Baada ya kuwasili nchini Burundi, Rais Samia Suluhu Hassan amepokelewa na viongozi mbalimbali wa Burundi akiwemo wa Makamu wa Rais wa Burundi,Prosper Bazombanza.
Rais Samia Suluhu Hassan akiwa nchini hapa anafanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake, Rais Ndayishimiye na atashuhudia utiaji saini wa hati za makubaliano.
Mbali na hayo, Mheshimiwa Rais Samia atapata fursa ya kuhudhuria na kuhutubia mkutano wa Jukwaa la Wafanyabishara wa Burundi na Tanzania.
Tags
Kimataifa