazo kama PVC Profiles HS Code
3916.10.00; 3916.20.00; 3916.90.00 ambazo hutumika kwa ajili ya
kutengenezea fremu za milango, madirisha n.k. Lengo la hatua hii ni
kuongeza mapato ya Serikali;
(x) Kutoza Ushuru wa Forodha wa
asilimia 25 badala ya asilimia 10 kwa mwaka mmoja kwenye karatasi
zinazozalishwa na viwanda vya hapa nchini ambazo zinazotambulika kwa HS
codes 4804.11.00; 4804.21.00; 4804.29.00; 4804.31.00 na 4804.41.00.
Lengo la hatua hii ni kuendelea kulinda viwanda vinavyozalisha
karatasi hizo hapa nchini;
(y) Kutoza Ushuru wa Forodha kwa
kiwango cha asilimia 10 kwa mwaka mmoja kutoka kiwango cha awali cha
asilimia 35 kwenye ngano inayotambulika kwa HS Code 1001.99.10 na HS
Code 1001.99.90 kwa utaratibu wa “Duty Remission” ambapo wanaonufaika
na unafuu huu ni wenye viwanda vya kusaga ngano. Lengo la hatua hii ni
kupunguza gharama kwa Viwanda vinavyozalisha unga wa ngano;
(z) Kutoza Ushuru wa Forodha kwa
kiwango cha asilimia 0 kwa mwaka mmoja kutoka kiwango cha awali cha
asilimia 25 kwa utaratibu wa duty remission kwenye bidhaa ijulikanayo
kama “Printed Alluminium Barrier Laminates” (ABL) HS Code 3920.10.90
ambayo hutumika
kama malighafi ya kutengeneza
vifungashio vya dawa ya meno kwenye viwanda vya ndani. Lengo la hatua
hii ni kutoa unafuu wa gharama kwa viwanda vinavyozalisha dawa ya meno
nchini;
(aa) Kutoza Ushuru wa Forodha kwa
kiwango cha asilimia 0 kwa mwaka mmoja kutoka kiwango cha awali cha
asilimia 10 kwa utaratibu wa “Duty Remission” kwenye malighafi ya
kutengeneza sabuni ijulikanayo kama RBD Palm Stearin (HS Code
1511.90.40) kwa viwanda
vinavyotengeneza sabuni nchini. Lengo la hatua hii ni kutoa unafuu kwa viwanda vya kuzalisha sabuni nchini;
(bb) Kutoza kwa mwaka mmoja Ushuru
wa Forodha wa asilimia 25 au dola za kimarekani 1.35 kwa kilo moja ya
viberiti (safety match boxes) vinavyotambuliwa kwenye HS code
3605.00.00 kutegemea kiwango kitakachokuwa kikubwa badala ya asilimia
25 pekee. Lengo la hatua hii ni kulinda viwanda vinavyozalisha viberiti
nchini dhidi ya bidhaa zenye ruzuku kutoka nje na hivyo kuwa na
ushindani sawa katika soko.
odi ya Nyama Tanzania
Kutoza ada ya shilingi 70,000 kwa Cheti cha Kukubaliwa kupeleka nyama nje ya Nchi badala ya kiwango cha asilimia 1 ya malipwani.
Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA)
Kupunguza
tozo ya ukaguzi wa Umeme kwa kipimo kimoja (electrical inspection,
electrical insulation test and general inspection) kutoka shilingi
590,000 hadi 150,000. Tozo hii inatozwa kabla ya kuanza biashara ya
mafuta. Pendekezo hili linatarajia kuchochea mazingira wezeshi ya
biashara nchini hususan katika maeneo ya vijijini.
Utoaji Leseni za Bima kwa Makampuni
Napendekeza
kubadili utaratibu wa sasa wa makampuni ya bima kulazimika kuomba
leseni upya kila mwaka na badala yake makampuni yanayofanya vizuri yawe
na leseni ya kudumu, na makampuni yalioko kwenye hali ya uangalizi
yapewe leseni ya miaka mitatu huku yakiwa kwenye uangalizi na
yakiimarika na kufanya vizuri yaingie kwenye leseni za kudumu. Taratibu
za ufuatiliaji na malipo ya kila mwaka yaendelee kama ilivyo sasa. Lengo
ni kupunguza ukiritimba.
Uboreshaji wa Mazingira ya Ufanyaji Biashara
Sambamba
na hatua za kikodi zilizolenga kupunguza gharama ili kuboresha
mazingira ya kufanya biashara, Serikali itakamilisha mfumo wa kimtandao
wa kuwa na dirisha moja la upatikanaji wa vibali mbalimbali katika Idara
zote zinazohusika na usajili na vibali ili kuwapunguzia wawekezaji
mizunguko ya kutembea ofisi zaidi ya moja kuhangaika nenda rudi kutafuta
vibali vinavyotolewana ofisi zaidi ya moja. Lengo la hatua hii
nikurahisisha mazingira ya kufanya biashara kama ilivyobainishwa kwenye
Blueprint.
Maeneo Mahususi
Barabara za Mijini na Vijijini
Mheshimiwa
Spika, hali ya barabara vijijini hairidhishi ambapo bado vipo vijiji
ambavyo havina barabara kabisa. Barabara nyingi zinazosimamiwa na TARURA
zina hali mbaya. Kwa sasa mtandao wa barabara zilizo chini ya TARURA
una urefu usiopungua kilomita 108,946.2 ambazo zinaunganisha maeneo
mbalimbali ya mijini na vijijini. Hadi Desemba 2020, mtandao wa barabara
zilizo chini ya TARURA wenye kiwango cha lami ulifikia kilometa
2,250.69, sawa na asilimia 2.1 tu, changarawe kilometa 27,809.26
(asilimia 25.6) na udongo kilometa 78,886.25 (asilimia 72.4).
Mheshimiwa
Spika, hali hii ya barabara ina madhara makubwa sana kwa jamii yetu
kwani baadhi ya akina mama wajawazito wanapoteza maisha kwa kuchelewa
kufika kwenye vituo vya afya. Aidha, wapo wengine ambao wanajifungulia
njiani kutokana na kuchelewa kufika kwenye vituo vya afya. Vilevile,
wapo baadhi ya wanafunzi wanaosombwa na maji na kufariki kutokana na
ubovu wa miundombinu ya barabara, hususan katika maeneo ya vijijini.
Kadhalika, bado kuna changamoto ya usafirishaji wa mazao na bidhaa
kutoka au kwenda barabara kuu katika baadhi ya maeneo. Serikali imeona
ipo haja ya kutafuta vyanzo vipya vya mapato kuongezea katika mgawo wa
sasa kupitia Mfuko wa Barabara ili kufanikisha ugharamiaji wa mtandao wa
barabara hizo.
