DIRAMAKINI Blog yatunukiwa tuzo ya Kimataifa na cheti cha heshima kwa habari bora

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Mkurugenzi Mtendaji wa Diramakini Business Limited inayomiliki DIRAMAKINI BLOG, Godfrey Nnko imeishukuru Taasisi ya Kimataifa ya Nishigandha Vsa Pratishan Trust, Khorda, Odisha ya nchini India kwa kuitunuku DIRAMAKINI BLOG tuzo na cheti cha heshima kutokana na uchakataji na usambazaji wa maudhui bora ya habari za Kiswahili na Kiingereza. Pongezi hizo alizitoa muda mfupi baada ya tuzo hiyo iliyotolewa Agosti 9, 2021 katika Jimbo la Odisha nchini India.

"Awali ya yote sisi Diramakini Blog tunamshukuru Mungu kwa kutupa nguvu na uwezo wa kuweza kuhudumia jamii kupitia maudhui ya mtandaoni,tulipokata tamaa kutokana na vikwazo vingi ambavyo tumekuwa tukikabiliana navyo, tulimuomba Mungu na akatupa ujasiri wa kusimama tena.

"Pili nichukue nafasi hii kuwashukuru sana wasomaji wa DIRAMAKINI Blog ambao wamekuwa washauri wakubwa kwetu, pale tunapokosea mara moja huwa wanatutumia barua pepe kutushauri namna bora ya kuchakata habari zetu ili ziweze kuwa na tofauti, hali hiyo imeendelea kutupa nguvu na ari ya kufanya kazi kwa bidii.

"Tatu tunaishukuru sana Taasisi ya Kimataifa ya Nishigandha Vsa Pratishan Trust, Khorda, Odisha ambayo imekuwa ikifuatilia kwa karibu maudhui yetu katika blogu yetu na kujiridhisha kuwa, yana hadhi na viwango bora, hivyo kututunuku tuzo na cheti cha heshima. Hii kwetu ni ishara tosha ya ushindi katika kuelekea malengo yetu ya kutoa huduma bora za taarifa zilizochakata zikiwa zimehaririwa, zenye uhakika na zinazogusa na kuleta mbadiliko chanya katika jamii. Tunaamini hii itatufanya tuongeze bidii zaidi,"amesema Mkurugenzi Mtendaji Diramakini Blog, Godfrey Nnko.

Nnko amesema kuwa, blogu yao ambayo inaongozwa na kauli mbiu ya Habari za Kuaminika na Zinazolenga Makundi yote imekuwa na mapokeo mazuri tangu ilipopata usajili zaidi ya miezi 10 iliyopita.Zinazohusiana soma;TAKUKURU yaitunuku DIRAMAKINI cheti cha pongezi

"Mafanikio haya yanakuja ikiwa bado hatujafikisha mwaka mmoja tangu tupatiwe usajili na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania zikiwemo mamlaka nyingine za Serikali, hii inamaanisha kwamba, tuendako kuna tumaini jipya kwa kuwa, kila mwenye bidii na amuombaye Mungu na kumtegemea katika kazi zake lazima atapata mafanikio, hivyo nichukue nafasi hii kuwaomba wasomaji wetu na hata wafanyabiashara waendelee kutuunga mkono ili tuweze kusonga mbele zaidi na hakika tutawapa taarifa na makala bora zenye kuleta hamasa na kuongeza maarifa ambayo yatamuwezesha kila mmoja kufanya maamuzi yatakayomvusha kutoka hatua moja kwenda nyingine,"amefafanua Nnko.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news