NA GODFREY NNKO, Diramakini Blog
Lucas Paqueta ambaye aliingia kutokea bechi, alifunga goli pekee kipindi cha pili kwa maana ya dakika ya 46 na kuwapa uhakika wa ushindi, dakika chache kabla Gabriel Jesus kuonyeshwa kadi baada ya kumpiga kwa teke Eugenio Mena.
Picha na Jean Catuffe/Getty Images.
Kwa msingi huo, Brazil imetinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Copa America dhidi ya Chile katika ushindi wa goli 1-0 walioupata wakiwa pungufu kufuatia mshambuliaji Gabriel Jesus kuonyeshwa kadi nyekundu.
Chile walipata nafasi moja ya kufunga goli kupitia kwa Ben Brereton bila mafanikio.
Kwa matokeo hayo, Brazil inafuzu kucheza nusu fainali sawa na Peru Julai 6,mwaka huu katika dimba la Nilton Santos.
Ni baada ya Peru kufuzu kwa kuitandika penati 4-3 baada ya sare ya bao 3-3.
Mtanange huo kati ya Brazil na Chile wa Julai 2, mwaka huu umepigwa katika dimba la Maracana jijini Rio de Janeiro nchini Brazil.
Neymar Jr na kocha wa Brazil, Adenor Bacchi wamesema, tukio hilo kati ya Jesus na Mena lilikuwa ajali ya kawaida katika soka kwa sababu Jesus ambaye ni mshambuliaji wa Manchester City, hakuwa amemuona mpinzani wake huyo alipowania mpira wa juu kwa kutumia miguu.
Naye Kiungo Arturo Vidal wa Chile kwa upande wake amesema kwamba, wamejitahidi kwa kila namna na wamefanikiwa katika hatua hiyo, lakini bahati haikuwa yao, hivyo wanakwenda kujiandaa kwa mechi za kufuzu kwa fainali zijazo za Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar.
Tags
Michezo