Babu wa Loliondo maarufu kwa kutoa kikombe tiba afariki

Na Mwandishi Maalum

Mchungaji Ambilikile Mwasapile maarufu kwa jina la 'Babu wa Loliondo', ambaye alipata umaarufu wa kutoa tiba ya kikombe kilichokuwa kinadaiwa kutibu magonjwa mbalimbali amefariki dunia.
Taarifa ambazo zimethibitishwa na mmoja wa waliokuwa wasaidizi wa mzee huyo, Paul Dudui zimesema mzee Mwasapile amefariki leo Ijumaa Julai 30, 2021 mchana katika kituo Cha Afya Cha Digodigo baada ya kuugua ghafla.

"Ni kweli mzee amefariki muda huu ndio tunasubiri mwili uletwe hapa chumba cha kuhifadhi maiti hospitali ya Wasso " amesema Dudui.

Dudui amesema, mwili huo utapokelewa na viongozi wa Serikali wa Wilaya ambao ndio watatoa taarifa rasmi.

"Huu msiba mkubwa kwa wilaya nzima ya Ngorongoro na Kata ya Samunge alipokuwa anaishi mzee kwani ameleta mafanikio makubwa kutokana na kikombe cha dawa alichokuwa anato, "amesema.

Amesema kabla ya kifo aliugua wiki iliyopita na kupewa matibabu kurejea nyumbani na leo ndio hali ilibadilika ghafla na kukimbizwa kituo cha Afya cha Digodigo na kufariki.(Mwananchi)

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news