Kwa mujibu wa Wizara ya Afya, Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan Julai 28, 2021 atazindua zoezi la utoaji chanjo ya Corona, uzinduzi utakaofanyika Ikulu mkoani Dar es Salaam kwa yeye kuchanjwa.
Aidha, baada ya hapo Wizara ya Afya itaendelea na usambazaji wa chanjo na kutoa utaratibu wa uchanjwaji wananchi katika vituo vilivyoandaliwa nchini;
Kufuatia chanjo hizo kupokelewa nchini, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anatarajiwa kufanya uzinduzi wa zoezi la uchanjaji," imeeleza taarifa hiyo.
Aidha, imeweka wazi kuwa uzinduzi wa uchanjaji unaweka historia kwa taifa katika kuendeleza mapambano dhidi ya UVIKO-19 ikiwa ni nyongeza mahususi ya afua nyinginezo za chanjo ikiwemo unawaji mikono kwa maji safi tiririka na sabuni, uvaaji wa barakoa katika maeneo hatarishi, ufanyaji wa mazoezi na upataji wa lishe bora na matumizi ya tiba asili zilizosajiliwa na Baraza la Tiba Asili.
Imebainisha kuwa itoaji wa chanjo ni moja ya afua muhimu na inayoaminika duniani kote katika kupambana na maradhi hususani ya kuambukiza ikiwemo ugonjwa
wa UVIKO-19 hivyo watanzania watumie fursa hiyo.
Imesema baada ya uzinduzi huo, serikali inatarajia kuendelea kupokea chanjo dhidi ya UVIKO-19 ili kuhakikisha watanzania wengi zaidi wanachanjwa.
Imewataka viongozi wote kuiga mfano huo wa kuonyesha njia ya kupata chanjo kwa hiari.