RC Mtaka: Dodoma tuna wagonjwa wa Corona, tukuchukue tahadhari

Na Doreen Aloyce,Diramakini Blog

MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Mheshimiwa Anthony Mtaka ametoa taarifa ya muendelezo wa hali ya ugonjwa wa Virusi vya Corona ambapo amesema, kama mkoa wagonjwa wapo na wameendelea kupatiwa huduma.
Akiongea na waandishi wa habari leo jijini hapa, huku akiwa ameambatana na timu yake ya afya, mkuu huyo amewataka wananchi kuacha kubahatisha hali zao za mwili na hivyo amewasihi wanapohisi mabadiliko ya kimwili wawahi katika vituo vya afya, zahanati na hospitali zilizopo karibu yao.

Aidha, amesema Mkoa wa Dodoma ni mojawapo ya mikoa Saba iliyopatiwa mtambo wa kufyatua hewa ya Oxgeni ambapo mpaka sasa maeneo yote ya wodi za wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa ya General zimeshafungwa hewa hiyo ya Oxgeni.

MAELEKEZO

Hata hivyo, amewataka wananchi kuacha kuchukulia mzaa kuhusu uwepo wa ugonjwa wa Virusi vya Corona na kuwataka kufahamu kwamba ugonjwa wa Corona upo na wagonjwa wapo kila mmoja azingatie taadhari za kiafya.

"Niendelee kutoa rai kwenye nyumba zetu za ibada, viongozi wetu wa dini endeleeni kuwaelimisha waumini kuzingatia masharti ikiwemo kunawa mikono, kuvaa barakoa, kutumia vitakasa mikono, na kukaa umbali wa mita moja," amesema Mtaka.

MIKUSANYIKO

Amewataka wananchi kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima na vyombo vya usafiri wahakiishe gari haijazi abiria hadi kufikia hatua ya kuwasimamisha.
Pia amewataka wananchi wa mkoa wa Dodoma kuondoa hofu na kupuuza habari zinazosambaa kwa baadhi ya watu kwamba hospitali ya Rufaa ya General na Hospitali ya Benjamin Mkapa zimefurika na kueleza kwamba hali iko vizuri

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa Dodoma, Dkt. Best Magoma amesema wanaishukuru serikali kwa kuwapatia mtambo wa kuzalisha hewa ya Oxgeni wenye thamani ya shilingi Billioni 1.2.

Ameeleza kwamba, uzalishaji wa hewa hiyo ya Oxgeni umewasaidia ambapo wameweza kusambaza karibu sehemu zote ndani za wodi za wagonjwa na wameanza na wodi za wagonjwa mahututi ICU, wodi ya dharura na wodi za watoto.

"Sasa hivi tumeachana na suala la kutumia mitungi ya gesi kwani ilikuwa na gharama, lakini tangu kuletwa kwa mtambo huu hewa ya Oxgeni tunazalisha hapa na mikakati yetu ni kusambaza hewa hii kwenye hospitali zote za hapa Dodoma, "amesema.

Amebainisha kwamba, mtambo huo wa kuzalisha hewa ya Oxgeni ni muhimu katika hospitali na hivyo mtambo kwa siku unazalisha mitungi hewa ya Oxgeni 250 hadi 300.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news