Upatikanaji wa Maji Safi na Salama Mijini na Vijijini
Mheshimiwa
Spika, hali ya upatikanaji wa maji safi na salama mijini na vijijini
bado hairidhishi. Maji hayana mbadala, maji ni uhai, maji ni maisha kwa
viumbe hai vyote. Bado vipo vijiji ambavyo havina kisima hata kimoja cha
maji safi na salama na badala yake hutumia maji ya mapalio, maji ya
madimbwi, maji ya mito wanayochangia na wanyama. Tanzania ina vyanzo
vikubwa na vya uhakika vya maji ikiwa ni pamoja na Ziwa Tanganyika,
Ziwa Victoria, Ziwa Nyasa, Ziwa Rukwa, Ziwa Chala, Mto Kiwira, Ruvu,
Rufiji na Ruvuma pamoja na mingine. Aidha, kuna uwezekano wa kutumia
mabwawa makubwa kama ya Kidunda, Ndembela na Farkwa kama yangekamilika
lakini utekelezaji wake haujaanza pamoja na fidia kutolewa na Serikali
kutokana na uhaba wa fedha. Ipo miradi mingi katika mikoa ya Iringa,
Kagera, Kigoma, Kilimanjaro, Lindi, Mara, Mbeya, Mtwara, Mwanza, Njombe,
Rukwa, Ruvuma, Shinyanga, Simiyu, Singida, Songwe, Tabora, Tanga na
Simiyu inayotakiwa kutekelezwa katika mwaka 2021/22, lakini haikuwa
katika bajeti. Mikoa mingine ambayo sikuitaja hapa iko kwenye bajeti ya
Wizara husika.
Mheshimiwa
Spika, hali ya ukosefu wa maji safi na salama ina madhara makubwa sana
kwa jamii yetu. Serikali imedhamiria kuhakikisha kuwa inampa nafuu
mwanamke katika kufanya shughuli zake za kiuchumi, lengo likiwa ni
kumtua mama ndoo kichwani na kuondoa changamoto mbalimbali zinazowakumba
akina mama na mabinti katika harakati za kutafuta maji. Aidha, kuna
baadhi ya wanafunzi wanakosa masomo na kuharibu maisha yao kutokana na
uhaba wa maji katika maeneo yao. Hivyo, Serikali imeona ipo haja ya
kuongeza fedha za kugharamia miradi ya maji kwa kubuni vyanzo mbadala
vya mapato kwa ajili ya kugharamia miradi ya maji hususan katika maeneo
ambayo yana uhaba mkubwa wa maji.
Afya na Bima ya Afya kwa Wote
Mheshimiwa
Spika, Sekta ya Afya ni sekta muhimu katika ustawi wa jamii yetu na ni
moja ya mahitaji muhimu sana katika maisha ya sasa ya mwanadamu.
Serikali ya CCM imefanya kazi kubwa sana katika sekta hii, ingawa bado
kuna kazi kubwa ya kufanya kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu na
mabadiliko ya hali za kiafya kwenye kizazi cha leo. Aidha, wananchi
katika maeneo mbalimbali wametumia nguvu kubwa katika kutafuta ufumbuzi
wa masuala ya upatikanaji wa huduma za afya kwa kujenga maboma karibu na
maeneo yao.
Majengo yaliojengwa kwa nguvu za wananchi yamekaa kwa muda
mrefu, kati ya miaka mitano (5) hadi 15. Hadi kufikia Juni 2021, kuna
jumla ya maboma 8,004 ya zahanati ambayo yapo katika mikoa mbalimbali
nchini na yapo katika hatua mbalimbali za kukamilishwa. Vilevile, yapo
maboma kwenye ngazi ya vituo vya afya zaidi ya 1,500 ambayo yametumia
nguvu ya wananchi na yanahitaji kukamilishwa. Serikali itaendelea na
jitihada za kutafuta fedha kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa maboma
hayo pamoja na kuajiri wataalamu wa afya na kuimarisha upatikanaji wa
dawa, vitendanishi, vifaa na vifaa tiba.
Mheshimiwa
Spika, kuna mradi mkubwa wa bima kwa wote (Universal Health Care)
unaolenga kuwafikia watanzania wote. Tanzania ina jumla ya kaya milioni
12.827, ambapo asilimia 20 ya kaya hizo inakadiriwa kuwa ni kaya
zisizokuwa na uwezo. Katika kufanikisha utekelezaji wa dhana ya bima ya
afya kwa wananchi wote, Serikali itahitaji zaidi ya shilingi bilioni 149
katika mwaka wa kwanza kwa ajili ya kaya zisizo na uwezo. Kiasi hicho
cha fedha kitaendelea kuongezwa kila mwaka ili ifikapo mwaka 2034/35,
wananchi wote wawe wamefikiwa na bima ya afya. Serikali imeendelea
kuboresha na kusogeza huduma za afya karibu na wananchi ambapo vituo vya
kutolea huduma za afya kwa ngazi mbalimbali vimeendelea kujengwa ili
bima ya Afya iweze kutumika na kuwanufaisha wananchi wote.
Elimu
Mheshimiwa
Spika, kuhusu sekta ya elimu kuna kazi kubwa bado iko mbele yetu. Bado
kuna shule ambazo zina wanafunzi wengi kuliko idadi ya madarasa na zipo
zinazogawa mikondo ili wanafunzi wengine wasome asubuhi na wengine
wasome mchana. Hali hii inapunguza muda wa wanafunzi kusoma. Zipo shule
ambazo kwenye darasa moja wanaweka uzio wa ubao kutenganisha ili chumba
kimoja wasome wanafunzi wa madaraja mawili. Aidha, zipo shule ambazo
miundombinu yake imechakaa sana kiasi cha kutishia usalama wa watoto na
walimu wetu. Yapo pia madarasa yaliyoezekwa kwa nyasi na yana sakafu ya
vumbi. Kadhalika, mwaka ujao utakuwa wa kwanza wa kupokea wanafunzi
kidato cha kwanza waliodahiliwa darasa la kwanza kwa mpango wa
elimumsingi bila ada. Jambo hili lisipoangaliwa mapema litakuja
kusababisha wanafunzi kuchaguliwa kujiunga kidato cha kwanza na kukosa
pa kwenda hadi miundombinu ijengwe kwa zimamoto. Kwa hatua ya maendeleo
nchi yetu iliyofikia katika sekta mbalimbali, hali hii haipendezi na
haitakiwi kuendelea. Kujenga miundombinu ya shule zetu kwa kusubiri
irushwe kwenye mitandao ya kijamii ndio tuone inatutia aibu, au kusubiri
watoto wakose pa kwenda au wakose pa kukaa ndipo tukimbizane na
kufukuzana, ni ishara ya kutopanga vizuri. Hili tusingependa liendelee
kuwepo.
