Na Andrew Chale
MBIO za Kimataifa za Zanzibar International Marathon 2021, tayari wametangaza rasmi zawadi nono kwa washindi wa mbio hizo zitakazofanyika 18 Julai, mwaka huu.
Waziri wa Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita (kushoto) akionyesha pamoja na kamati ya mbio za Zanzibar International Marathon, zawadi kwa watakaoibuka washindi hiyo 18 Julai, mwaka huu.
Kamati ya Maandalizi ya Zanzibar International Marathon imetangazwa rasmi zawadi hizo za washindi wa mbio zote mbele ya mgeni rasmi Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita tukio ambalo limefanyika katika Hotel ya Park Hyatt Zanzibar.
Zawadi hizo ni pamoja na: Milioni 3,000,000 (Mil3) kwa washindi wa KM21 kike/kiume, Mil 2,500,000 kwa washindi wa pili na Mil 1,000,000 kwa mshindi wa Tatu.
Kwa mbio za KM 10, Mshindi wa kwanza ni Mil 2,500,000, Mshindi wa wa pili 2 ni Mil 1,000,000 na wa Tatu ni Tsh. 750,000.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na kamati ya mbio za Zanzibar International Marathon na baadhi ya wadhamini wa mbio hizo wakati wa kutangaza rasmi zawadi kww watakaoibuka washindi hiyo 18 Julai, mwaka huu.
Mbio za KM 5 mshindi wa kwanza ni mil 1,000,000, wa pili Tsh.750,000 na wa Tatu ni Tsh. 500,000.
Aidha, kwa upande wa Walemavu watatoa zawadi kwa mshindi wa kwanza hadi wa tatu pekee ikiwemo Mshindi wa kwanza ni Mil 1,000,000 wa pili Tsh.750,000 na wa tatu ni 500,000.
Kwa upande wake, Msemaji wa mbio hizo, Hassan Mussa Ibrahim amesema zoezi la kujiandikisha linaendelea katika maeneo tofauti
"Unaweza kulipia mtandaoni na pia kwa kujiandikisha kupata fomu za ushiriki kwenye maduka ya Dauda sports, Just Fit sports gear Kijitonyama na Mlimani cty na kwa hapa Zanzibar zinapatikana kupitia Cataluna Barbershop iliopo Kiembesamaki, Park Hyatt Zanzibar, Cape Town fish market Zanzibar." Alisema Hassan Mussa Ibrahim.
Tags
Michezo