NA MWANDISHI DIRAMAKINI
Mwenyekiti wa Bodi wa Klabu ya Simba SC, Bilionea Mohammed Dewji leo ameweka hisa ya asiilimia 49 yaani Shilingi Bilioni 20 kwenye klabu hiyo kama mdhamini wa klabu.
Lengo ni kuwezesha klabu hiyo kufanya vizuri kwenye soka na kuweza kufika mbali.
MO Dewji ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Bilionea huyo ameomba taasisi hiyo iendeshwe kwa uwazi na kwa nidhamu na asitokee mtu au kikundi cha watu kufanya kitu ambacho kitaigharimu timu hiyo.
“Naomba hii taasisi iendeshwe kwa uwazi na kwa nidhamu ya hali ya juu, hatuwezi kutoka kwenye ishu ya nidhamu, la tatu hakuna mtu mkubwa kuliko Simba, Simba tumeikuta, sisi tutakufa tutaiacha Simba itaendelea, hatuwezi kukubali mtu kuwa juu ya Simba na hiyo hata Mimi ‘Mo’ sio mkubwa kuliko Simba,"amesema MO Dewji.
Amesema, ndani ya miaka minne ametumia kiasi cha shilingi Bilioni 21.3 ambapo Bilioni 5.3 ilitumika kusajili wachezaji, makocha,pre seasons, mishahara na uendeshaji wa klabu hiyo.
Nimewekeza kwa damu, jasho, na machozi ndani ya Simba. Simba ni kubwa kuliko mimi, ni kubwa kuliko kila mtu. Sisi ni Simba. Nawashukuru Wanasimba na Watanzania. Nisingekua hapa bila ya nyie wote. Tupo pamoja
Pamoja na hayo, MO Dewji amesema kuwa wameshakamilisha mchakato wa mabadiliko ambapo wamepata hati kutoka Tume ya Ushindani (FCC) ya kuwaruhusu kumaliza mchakato.
''FCC imeshatupa ruhusa kuwa mchakato wa mabadiliko umekamilika na kuna vipengele lazima vikamilike, mojawapo ikiwa ni kutoa pesa na vingine, hivyo nashukuru baada ya miaka minne ya mchakato tumefanikiwa.
''Namshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu, Spika wa Bunge Job Ndugai, Naibu Spika Tulia Ackson na wabunge mbalimbali ambao tumeshirikiana nao kufanikisha hili pamoja na wengine ambao wako nyuma ya pazia kama January Makamba ambapo wote nia yao ni kuona Simba ikifikia mafanikio,"amesema Mo Dewji.
Tags
Michezo