Mheshimiwa
Spika, kila mwaka kuna wanafunzi kati ya asilimia 15 - 20 wanatoka
kwenye mfumo wa elimu kwa kutoendelea na kidato cha kwanza kutokana na
sababu mbalimbali zikiwemo kupata ujauzito, utoro na hali ngumu ya
maisha. Ukosefu wa mpango wa kugharamia mahitaji ya sekta ya elimu ndiyo
chanzo cha tatizo hili.
Mheshimiwa
Spika, kwa upande wa elimu ya juu, zaidi ya wanafunzi 11,000 wenye sifa
za kujiunga na vyuo vikuu ambao tayari walishapata udahili katika vyuo
mbalimbali walikosa mikopo. Naongelea mkopo, sio fedha ya bure, bali ni
mkopo ambao ataurejesha. Katika jamii nyingi za kitanzania, mtoto
akikosa mkopo huku akiwaona wenzake wanaendelea, inamfadhaisha sana. Ni
mfadhaiko kwake na familia nzima. Kwa hatua ya maendeleo ambayo nchi
yetu imepata katika sekta mbalimbali hali hii haipendezi na haitakiwi
kuendelea. Serikali inakusudia kuchukua hatua za kuhakikisha kuwa
inaongeza bajeti ya mikopo ya elimu ya juu ili kuwanufaisha vijana wote
wenye sifa za kupata mkopo.
Miradi ya Kielelezo ya Bwawa la Kufua Umeme wa Maji la Mwalimu Nyerere na Reli ya Kisasa (SGR)
Mheshimiwa
Spika, Miradi ya bwawa la Kufua Umeme la Mwalimu Nyerere na Reli ya
Kisasa (SGR) sio tu ni miradi ya kielelezo bali ni miradi mama kwa kila
mtanzania. Ni miradi inayoashiria uhuru wa nchi yetu, ni miradi
inayoashiria kujitegemea kwa nchi yetu, ni miradi inayoashiria heshima
ya mtanzania na inajengwa na mtanzania. Kama alivyosema Mheshimiwa Rais,
kutokamilika kwa miradi hii itakuwa laana kwa Taifa letu. Hatutajengewa
miradi hii na mtu yeyote, tutawaenzi wabeba maono wa miradi hii kwa
kujenga na kuikamilisha. Mwalimu Nyerere alibeba maono ya miradi hii,
Rais Magufuli alianzisha miradi hii, Rais Samia anakwenda kuijenga
miradi hii. Niwahakikishie watanzania hapatakuwepo GOFU hata la Mradi
mmoja wala kusimama kwa mradi unaotekelezwa hata kwa mwezi mmoja.
Mheshimiwa
Spika, ili kukabiliana na maeneo mahsusi hayo niliyotangulia kuyasema,
napendekeza kufanya marekebisho kwenye Sheria zifuatazo:
Sheria ya Ushuru wa Barabara na Mafuta, SURA 220
Kufanya marekebisho kwenye Sheria ya Ushuru wa Barabara na Mafuta kama ifuatavyo:
Kuongeza Ushuru wa barabara kwa shilingi 100 kwa kila lita ya mafuta ya petroli na dizeli;
Kufanya
marekebisho ya kifungu cha 4 A(a) cha sheria ili kuelekeza fedha
zitakazokusanywa kutokana na ongezeko la ushuru wa barabara na mafuta la
shilingi 100 kwa aina zote za mafuta ziwe kwa ajili ya ujenzi na
ukarabati wa barabara za vijijini kupitia TARURA.
Hatua hii ya marekebisho ya Sheria inatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 322,158.20.
Sheria ya Petroli, SURA 392
Kufanya
marekebisho kwenye Sheria ya Petroli ili kuongeza tozo ya Mafuta ya Taa
kutoka shillingi 150 hadi shillingi 250. Lengo la hatua hii ni
kupunguza uchakachuaji wa mafuta kufuatia ongezeko la ushuru wa mafuta
kwenye dizeli na petroli.
Sheria ya Posta na Mawasiliano ya Kielektroniki, SURA 306
Kufanya marekebisho kwenye Sheria ya Posta na Mawasiliano ya Kielektroniki kama ifuatavyo:
Kutoza
tozo ya shillingi 10 hadi shilingi 10,000 katika kila muamala wa kutuma
au kutoa pesa. Kiasi cha tozo kinatofautiana kulingana na thamani ya
muamala wa fedha unaotumwa au kutolewa. Pendekezo hili litaongeza mapato
ya Serikali kiasi cha shillingi milioni 1,254,406.14; na
Kutoza
kiasi cha shilingi 10 hadi shilingi 200 kwa siku kwa kila laini ya simu
kulingana na uwezo wa kuongeza salio kwa watumiaji. Pendekezo hili
litapelekea kuongeza mapato ya Serikali kiasi cha shillingi milioni
396,306.0.
Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, SURA 147
Kutokana
na vinywaji vikali kuwa na kiwango kikubwa cha kilevi, napendekeza
kuongeza ushuru wa bidhaa kwa asilimia 30 ili kuwa na uwiano wa viwango
vya kodi kati ya Vinywaji kali na Bia. Hatua hii inatarajia kuiongezea
mapato Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 60,769.35.
Utekelezaji wa hatua hizi nne kwa pamoja unatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 2,033,639.66.
Tarehe ya Kuanza Kutekeleza Hatua Mpya za Kodi.
Mheshimiwa
Spika, hatua hizi za kikodi zinazopendekezwa zitaanza kutekelezwa
tarehe 1 Julai, 2021, isipokuwa pale itakapoelezwa vinginevyo. Aidha,
Marekebisho hayo yataainishwa katika Muswada wa Sheria ya Fedha ya mwaka
2021 na Matangazo ya Serikali (Government Notices).
Njia Mbadala za Kutekeleza Miradi Mikubwa
Mheshimiwa
Spika, mwaka 2020 nchi yetu ilifanikiwa kuingia katika kundi la nchi
zenye kipato cha kati cha chini (Lower Middle-Income Country). Kuingia
katika kundi la nchi zenye uchumi wa kati kunaifanya nchi yetu kutakiwa
kujiendesha kiuchumi bila kutegemea kwa kiwango kikubwa misaada na
mikopo yenye masharti nafuu ambayo, hupewa nchi zenye kipato cha chini.
Hivyo, ni lazima Serikali iboreshe mbinu inazotumia na kubuni mbinu mpya
za kupata mapato. Katika kutekeleza hatua hii, Serikali imeanza kufanya
uchambuzi wa vyanzo mbadala vya rasilimali fedha kwa ajili ya miradi ya
maendeleo kama vile ufadhili mchanganyiko (Blended Finance). Wafadhili
wanaotoa aina hii ya ufadhili hutoa fursa kwa nchi zinazoendelea kama
Tanzania, kurekebisha au kujumuisha (restructuring or consolidation)
deni lake kwa makubaliano ya kutumia sehemu ya malipo ya deni katika
uhifadhi wa mazingira au kuimarisha sekta za kiuchumi na kijamii.
