Mashindano ya Kombe la Kagame 2021 yameanza kati ya Yanga ya Tanzania na Nyasa Big Bullets ya Malawi. Mtanange huo safi umepigwa katika dimba la Benjamin Mkapa lililopo Halmashuri ya Manispaa ya Temeke mkoani Dar es Salaam ambapo umemalizika kwa sare ya bao 1-1. Aidha, Yanga SC imetambulisha baadhi ya wachezaji wake iliyowasijili kwa msimu ujao. |
Hiki ndiyo kikosi cha Yanga SC kilichoanza dhidi ya Nyassa Big Bullet, sura mpya ni pamoja na Dickson Ambundo winga kutoka Dodoma Jiji,Jimmy Ukonge kutoka UD Songo.
Chini ya Razak Siwa kama Kocha Mkuu kwenye mashindano hayo, Yanga iliwachezesha nyota wake hao akiwemo Dickson Ambundo na Jimmy Julio Ukonde kutoka Msumbiji, huku Fiston Mayele naye akishuhudia akiwa jukwaani.
Ni ndani ya dakika 45 za kipindi cha kwanza ambapo zilimalizika kwa sare ya bao 1-1.
Waziri Junior kwa upande wa Yanga alifunga dakika ya 8, kabla ya Chiukepo Msowoya kuisawazishia Nyasa dakika ya 29 kwa mkwaju wa penati baada ya Abdalah Shaibu wa Yanga kumchezea rafu Babatunde Adepoju wa Nyasa.
Kipindi kilirejea kwa timu zote mbili kuanza kwa kasi kila moja ikitafuta bao la kuongoza lakini hadi dakika ya 75 hakuna aliyekuwa amepata bao.
Aidha, dakika ya 83, Paulo Godfrey wa Yanga alioneshwa kadi ya njano baada ya kumchezea rafu mshambuliaji wa Nyasa, Hassan Kajoke nje kidogo ya eneo la boksi la Yanga.
Baada ya hapo Nyasa walipiga pigo la faulo na mpira kupaa juu lakini dakika moja baadae Nyasa kupitia kwa Kajoke alifanya shambulizi lililookolewa na kipa wa Yanga Ramadhan Kabwili.
Dakika ya 89 kipa wa Yanga, Kabwili alioneshwa kadi nyekundu baada ya kumchezea faulo ya makasudi mshambuliaji Kajoke wa Nyasa aliyekuwa akielekea langoni kwa Yanga.
Kadi nyekundu hiyo iliwalazimu Yanga kumfanya mabadiliko ya lazima kwa kumtoa mshambuliaji Julio Ukonde na nafasi yake kuchukuliwa na kipa Geofrey Magaigwa.
Tags
Michezo