Chini ni sehemu ya kazi bora zaidi za ujenzi wa madaraja na barabara ikiwa ni kazi inayofanywa na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA);
Hivi karibuni, Serikali ilizindua Mpango Mkakati wa Pili wa miaka mitano wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) wenye thamani ya shilingi Trilioni 3.6.
Akizindua
mpango huo jijini Dodoma, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Ummy Mwalimu amebainisha namna Serikali
itakavyoimarisha utendaji kazi wa wakala huo kwa kuwapa magari na
kuajiri watumishi wa kada mbalimbali ikiwemo wahandisi.
Uzinduzi
wa mpango huo ulioenda sambamba na uzinduzi wa kauli mbiu isemayo
‘TARURA tunakufungulia barabara, kufika kusikofikika’, Waziri Ummy
amesema utekelezaji wa mpango huo utaleta mapinduzi makubwa ya ujenzi wa
barabara nchini na kurahisisha maeneo ya mijini na vijijini kufikika.
“Mpango
huu unaanza mwaka huu 2021/22 hadi 2025/26 na utaongeza mtandao wa
barabara kutoka kilometa 2,404.90 hadi 3,855.65, changarawe kutoka
kilometa 29,116.57 hadi 102,358.14 na madaraja kutoka 2,812 hadi 6,620
na fedha zitakazotumika ni Sh.Trilioni 3.6,”amesema.
Ameseza
kuwa, kama mpango mkakati huo utatekelezwa vyema zitajengwa barabara za
changarawe kilometa 73,242 na kwamba hayo ni mafanikio makubwa kwa kuwa
asilimia 70 ya barabara nchini ni za vumbi.