ACT Wazalendo nao wasusia mwaliko wa Tume ya Uchaguzi kesho

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Chama cha ACT Wazalendo kimesema hakitahudhuria hafla ya uwasilishaji wa ripoti ya uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 28 mwaka jana itakayofanyika kesho Agosti 21 Ikulu, Dar es Salaam.
Chama hicho kimesema kimepokea mwaliko kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ambayo itamkabidhi Rais Samia Suluhu Hassan ripoti hiyo lakini hawatahudhuria kwakuwa wanaamini uchaguzi huo ulivurugwa.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo Agosti 20, 2021 na Katibu wa Habari, Uenezi na Uhusiano wa chama hicho, Salim Bimani amesema wameiandikia NEC kwamba hawatashiriki na kuwaeleza sababu zao.

"Kwenye tukio hilo, NEC itasoma na kuwasilisha ripoti ya uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020 kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

"Katibu Mkuu wa Chama (Ado Shaibu) ameiandikia Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuieleza kuwa Chama cha ACT Wazalendo hakitashiriki kwenye shughuli hiyo,"ameeleza.Unaweza kusoma, CHADEMA nao wasusia mwaliko.

Amesema, uamuzi huu umefikiwa kutokana na kile walichodai kwamba mwaka 2020 hakukuwa na uchaguzi bali uchafuzi "hivyo chama chetu kushiriki kwenye tukio hilo itakuwa ni sawa na kuhalalisha hujuma kubwa iliyofanyika mwaka 2020."

Kwa mujibu wa Bimani, uzoefu wa Ripoti ya Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) ya uchaguzi wa Mwaka 2020 unaonesha kuwa, ripoti za uchaguzi za ZEC na NEC zinatumika kuhalalisha kilichotokea kwa kuandika hadaa na uzushi kwahiyo hawatarajii kitu tofauti.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news