Mheshimiwa
Spika, Katika mwaka 2021/22, Serikali inadhamiria kukamilisha mchakato
wa Tathmini na Ukadiriaji wa Kukopesheka kwa Nchi (Sovereign Credit
Rating). Hatua hii inalenga kutuwezesha kujua nafasi yetu katika masoko
ya fedha ya kimataifa na jinsi wakopeshaji wanavyotuona hasa katika
uwezo wa kusimamia uchumi na kulipa madeni yetu. Hatua hiyo itatuwezesha
pia kuongeza wigo wa wakopeshaji ambao wako tayari kutukopesha, hususan
katika Masoko ya Mitaji ya Kimataifa (International Capital Markets).
Serikali itaanza mara moja mchakato wa wazi wa kutekeleza na kukamilisha
kazi ya Sovereign Credit Rating ndani ya mwaka 2021/22.
Mheshimiwa
Spika, katika jitihada za kupanua wigo wa vyanzo vya rasilimali fedha,
Serikali itaangalia uwezekano wa kutumia Hati Fungani zitakazotolewa na
Halmashauri za Manispaa na Majiji kama njia mbadala ya kupata rasilimali
fedha kwa ajili ya miradi ya kimkakati. Hatua hii itapunguza mzigo
kwenye Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali hasa kwa Halmashauri zenye
miradi ambayo imefanyiwa upembuzi yakinifu na kuwa na uhakika wa uwezo
wa miradi hii kujiendesha kwa faida (bankable projects). Serikali kwa
kushirikiana na Mfuko wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (United National
Capital Development Fund - UNCDF) na Mamlaka ya Usimamizi wa Masoko ya
Mitaji (Capital Markets and Securities Authority - CMSA) imeanza
mchakato wa kuhakikisha kwamba Halmashauri, Manispaa na Majiji
yatakayokidhi vigezo na masharti ya matumizi ya Hati Fungani hizi
yanaanza kutumia utaratibu huu.
Mheshimiwa
Spika, Serikali inaona umuhimu wa kutumia Masoko ya Hati Fungani za
Kimataifa maarufu kama Eurobonds ikiwa ni chanzo cha kuaminika na
thabiti cha kugharamia miradi ya maendeleo kwa kuzingatia Mkakati wa
Deni la Muda wa Kati (Medium Term Debt Strategy - MTDS). Hatua hii
inakwenda sambamba na hatua nyingine inayopendekezwa katika hotuba hii
ya kufungua soko la dhamana za Serikali ili kuruhusu wawekezaji wa nje
ya Tanzania na Afrika Mashariki kununua hati fungani zetu ili kuongeza
ukwasi katika soko la ndani.
Mheshimiwa
Spika, Soko la Eurobond ulimwenguni linakadiriwa kuwa na zaidi ya dola
za Marekani trilioni 30 zilizotolewa kwa nchi zinazotafuta rasilimali
fedha kwa njia ya mikopo kutoka kwenye masoko ya kimataifa yenye ukwasi
mkubwa ili kugharamia miradi ya maendeleo. Njia hii pia hutumiwa na
mashirika ya kimataifa kama Benki ya Dunia na Benki ya Maendeleo ya
Afrika wanapotafuta fedha kwa ajili ya kufadhili miradi yao kote
duniani. Aidha, nchi mbalimbali za kusini mwa Jangwa la Sahara
zinazofanya vizuri kiuchumi zimekuwa zikitumia Soko la eurobond kama
chanzo thabiti na chenye masharti rafiki katika kugharamia utekelezaji
wa miradi yao ya maendeleo. Tanzania itahitaji kufanyiwa tathmini ya
kukopesheka ili kufikia masoko ya mitaji ya kimataifa kupitia eurobonds.
Hivyo, zoezi la kukadiria au kutathmini kukopesheka kwa Tanzania ni
hatua isiyoepukika.
Mheshimiwa
Spika, tangu mwaka 2010 tulipopitisha Sheria ya PPP hatujapata
mafanikio ya kujivunia katika eneo hili pamoja na faida kubwa na nyingi
ambazo Taifa linaweza kupata kupitia mfumo wa PPP hasa katika miradi
mikubwa inayohitaji fedha nyingi na utaalamu kutoka sekta binafsi.
Utekelezaji wa miradi ya PPP hupunguza mzigo kwenye deni la Serikali na
hata katika Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali na hutoa nafuu ya kibajeti
(Fiscal Space) kwa kuiwezesha Serikali kutekeleza majukumu mengine
ambayo hayawezi kugharamiwa na sekta binafsi. Hivyo, ni muhimu kutumia
PPP kwenye miradi mbalimbali inayokidhi Sheria ya Ubia baina ya Sekta ya
Umma na Sekta Binafsi, Sura 103.
Mheshimiwa
Spika, kwa kuzingatia manufaa ya PPP, Serikali itaongeza kasi ya
kushughulikia miradi ya ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi ikiwa ni
pamoja na: Ujenzi wa viwanda vya dawa muhimu na vifaa tiba; ujenzi wa
Hoteli ya Nyota Nne na Kituo Changamani cha Biashara katika Kiwanja cha
Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere; ujenzi wa miundombinu ya
kusambaza gesi asilia katika mikoa ya Dar es Salaam, Lindi na Mtwara; na
ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza simu za mkononi kupitia Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (TCRA). Aidha, wananchi na wawekezaji wengine
wanaalikwa kubainisha maeneo ambayo wanaweza kushiriki katika
utekelezaji wa miradi ya PPP kulingana na uwezo wao wa mitaji na
utaalamu.
SURA YA BAJETI KWA MWAKA 2021/22
Mheshimiwa
Spika, kwa kuzingatia shabaha, malengo pamoja na sera za bajeti kwa
mwaka 2021/22, Sura ya Bajeti inaonesha kuwa jumla ya shilingi trilioni
36.33 zinatarajiwa kukusanywa na kutumika. Mapato ya ndani yanatarajiwa
kuwa shilingi trilioni 26.03, sawa na asilimia 71.7 ya bajeti yote. Kati
ya mapato hayo, mapato ya kodi ni shilingi trilioni 22.18, sawa na
asilimia 13.5 ya Pato la Taifa. Aidha, Serikali inalenga kukusanya
mapato yasiyo ya kodi ya shilingi trilioni 2.99 na mapato kutoka vyanzo
vya Halmashauri shilingi bilioni 863.9.
Mheshimiwa
Spika, Washirika wa Maendeleo wanatarajia kuchangia misaada na mikopo
nafuu yenye jumla ya shilingi trilioni 2.96, sawa na asilimia 8.1 ya
bajeti yote. Kiasi hicho kinajumuisha fedha za miradi ya maendeleo
shilingi trilioni 2.67 na Mifuko ya Pamoja ya Kisekta shilingi bilioni
282.3. Napenda kuwashukuru Washirika wa Maendeleo kwa kuendelea kutoa
fedha za misaada na mikopo nafuu ili kufanikisha miradi na programu
mbalimbali za maendeleo zitakazotekelezwa katika bajeti ya mwaka
2021/22.
