NA MWANDISHI DIRAMAKINI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan tayari amewasili nchini Burundi kuanza ziara ya siku mbili, kwa mwaliko wa Rais Evariste Ndayishimiye wa nchi hiyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Makamu wa Rais wa Burundi, Prosper Bazombanza alipowasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa Melchion Ndadaye Jijini Bujumbura Burudi kwa ajili ya kuanza ziara ya kitaifa ya siku mbili leo Julai 16,2021.(Picha na Ikulu).
Aidha, baada ya kuwasili nchini humo, Rais Samia Suluhu Hassan amepokelewa na viongozi mbalimbali wa Burundi akiwemo wa Makamu wa Rais wa Burundi,Prosper Bazombanza.
Rais Samia Suluhu Hassan akiwa nchini humo anatarajia kufanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake, Rais Ndayishimiye na atashuhudia utiaji saini wa hati za makubaliano.
Mbali na hayo, Mheshimiwa Rais Samia atapata fursa ya kuhudhuria na kuhutubia mkutano wa Jukwaa la Wafanyabishara wa Burundi na Tanzania.
Tags
Kimataifa