NA MWANDISHI DIRAMAKINI
Mathias Manga ambaye anatajwa kuwa miongoni mwa Watanzania wenye ukwasi mkubwa amefariki.
Manga ambaye ni miongoni mwa Mabilionea waliowekeza katika miradi mbalimbali huku akijishughulisha na biashara ya madini ya Tanzanite amefariki leo.
Kifo cha Bilionea huyo ni pigo na simanzi kwa watu wengi kwani. Licha ya biashara pia aliwahi kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC).
"Manga ametutoka,huyu alikuwa tajiri wa wote, amefariki dunia akitibiwa huko nchini Afrika Kusini,"mmoja wa watu wa karibu amemdokeza Mwandishi Diramakini.
Bilionea Manga alikuwa anaendesha Hoteli ya Gold Crest zilizopo jijini Arusha na Mwanza na alikuwa anamiliki majumba ya kifahari jijini Arusha.
Aliyewahi kuwa Mbunge wa Shinyanga Mjini na Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika, Stephen Masele ameandika kupitia akaunti yake ya Twitter…
“RIP Mathias Manga: Nimehuzunika sana. Siamini rafiki yangu umetangulia: Mtu mwema,mwenye roho nzuri na upendo, mkarimu, mwenye kujitoa kwa ajili ya jamii na watu. Mwenyezi Mungu akupe pumziko la amani. Pole kwa familia, ndugu na marafiki wote.”
Haya yanajiri ikiwa ni saa chache zimepita baada ya Bilionea mwingine Tanil Somaiya wa SHIVACOM kufariki.
Bilionea Tanil Chandulal Somaiya alifariki ghafla Agosti 11 jijini Dar es Salaam.
Kutokana na changamoto ya Corona, familia iliwaomba waombolezaji kutoenda nyumbani kwa marehemu kwa ajili ya msiba