Mheshimiwa
Spika, kipekee ningependa kuwatambua Washirika wetu wa Maendeleo kama
ifuatavyo: Serikali za Canada, China, Denmark, Finland, India, Ireland,
Italia, Korea ya Kusini, Japan,Ufaransa, Ujerumani, Norway, Poland,
Ubelgiji, Uholanzi, Uswisi, Uingereza, Sweden na Marekani. Vilevile,
kuna Mashirika ya Kimataifa ambayo ni Benki ya Maendeleo ya Afrika,
Benki ya Dunia, Benki ya Kiarabu kwa Maendeleo ya Kiuchumi katika
Afrika, Mfuko wa Abu Dhabi, Mfuko wa Kuwait, Mfuko wa kimataifa wa
kusaidia mapambano dhidi ya virusi vya Ukimwi, kifua kikuu na malaria,
Umoja wa Ulaya, Benki ya Uwekezaji ya Ulaya, Umoja wa mataifa na
mashirika yote yaliyopo chini yake, Mfuko wa OPEC kwa Maendeleo ya
Kimataifa, Mfuko wa Mazingira, pamoja na Shirikisho la GAVI. Ninapenda
pia kuyatambua Mashirika yasiyo ya Kiserikali ya ndani na nje pamoja na
mashirika ya ufadhili - philanthropies kwa misaada yao kwenye sekta
mbalimbali.
Mheshimiwa
Spika, Serikali inatarajia kukopa shilingi trilioni 7.34 kutoka soko la
ndani na nje kwa masharti ya kibiashara. Kati ya kiasi hicho, shilingi
trilioni 4.99 ni mikopo ya ndani ambayo inajumuisha shilingi trilioni
3.15 kwa ajili ya kulipia hatifungani na dhamana za Serikali zinazoiva
na shilingi trilioni 1.84 kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo.
Aidha, shilingi trilioni 2.35 zinatarajiwa kukopwa kutoka soko la nje
kwa lengo la kuongeza kasi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Mheshimiwa
Spika, kwa mwaka 2021/22, Serikali inapanga kutumia jumla ya shilingi
trilioni 36.33 kwa matumizi ya kawaida na maendeleo. Kati ya fedha hizo,
shilingi trilioni 23.0 zimetengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida na
shilingi trilioni 13.33 kwa ajili ya matumizi ya maendeleo. Fedha
zilizotengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida zinajumuisha shilingi
trilioni 10.66 kwa ajili ya ulipaji wa deni la Serikali, shilingi
trilioni 8.15 kwa ajili ya mishahara na shilingi trilioni 4.19 kwa ajili
ya matumizi mengineyo. Aidha, Serikali imetenga jumla ya shilingi
bilioni 200.0 kwa ajili ya kulipa madeni yaliyohakikiwa ya watumishi,
wazabuni na watoa huduma.
Mheshimiwa
Spika, jumla ya shilingi trilioni 13.33 zimetengwa kwa ajili ya
matumizi ya maendeleo, sawa na asilimia 37 ya bajeti yote. Kati ya kiasi
hicho, fedha za ndani ni shilingi trilioni 10.37 na fedha za nje
shilingi trilioni 2.96. Aidha, fedha za maendeleo zinajumuisha, shilingi
trilioni 1.19 kwa ajili ya miradi ya reli ikiwemo ujenzi wa Reli ya
Kati kwa Kiwango cha Kimataifa; shilingi trilioni 2.08 kwa ajili ya
miradi ya barabara, ujenzi wa madaraja, na viwanja vya ndege; shilingi
trilioni 2.34 kwa ajili ya miradi ya kuzalisha, kusafirisha na kusambaza
umeme ikiwemo mradi wa kufua umeme wa maji wa Julius Nyerere; shilingi
bilioni 589.4 kwa ajili ya miradi ya maji mijini na vijijini; shilingi
bilioni 233.3 kwa ajili ya ununuzi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi;
shilingi bilioni 500 ni kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya
juu; shilingi bilioni 215.6 kwa ajili ya maandalizi ya Sensa ya Watu na
Makazi ya mwaka 2022; na shilingi bilioni 312.1 kwa ajili ya elimumsingi
bila ada. Aidha, Serikali imetenga jumla ya shilingi bilioni 400.0 kwa
ajili ya kulipa madeni yaliyohakikiwa ya miradi ya maendeleo.
HITIMISHO
Mheshimiwa
Spika, ninapoelekea mwisho wa hotuba hii, napenda kumshukuru kwa dhati
MAMA YETU kwa kuniamini na kuniteua kuwa Waziri wa Fedha na Mipango.
Ninamuahidi Mheshimiwa Rais, Waheshimiwa wabunge na Watanzania wote
kwamba, nitaibeba dhamana hii kwa uadilifu, weledi na uwezo wangu wote
na ninamuomba Mwenyezi Mungu anijalie afya njema, hekima na busara
katika kutekeleza majukumu hayo. Naomba nielezee masuala machache muhimu
kabla ya kuhitimisha hotuba hii.
Mheshimiwa
Spika, kwanza natoa pongezi kwa MAMA YETU kwa matumaini makubwa
aliyowapa watanzania. MAMA YETU ameonesha ni Kiongozi Makini, ni
Kiongozi Shupavu, ni Kiongozi Mchapa Kazi, ni Kiongozi Mwadilifu, ni
Kiongozi Msikivu, ni Kiongozi aliye na dira thabiti na maono ya
kuendelea kuiletea nchi yetu maendeleo makubwa. Ameweka wazi kuwa hataki
kodi ya dhuluma, hataki kuendesha Serikali kwa mapato ya dhuluma,
ameweka wazi kusimama imara kwenye masuala ya mapato na matumizi ya
Serikali, ameweka wazi kuwa atakuwa imara kwenye vita dhidi ya rushwa.
Mheshimiwa
Spika, kwa kauli hizo MAMA YETU ameonesha kuwa, kukaa kwake katika
nafasi mbalimbali katika Serikali za awamu mbalimbali SMT na SMZ
kumemfanya awe kiongozi aliyeandaliwa na KUIVA na aliye tayari kuiongoza
nchi kwa ufanisi mkubwa. Itakumbukwa mbali na nafasi zingine nyingi
alizoshika katika miaka yake takribani ishirini Serikalini, MAMA YETU
amekuwa Waziri katika Awamu ya Nne na amekuwa Makamu wa Rais katika
Awamu ya Tano. Kuna style za uongozi amejifunza.
