NA MWANDISHI DIRAMAKINI
Katibu wa Ofisi ya Mbunge wa Kibaha Vijijini, Johari Marijani ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo.
Johari ameyasema hayo kupitia taarifa kwa umma aliyoitoa leo Agosti 20,2021.a
"Naomba kuufahamisha umma wa Kibaha Vijijini kwamba kuanzia sasa, mimi JOHARI MARIJANI si Katibu tena wa Ofisi ya Mbunge wa Kibaha Vijijini. Nimejiuzulu."Sababu ya kujiuzulu ni kuelemewa na majukumu ya Ofisi ya Mbunge na majukumu mengine mengi yanayonihusu, huku majukumu ya pande zote yakiwa na umuhimu mkubwa na uzito unaokaribiana. Kwa hiyo, nimechagua kutokuwa mkwamishaji wa majukumu muhimu ya Ofisi ya Mbunge kwa kuamua kujiuzulu.
Namshukuru sana Mhe Mbunge kwa imani na ushirikiano mkubwa alionipatia kwa kipindi chote ambacho nimefanya naye kazi.
"Aidha, nawashukuru pia wananchi na wadau wote wa Jimbo la Kibaha Vijijini kwa kushirikiana nami vema kwa kipindi chote ambacho nimehudumu katika Ofisi hii. Namtakia kila la kheri Mhe Mbunge anapojipanga upya kuendeleza vema huduma za Ofisi hii bila uwepo wangu,"amefafanua aliyekuwa Katibu wa Ofisi ya Mbunge wa Kibaha Vijijini aliyejiuzulu,Johari Marijani.
Jimbo la Kibaha Vijijini Mkoa wa Pwani linaongozwa na Mheshimiwa, Michael Mwakamo.