Amber Rutty azua jambo Manispaa ya Temeke baada ya kualikwa mgeni rasmi shuleni

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke umeeleza kuchukizwa kwake na kitendo cha Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nzasa kumualika Amber Rutty kama mgeni rasmi na kuongea na wanafunzi.
“Kumekua na taarifa zinazosambaa kupitia kipande cha video mitandaoni zikimuonesha mtu mmoja akitembelea Shule ya Msingi Nzasa iliyopo Temeke, akiwa amevaa mavazi yaliyo kinyume na maadili ya Kitanzania.

“Tunapenda kutoa taarifa kwamba uongozi wa Manispaa ya Temeke umechukizwa na ugeni huo, umemuonya Mkuu wa Shule kwa kukiuka maadili ya utumishi wa umma kutokana na kitendo kilichotokea na Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza,"imeeleza taarifa ya Kitengo cha Habari na Uhusiano, Manispaa ya Temeke.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news