Mheshimiwa
Spika kuna style za uongozi amejifunza kupitia Awamu hizo alikopewa
nafasi kuhudumu katika nafasi mbalimbali. MAMA YETU alikuwa Waziri
katika awamu ya nne iliyokuwa ikiongozwa na Rais Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete. Mheshimiwa Kikwete alikuwa Mzalendo wa kweli, alikuwa na maono
(Visionary Leader), alikuwa mwalimu, alikuwa mzazi, alikuwa mlezi na
kiongozi, alikuwa rahim sana, alikuwa mvumilivu sana aliyeamini kwenye
Mifumo, Taasisi na Utendaji wa Kitaasisi. Hii naweza kuifananisha kama
Refa kwenye mchezo wa mpira wa miguu, ambaye anachezesha mechi zake
akiwa na kadi ya njano tu, kadi nyekundu anaiacha nyumbani. Ukicheza
rafu mara ya kwanza anakuonya kwa kukuelekeza, ukicheza rafu mara ya
pili anakupa kadi ya njano, ukikosea anakupa kadi ya njano tena na
alipotakiwa kutoa kadi nyekundu mara nyingi alionya kwa mdomo, kwa kuwa
kadi nyekundu alikuwa anaiacha nyumbani. Rais Kikwete aliamini sana
kwenye Mifumo na Utendaji wa Kitaasisi. Kwa mtazamo wangu, jinsi MAMA
YETU alivyoanza ni dhahiri amepata funzo kwenye awamu hiyo ikiwemo funzo
la Uzalendo, maono na kuamini kwenye Mifumo, Taasisi na Utendaji wa
Kitaasisi”, na hapa naweza kusema ameichukua kadi ya njano, anayo na
ameanza kutumia kama mnavyoona.
Mheshimiwa
Spika, MAMA YETU alikuwa Makamu wa Rais katika awamu ya tano iliyokuwa
ikiongozwa na Hayati Rais Dkt. John Pombe Magufuli. Rais Magufuli
alikuwa mzalendo wa kweli, alikuwa na Maono (Visionary Leader), alijitoa
kwa nguvu zote (Dedicated), alikuwa na uthubutu sana, mtu wa vitendo
sana na muumini wa matokeo na kuchukua hatua za papo kwa papo. Kama refa
wa mchezo wa mpira wa miguu, alikuwa akienda kuchezesha Mechi zake
akiwa na kadi nyekundu tu, kadi ya njano alikuwa anaiacha nyumbani.
Ukicheza rafu mara ya kwanza tu anakupa kadi nyekundu, wakati mwingine
hata asipoiona rafu yeye, mchezaji au shabiki akisema ameona rafu
anakupa kadi Nyekundu (no nonsense), hata mimi mwenyewe niliwahi
kutembelewa na kadi nyekundu nikakosa michezo kadhaa. Hayati Dkt.
Magufuli aliamini kwenye nidhamu ya hali ya juu ya mchezo. MAMA YETU
alikuwa Line one na Mheshimiwa Majaliwa akiwa Line two. Hivyo, MAMA YETU
amepata mafunzo kwenye awamu hiyo ya Uzalendo, Uthubutu, mtu wa vitendo
kuamini kwenye matokeo na nidhamu kazini na ameichukua kadi ya
nyekundu.
Mheshimiwa
Spika kuna style za uongozi amejifunza. MAMA YETU anazo kadi zote, kadi
ya njano na kadi nyekundu. MAMA YETU ni Mzalendo wa kweli, ni Mwadilifu
sana, ana Uthubutu, ana Maono, anaamini kwenye Mifumo, Taasisi na
Utendaji wa Kitaasisi”, hataki maneno anataka vitendo. Nitoe rai kwa
watumishi wote wa umma na watanzania kwa ujumla tuchape kazi kwa bidii,
kwa uadilifu na uzalendo mkubwa. Kwa watumishi wa umma tusimamie
matumizi ya fedha za walipa kodi kwa uadilifu mkubwa na kwa watanzania
tulipe kodi bila shuruti. Tabia moja ya refa asiyependa kuonea upande
wowote, huwa hawezi kupendelea upande wowote. Kwenye michezo ya mieleka
huwa mnapewa tahadhari ya dont try this at home, kwenye maslahi ya nchi
wanaotaka kumjaribu MAMA YETU nawaonya “Dont try at all”. Tujiepushe na
kadi Nyekundu.
Mheshimiwa
Spika, lazima tujenge utamaduni wa kuheshimu mali na rasilimali hapa
nchini (mali za umma na mali binafsi). Kwa upande wa mali za umma,
lazima tutangulize uzalendo na uadilifu tunapotekeleza majukumu yetu.
Serikali inapoteza fedha nyingi kwenye kutekeleza Sheria ya Ununuzi wa
Umma kwa kutojali thamani ya fedha kwenye miradi. Watumishi wa Serikali
wasio waaminifu wamekuwa wakishirikiana na wafanyabiashara wasio
waaminifu kuongeza gharama za miradi ikilinganishwa na gharama halisi
ingawa wanafuata taratibu zote za ununuzi. Taratibu za ununuzi
zinapokamilika, watumishi na wafanyabiashara hawa hugawana fedha na
kiasi kidogo tu kilichosalia ndicho kinaelekezwa kwenye mradi husika na
hatimaye kupata mradi ulio chini ya kiwango. Ukiwafuatilia kisheria
hupati moja kwa moja pa kuwashika, hivyo wanakuwa wameiba kwa kuzingatia
sheria. Nawaelekeza wote wanaohusika na ununuzi wa umma kuzingatia
sheria, taratibu, kanuni na kutanguliza mbele uzalendo na uadilifu.
Serikali itachukua hatua za makusudi katika kuimarisha usimamizi wa
sheria na taratibu za ununuzi.
Mheshimiwa
Spika, kwa upande wa mali binafsi, ni lazima tuheshimu biashara zetu na
mali zinazotokana na biashara hizo. Kuna hatua tunazozifanya sekta zote
za umma na binafsi zinadumaza uchumi wetu. Kwa mfano, kuna tabia ya
kutolipa madeni kwenye benki zetu, jambo ambalo linapunguza uwezo wa
benki kutoa mikopo kwa watu wengine. Aidha, wapo watu wengine ambao
wakidaiwa kwa makusudi ya kuchelewesha malipo wanakimbilia mahakamani.
Tusitumie vibaya vyombo vyetu vya sheria. Vilevile, kuna baadhi ya
wakopeshaji ambao hawaheshimu mali za wateja wao. Mfano, mteja anakuwa
amelipa sehemu kubwa ya mkopo wake lakini ikitokea mkopeshaji, rafiki au
dalali akaipenda dhamana iliyowekwa, hufanya njama ya kupiga mnada
dhamana hiyo kwa bei isiyolingana na thamani ya dhamana au sehemu ya
deni iliyobaki sio hata robo ya dhamana hiyo. Natoa wito kwa vyombo vya
ulinzi na usalama kufuatilia kila eneo panapokuwa na minada kwenye sekta
binafsi na hata sekta ya umma na pale patakapoonekana kuwepo kwa njama
za kudhulumu wamiliki wa mali au kuchepusha sehemu ya mali zinazouzwa
kwa mnada hatua kali za kisheria ziweze kuchukuliwa.
