Na Robert Kalokola, Diramakini Blog
Waziri wa Maji Jumaa Aweso amevunja Kamati ya Maji ya Jumuiya ya Watumia Maji ya Kijiji cha Mharamba,Kata ya Nkome wilayani Geita baada ya kubaini dalili za ubadhirifu katika makusanyo ya maji katika mradi wa Mharamba.
Waziri wa Maji Jumaa Aweso akizungumza katika mkutano wa hadhara katika Kijiji Cha Mharamba ,Kata ya Nkome Wilaya ya Geita (Robert Kalokola/DIRAMAKINI BLOG).
Mwenyekiti wa Kamati hiyo alimueleza Waziri wa Maji kuwa kamati hiyo ina laki tano benki lakini baada ya mahojiano na Waziri ikaonekana kamati ilipaswa kuwa imekusanya zaidi ya milioni 20.
Kufuatia tukio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Geita Wilson Shimo ameagiza Mkuu wa Polisi Wilaya ya Geita na Takukuru kuwakamata Mwenyekiti,Katibu na Mweka hazina wa kamati hiyo ili kufanya uchunguzi wa mapato na matumizi ya mradi huo.

HABARI ZAIDI ZINAKUJIA HAPA PUNDE