NA MWANDISHI DIRAMAKINI
Askofu Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima na Mbunge wa Kawe mkoani Dar es Salaam amefika kuhojiwa katika Kamati ya Bunge Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge.
Askofu Gwajima pamoja na Mbunge wa Ukonga (CCM) Jerry Silaa wameitwa mbele ya Kamati ya Maadili na Madaraka ya Bunge ili kujibu tuhuma mbalimbali ikiwemo kusema uongo na kushusha hadhi na heshima ya Bunge.
Taarifa iliyotolewa Jumamosi Agosti 21, 2021 na Kitengo cha Mawasiliano Ofisi ya Bunge, imeeleza wabunge hao wameitwa mbele ya Kamati hiyo kwa agizo la Spika wa Bunge Job Ndugai.
Aidha, Gwajima alifika katika viwanja vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
majira saa 6:35 mchana leo kuitikia wito huo.
Baadae Askofu
Gwajima alikaa saa moja na nusu akisubiri kuitwa na kamati na
muda ulipofika alitakiwa kuingia kwenye ukumbi ambao kamati walikuwa
wakimsubiri.
Aidha,taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Kamati, Emmanuel
Mwakasaka ilisema shahidi ambaye ni Mbunge wa Kawe, Askofu Gwajima kuna
dawa anaitumia hivyo waendelee kumsubiri kwani alimuagiza dereva.
"Sina taarifa ya shahidi kama ana tatizo lolote la kiafya linalomtaka shahidi ameze dawa kwanza ndio aje, kwa hiyo tuendelee kumsubiri inawezekana limempata baada ya kufika hapa,"amesema Mwenyekiti huyo.
"Sina taarifa ya shahidi kama ana tatizo lolote la kiafya linalomtaka shahidi ameze dawa kwanza ndio aje, kwa hiyo tuendelee kumsubiri inawezekana limempata baada ya kufika hapa,"amesema Mwenyekiti huyo.
Dakika chache baadae Askofu Gwajima aliingia katika ukumbi waliokuwepo kamati na akaomba kubadilishiwa kiti kilichokua kimeandaliwa kwa ajili yake na kubadilishiwa kipaza sauti.
Ni kipazasauti ambacho kilikuwa kimendaliwa akitumie yeye
kuongelea, ombi lililokubaliwa na wajumbe wa kamati hiyo na baada ya muda
Mhudumu wa Bunge alibadilisha vifaa hivyo na kamati kuanza kumuhoji. Baada ya mahojiano na Askofu Gwajima, Kamati itamuhoji, Jerry Silaa.
MUHIMU
UNATAMANI DIRAMAKINI BLOG TUWE HEWANI SAA 24 KUKUPA HABARI ZA KINA KILA DAKIKA, TUNAOMBA UTUUNGE MKONO KWA KUCHANGIA GHARAMA ZA MAWASILIANO NA INTANETI KWA WAANDISHI WETU POPOTE WALIPO NDANI NA NJE YA TANZANIA; TUNAPOKEA MCHANGO WAKO KUPITIA 0719254464 (Tigo Pesa-Godfrey Nnko) AU UKIHITAJI NAMBA YA BENKI TUJULISHE. MUNGU AKUBARIKI SANA KWA SAPOTI YAKO. ASANTE