NA MWANDISHI DIRAMAKINI
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, raia wa Denmark, Kim Poulsen amemrejesha kikosini kipa Ramadhani Kabwili wa Yanga katika kikosi kitakachoingia kambini Agosti 24 kujiandaa na mechi za kufuzu Kombe la Dunia.
Taifa Stars itamenyana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Septemba 2 Uwanja wa TP Mazembe mjini Lubumbashi katika mchezo wa Kundi J kufuzu Kombe la Dunia.
Ni kabla ya kurejea Dar es Salaam Septemba 7, mwaka huu kumenyana na Madagascar na Oktoba 10 itaifuata Benin kukamailisha mechi za mzunguko wa kwanza wa kundi lake.
Kikosi hicho kinaundwa na Aishi Manula, Metacha Mnata, Ramadhani Kabwili, Wilbol Maskeke, Shomari Kapombe, Israel Mwenda, Erasto Nyoni, Dickson Job, Bakari Mwamnyeto, Kennedy Juma, Lusajo Mwaikenda, Abulrazack Mohamed, Mohamed Hussein, Nickson Kibabage, Edward Manyama.
Wengine ni Ayoub Lyanga, Meshack Mwamita, Novatus Dismas, Msamiru Yassin, Mudathir Yahya, Feisal Salum, Salum Abubakar, Zawadu Mauya, Iddy Selemani, Abdul Hamis, Mbwana Samatta, John Bocco, Simon Msuva.