Mwanri ateuliwa kuwa Balozi wa pamba nchini

Na Derick Milton, Busega

Bodi ya Pamba nchini imemtangaza aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri, kuwa balozi wa pamba nchini ambapo kazi yake kubwa itakuwa kuhamasisha wakulima wa zao hilo nchini kuzalisha kwa tija.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kampeini ya kitaifa ya kuongeza tija katika kilimo cha zao la pamba iliyofayika leo katika Kijiji cha Kijereshi Wilayani Busega mkoa wa Simiyu,Mkurugenzi wa Bodi ya Pamba nchini, Marco Mtunga, amesema kuwa bodi imemchangua Mwanri kuwa balozi kutokana na kazi kubwa ya kuhamasisha kilimo hicho katika mkoa wake kipindi akiwa Mkuu wa mkoa.

Mtunga amesema kuwa, Mwanri akiwa Mkuu wa mkoa alihamasisha kilimo chenye tija katika Wilaya ya Igunga, na kupelekea bodi kuanzisha kitalu cha mbengu bora katika wilaya hiyo.

Amesema kuwa, Mkuu huyo wa mkoa mstaafu atafanya kazi ya kuhamasisha kampeni hiyo ya kilimo chenye tija katika zao la pamba, kwenye mikoa yote nchini ambayo inazalisha pamba.

"Kazi kubwa ya balozi huyu, itakuwa kuhamasisha wakulima kuzalisha kwa tija kwa kufuata kanuni bora 10 za kilimo cha pamba, kazi ambayo ataianza kuanzia sasa hadi mwezi Novemba mwaka huu," amesema Mtunga.

Amesema kuwa, katika kampeni hiyo, wakulima watahamasishwa kuweka mbolea ya samadi wakati wa kupanda, kutumia kanuni mpya ya vipimo ya 60 kwa 30 lengo likiwa kuzalisha kutoka kilo 200 hadi 1000 kwa hekari moja.

Akiongea Mwanri ameishukuru Bodi ya Pamba kwa kumteua kuwa balozi, ambapo ameeleza atafanya kazi hiyo kwa kiwango kikubwa ili kuweza kufikia malengo ambayo yamewekwa.

Amewataka wadau wote katika kilimo cha pamba, wakiwemo viongozi wa serikali na siasa ngazi zote kutoa ushirikiano katika mapinduzi hayo huku akiwataka wadau wote kushirikiana katika kampeni hiyo ya kuhamasisha wakulima.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news