NA MWANDISHI DIRAMAKINI
Aliyekuwa Msemaji wa Klabu ya Simba SC , Haji Manara ametambulishwa rasmi na Klabu ya Yanga huku akitangaza kuhamia na familia yake nzima.
"Nakwenda Yanga kwa sababu ina viongozi watakaonipa nafasi ya kuwasaidia, nilibanwa mno, nilidhihakiwa mno, sijawahi kuwa na matatizo na Simba;
Haji Manara ametambulishwa ndani ya Yanga leo Jumanne Agosti 24,2021 huku akiahidi kuwa tamasha la Jumapili la Wiki ya Mwananchi halijawahi kutokea.
Manara amesema kuwa kazi anaanza kesho rasmi kwa kuzindua jezi mpya ambayo haina makando.
“Nimejiunga na Klabu kubwa kupita zote Afrika Mashariki na Kati, huu ukubwa lazima nifanye na klabu kubwa. Nitashirikiana na wenzangu kutimiza malengo ya Klabu” ,amesema Haji Manara.
"Nakwenda Yanga kwa sababu ina viongozi watakaonipa nafasi ya kuwasaidia, nilibanwa mno, nilidhihakiwa mno, sijawahi kuwa na matatizo",amesema Manara.
Ikumbukwe kuwa Manara aliondoka Simba Sc baada ya kutupiana maneno na viongozi wa klabu hiyo kwa tuhuma za kuihujumu timu yake ambayo amekuwa nayo kwa muda mrefu.