RC SENGATI ATAKA KIPAUMBALE ZAIDI KUKABILIANA NA SUALA LA LISHE SHINYANGA

Na Anthony Ishengoma-Shinyanga

Takwimu za lishe kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe za mwaka 2018 zinaonesha tatizo la upungufu wa damu kwa akina mama waliokatika umri wa kuzaa limepungua kutoka 59.4% kwa mwaka 2015/16 hadi kufikia 30.6% mwaka huu na kiwango cha udumavu kwa watoto walioko chini ya miaka mitano umeongezeka kutoka 30% hadi 32.1%.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akitoa hotuba yake kwa wadau wa lishe mkoa wa Shinyanga katika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati amebainisha hayo jana wakati akiutubia kikao cha Mkoa wake kilichokaa kujadili tathimini ya hali ya lishe lakini pia kuangazia suala zima la kuhamasisha wananchi kujiunga na Bima ya Afya iliyoboreshwa katika wilaya zinazounda mkoa wa Shinyanga.

Dkt. Sengati alisema takwimu hizo pia zinaonesha kuwa takwimu za ukondefu kwa watoto pia limeongezeka kutoka 2% hadi 4.3% na kuongezeka kwa uzito kwa watoto hao wachanga pia limepungua kutoka 22%hadi 15% hivyo kuwataka viongozi Mkoani Shinyanga kuwa inahitajika dhamira ya dhati kabisa kufikia hatua nzuri zaidi katika utekelezaji wa hafua hizi za lishe.

Mkuu wa Mkoa pia ameagiza Halmashauri zote kuendelea kutenga bajeti ya mtoto kwa kutoa shilingi elfu moja kwa kila mtoto aliye chini ya miaka mitano kutoka vyanzo vya mapato ya ndani kwa lengo la kuboresha hafua za lishe kwa watoto hao na kuongeza kuwa kwa hili baadhi ya Halmashauri zimeendelea kufanya vizuri isipokuwa kwa Halmashauri ya Kishapu ndiyo haijafanya vizuri.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Bw. Joseph Modest Mkude akiongea na vyombo vya habari kuhusu kutofanya vizuri katika eneo la lishe alisema sio vigezo vyote ambavyo Wilaya yake imeshindwa kufanya vizuri bali mapungufu yamejitokeza katika eneo la uchangiaji shilingi elfu moja kwa kila mtoto chini ya miaka mitano.

Aidha Bw. Mkude aliongeza kuwa katika hatua muhimu anayoenda kuifanya Wilayani kwake ni kuwaimiza wakurugenzi kuweka dhamira ya dhati katika suala hilo ikiwemo kutoa elimu ya masuala ya lishe kwa jamii kama hatua muhimu ya kujiweka vizuri katika boresha suala la lishe katika Wilaya ya Kishapu.

Akiangazia suala la Bima ya Afya iliyoboreshwa Mkurugenzi wa Manispaa ya kahama Bw. Anderson Nsumba aliwaambia wajumbe wa Mkutano kuwa changamoto inayojitokeza katika Bima ya Afya iliyoboreshwa ni upungufu wa dawa unaochangiwa na Bohari Kuu ya Dawa kushindwa kutoa dawa kulingana na kiwango ambacho kinalipwa na Halmashauri zinaomba kwa ajili mahitaji yao.

Bw. Nsumba aliongeza kuwa kwasasa unatanguliza malipo Bohari ya Dawa lakini unapewa kiasi kidogo cha dawa ulizolipia hivyo mteja wa Bima ya Afya iliyoboreshwa akija katika kituo cha Afya na kukosa dawa anakata tamaa na kadi yake inapoisha muda anakuwa haendelei na utaratibu wa kukata nyingine.
Baadhi ya wadau wa lishe mkoa wa Shinyanga wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Philemon Sengati mapema jana katika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

Wakati huo huo Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga aliongeza kuwa wakati mwingine kunakuwa hakuna changamoto ya upungufu wa dawa bali kuna baadhi ya watumishi wa sekta ya Afya wanawambia wagonjwa kuwa dawa hakuna wakati zipo na kuongeza kuwa watumishi hao watachukuliwa na anataka kuona ni hatua zipi zimechukuliwa dhidi yao.

Wadau wa lishe mkoa wa Shinyanga walikutana jana kufanya tathimini ya lishe katika mkoa wa shinyanga kwa kutumia vigezo tisa vilivobainishwa katika katika kadi maalumu inayoandaliwa Afisa lishe Mkoa kuangalia maeneo ambayo kila Halmashauri imefanya vizuri na katika maeneo ambayo hazijafanya vizuri kujitathimini na kuchukua hatua kwa lengo la kuboresha hafua za lishe katika ngazi ya mkoa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news