Mheshimiwa
Spika, Serikali ya Awamu ya Sita itaendelea kuimarisha ukusanyaji wa
mapato. Kuna wanaodhani tunapoongelea kukusanya kwa weledi, sheria na
haki wanachukulia tutaacha kukusanya kodi. Nataka nisisitize kuwa,
tutakusanya Mapato ya Serikali. Tutakusanya Mapato ya Serikali.
Tutakusanya Mapato ya Serikali. Nitoe rai kwa watumishi wote wa Serikali
wanaohusika na kukusanya kodi, maduhuli na ushuru kuelewa vizuri
maelekezo haya kwa kuzingatia sheria, weledi na kutenda haki kama
Mheshimiwa Rais alivyoelekeza. Nimeanza kusikia visingizio kila kona,
mara mfumo, mara mtandao mara EFD haifanyi kazi. Kwa watoza kodi na
walipakodi wote visingizio hivi vitaturudisha kwenye ukaguzi. Tusiwekeze
kwenye kusaidiwa kukwepa kodi bali tusaidiwe kwenye kufuata sheria.
Akiwepo mtumishi akakusaidia kukwepa kodi nawe ukampa asante
unatengeneza tatizo tu sio unafuu kwani kuna siku utakuja kukaguliwa
huku aliyekusaidia akiwa amehamishwa au kuachishwa kazi. Nitumie fursa
hii kumwelekeza Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato kuweka watu mahususi
wa kufanya doria kila kona, nchi nzima kuangalia mwenendo wa matumizi
sahihi ya EFD na mifumo mingine ya malipo kuwa muda wote inafanya kazi.
Mheshimiwa
Spika, tutasimamia nidhamu katika matumizi. Tutasimamia nidhamu katika
matumizi. Tutasimamia nidhamu katika matumizi na tutaendeleza mapambano
dhidi ya Rushwa na Ufisadi. Nazijua mbinu zote za udanganyifu, nazijua
njia zote za majizi na watakaoendelea na tabia za kudokoadokoa fedha za
walipa kodi, nitawashukia kama mwewe. Kazi inaendelea, watanzania
endeleeni kumwamini Mheshimiwa Rais wetu, yuko macho na wasaidizi wake
tuko macho, tutapambana na MCHWA wote, kuna mengine mnayasikia, kuna
mengine mnayaona na mengine hata hamyaoni, yote tunaendelea kuyafanyia
kazi kwa maelekezo thabiti na ya kizalendo ya Mheshimiwa Rais wetu.
Kinyiramba kuna msemo usemao MWINDA KANGA HAPIGI YOWE.”
Mheshimiwa
Spika, tuendeleze kwa kasi na kukamilisha miradi ya kimkakati ambayo
inalenga kukuza uchumi, kuimarisha huduma za jamii na kuongeza fursa za
ajira, hususan ajira kwa vijana. Tutakamilisha ujenzi wa Bwawa la Umeme
la Mwalimu Nyerere, tutaendelea na ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) mpaka
itakamilika, tutamalizia ujenzi wa barabara zinazounganisha mikoa
zilizosalia, tutakamilisha ujenzi wa Daraja la Kigongo-Busisi na
madaraja mengine kuwaunganisha wananchi wetu, tutaendelea na usambazaji
wa umeme kutoka kila kijiji kwenda kila kitongoji na hatimaye kila
nyumba.
Mheshimiwa
Spika, Serikali itaendelea kuboresha miundombinu ya Jiji la Dodoma na
kulifanya kuwa la kisasa. Shughuli zitakazofanyika ni pamoja na
kuendelea na ujenzi wa ofisi za wizara na taasisi zake katika mji wa
Serikali Mtumba; kujenga barabara za mzunguko; na kuboresha miundombinu
ya maji. Aidha, Serikali itaanza ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa
katika eneo la Msalato.
Mheshimiwa
Spika, Mheshimiwa Rais amenituma niwahakikishie watanzania kupitia
hotuba hii kuwa, tunaendelea kuijenga nchi, tunaendelea kuijenga nchi,
ije mvua, lije jua, tunaendelea kuijenga nchi, uwe usiku au mchana,
tunaendelea kuijenga nchi. Hakuna mradi hata mmoja utakaokwama, wala
hakuna Sekta ya maendeleo itakayozorota. KAZI INAENDELEA.”
Mheshimiwa
Spika, nampongeza Dkt. Philip Isdor Mpango aliyekuwa Waziri wa Fedha na
Mipango kwa kuteuliwa na Mheshimiwa Rais na kuthibitishwa na Bunge kuwa
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aidha, napenda
kumpongeza kwa dhati kwa kazi nzuri aliyoifanya katika usimamizi wa
uchumi kama Waziri wa Fedha wa Serikali ya Awamu ya Tano ulioiwezesha
nchi yetu kuingia katika kundi la nchi za hadhi ya uchumi wa kipato cha
kati cha chini. Vilevile, nampongeza kwa kazi nzuri iliyotukuka katika
kuisimamia Wizara ya Fedha na Mipango ambayo kwa hakika imeweka msingi
mzuri wa utekelezaji wa majukumu yangu.
Mheshimiwa
Spika, napenda kumpongeza Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, kwa
kuchaguliwa na wananchi wa Zanzibar kuwa Rais wa Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Mhe Rais Mwinyi, ameanza
kazi vizuri sana na kuwapa matumaini mapya wananchi wa Zanzibar katika
kukuza uchumi na maendeleo hasa kwa kuwekeza kwenye Blue Economy”.
Mheshimiwa
Spika, napenda kumpongeza Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa, Mbunge
wa Jimbo la Ruangwa kwa kuteuliwa na kuthibitishwa na Bunge kuwa Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Nampongeza kwa uongozi wake
hodari ndani ya Serikali na hapa Bungeni pamoja na kuendelea kumsaidia
Mheshimiwa Rais kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa ahadi zilizomo
katika Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi katika kipindi cha mwaka
2020 hadi 2025.
Mheshimiwa
Spika, naomba niwapongeze wakuu wa mihimili mingine ya Dola kwa
usimamizi na uongozi shupavu, nikianza na wewe Mheshimiwa Job Yustino
Ndugai, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa
Jimbo la Kongwa na Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson, Naibu Spika na Mbunge
wa Jimbo la Mbeya Mjini kwa kuongoza Bunge hili kwa umahiri na busara.
Aidha, nampongeza Mheshimiwa Prof. Ibrahim Hamisi Juma, Jaji Mkuu wa
Tanzania kwa uongozi makini wa Mhimili wa Mahakama unaozingatia,
miiko,dira na dhima ya mhimili huo. Hakika uongozi wake umefanikisha
upatikanaji wa HAKI kwa wanyonge na kujenga misingi imara ya utawala wa
sheria hapa nchini.
Mheshimiwa
Spika, niruhusu pia kumpongeza Mheshimiwa Balozi Hussein Athman
Kattanga kwa kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi ambaye pia ni Katibu wa
Baraza la Mawaziri na Mkuu wa Utumishi wa Umma. Nampongeza kwa
kuendelea kutekeleza majukumu yake kwa umakini na kwa weledi mkubwa.
Vilevile, nawapongeza Mheshimiwa Othman Masoud Othman kwa kuteuliwa kuwa
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na
Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla kuwa Makamu wa Pili wa Rais wa
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Mheshimiwa
Spika, napenda niwapongeze na kuwashukuru kwa dhati wakuu wote wa
vyombo vya ulinzi na Usalama. Kipekee, naomba niwatambue Mkuu wa
Majeshi, Jenerali Venance Salvatory Mabeyo; Inspekta Jenerali wa Polisi,
Simon Nyakoro Sirro; Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Diwani Athuman
Msuya; Kamishna Jenerali wa Magereza, Meja Jenerali Suleiman Mungiya
Mzee; Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Peter Makakala;
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, CP Salum
Hamdun; Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Madawa ya
Kulevya, Gerald Kusaya Musabila; na Kamishna Jenerali wa Zimamoto na
Uokoaji, John William Masunga. Utumishi wao uliotukuka na uzalendo wa
hali ya juu umetuwezesha kutekeleza shughuli mbalimbali za kijamii na
kiuchumi kwa amani Tunawaomba muendelee kutimiza wajibu wenu wa kulinda
amani na usalama wa nchi yetu kwa moyo wa uzalendo.
Mheshimiwa
Spika, kwa moyo wa dhati napenda kuipongeza na kuishukuru Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Bajeti chini ya uongozi thabiti wa Mheshimiwa Sillo
Daniel Baran, Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini na Makamu wake
Mheshimiwa Omar Mohamed Kigua, Mbunge wa Jimbo la Kilindi, kwa umakini
wao katika kuchambua na kutoa maoni na ushauri ambao umesaidia kuboresha
mapendekezo ya Bajeti hii. Aidha, ninawapongeza Wenyeviti, Makamu
Wenyeviti na Wajumbe wa Kamati zote za Kudumu za Bunge za Kisekta kwa
michango waliyotoa kupitia vikao vya Kamati za Kisekta iliyowezesha
kuboresha makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka 2021/22.
Mheshimiwa
Spika, ninawashukuru viongozi na watumishi wenzangu wa Wizara ya Fedha
na Mipango na taasisi zake kwa ushirikiano mkubwa wanaonipa katika
kutekeleza majukumu yangu ya kila siku hususan maandalizi ya bajeti hii.
Kipekee ninamshukuru Mheshimiwa Hamad Y. Masauni, Naibu Waziri wa Fedha
na Mipango na Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni. Ninamshukuru sana Katibu
Mkuu Hazina na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Emmanuel M. Tutuba, pamoja na
Naibu Makatibu Wakuu, Amina Kh. Shaaban, Adolf H. Ndunguru na Dkt.
Khatibu M. Kazungu pamoja na watumishi wa kada zote wa Wizara ya Fedha
na Mipango. Aidha, ninamshukuru Profesa Florens D. Luoga, Gavana wa
Benki Kuu ya Tanzania kwa kusimamia sekta ya fedha kwa weledi mkubwa.
Mheshimiwa
Spika, namshukuru Ndugu Alphayo J. Kidata, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA) kwa kuendelea kusimamia ukusanyaji wa mapato kwa
ufanisi mkubwa. Kadhalika, namshukuru CPA Charles E. Kichere, Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa kazi nzuri anayoifanya ya
kukagua na kutoa taarifa za matumizi ya fedha za umma kwa wakati pamoja
na kuishauri Serikali. Ninamshukuru CPA Athumani S. Mbuttuka, Msajili wa
Hazina kwa kuendelea kusimamia Mashirika ya Umma na kuhakikisha
Serikali inapata mchango na gawio stahiki. Ninamshukuru pia Dkt. Albina
Chuwa, Mtakwimu Mkuu wa Serikali kwa kusimamia vizuri Ofisi ya Taifa ya
Takwimu (NBS) na kuendelea na maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi ya
mwaka 2022.
Mheshimiwa
Spika, nawapongeza Mawaziri wenzangu na Naibu Mawaziri wote
walioaminiwa na kuteuliwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye nyadhifa hizo. Aidha, niwapongeze
pia wabunge wenzangu wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
kwa kuaminiwa na vyama vyao na kuchaguliwa na wananchi ili kuwawakilisha
bungeni. Kwa moyo wa dhati napenda kumshukuru mke wangu mpenzi Bi Neema
Nchemba, kwa kunitia moyo na kuniombea wakati wote ninapokuwa katika
utekelezaji wa majukumu yangu. Vile vile, nitumie fursa hii kuwashukuru
kwa dhati wapiga kura wangu wa Jimbo la Iramba Magharibi walioniamini na
kunichagua tena kwa kishindo kuwa Mbunge wao. Ninawaahidi kuwa
sitawaangusha.
Mheshimiwa
Spika, niwashukuru wafanyabiashara na wananchi wote ambao wameendelea
kulipa kodi kwa hiari. Rai yangu kwao ni kuwa, tukitumia rasilimali za
nchi yetu vizuri na kufanya kazi kwa umoja na bidii, tutaifanya Tanzania
kuwa kitovu cha uchumi na biashara sio tu kwa ukanda wa Afrika
Mashariki bali kwa Afrika nzima. Vile vile, navishukuru vyombo vyote vya
habari kwa kuendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa kulipa kodi
kwa hiari kwa maendeleo ya Taifa letu.
Mheshimiwa
Spika, nitakuwa mchoyo wa fadhila nisipowashukuru viongozi wa dini kwa
sala na dua zao zilizotuwezesha kukamilisha Uchaguzi Mkuu wa Rais,
Wabunge na Madiwani kwa amani na utulivu. Aidha, nawashukuru kwa
kuliombea Taifa katika kipindi kigumu tulichopitia cha kuondokewa na
viongozi wa kitaifa pamoja na mlipuko wa homa kali ya mapafu
inayosababishwa na virusi vya korona. Sala na dua zao zimetuwezesha
kupita kwa amani katika kipindi cha mabadiliko ya uongozi wa kitaifa na
hatimaye kumpata Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa
Samia Suluhu Hassan. Ninawasihi waendelee kuliombea Taifa letu bila
kuchoka.
Mheshimiwa
Spika, mwisho kabisa lakini si kwa umuhimu napenda nikushukuru wewe
binafsi kwa kunipa nafasi ya kuwasilisha hoja hii na Waheshimiwa Wabunge
wote kwa kunisikiliza.