Students selected to join form five and Technical Colleges 2021/22 academic year -Waliochaguliwa Kidato Cha Tano 2021( Second Selection)
List of students selected to join Form Five (TAMISEMI) Form five Selection 2021):( Second Selection)
OFISI YA RAIS - TAMISEMI
UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA KATI, 2021
BOFYA HAPA CHINI JINA LA MKOA KUONA ORODHA YA WANAFUNZI WALIOPANGWA KWENDA SHULE MOJA
CHAGUA MKOA ULIKOSOMA
ARUSHA | DAR ES SALAAM | DODOMA |
GEITA | IRINGA | KAGERA |
KATAVI | KIGOMA | KILIMANJARO |
LINDI | MANYARA | MARA |
MBEYA | MOROGORO | MTWARA |
MWANZA | NJOMBE | PWANI |
RUKWA | RUVUMA | SHINYANGA |
SIMIYU | SINGIDA | SONGWE |
TABORA | TANGA |
Wanafunzi 4,105 wamechaguliwa kujiunga kidato cha tano kwa mwaka huu katika uchaguzi wa awamu ya pili kutokana na waliochaguliwa awamu ya kwanza kutoripoti kwenye shule walizopangiwa.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Prof.Riziki Shemdoe, wakati akitangaza matokeo ya uchaguzi wa awamu ya pili mbele ya waandishi wa habari jijini Dodoma.
Prof. Shemdoe amesema kuwa kati ya wanafunzi waliochaguliwa, wanafunzi 499 (wavulana 424 na wasichana 75) wamepangiwa tahasusi za Sayansi na Hisabati na wanafunzi 3,604 wakiwemo wavulana 3,461 na wasichana 143 wamepangiwa tahasusi za masomo ya Sanaa na Biashara.
Amebainisha kuwa upangaji wa awamu ya pili umefanyika baada ya Wizara kujiridhisha na nafasi zilizo wazi katika shule ambazo wanafunzi hawakuripoti.
“Kwa kuangalia idadi ya wasichana waliopangiwa kujiunga na kidato cha tano awamu ya pili imekuwa ndogo, hii ni kwa sababu katika uchaguzi wa awamu ya kwanza wanafunzi wote wasichana waliokuwa na vigezo walichaguliwa hivyo hapakuwa na wanafunzi wasichana waliokuwa wamebakia,”amesema Prof. Shemdoe
Amefafanua kuwa, wanafunzi wasichana waliochaguliwa katika awamu ya pili ni wale ambao waliomba kubadilishiwa machaguo yao kutoka vyuo mbalimbali walivyokuwa wamechaguliwa awali na kupelekwa kidato cha tano.
“Wanafunzi waliopangwa awamu ya pili wanatakiwa kuripoti katika Shule walizopangiwa kuanzia tarehe 16 hadi 30 Agosti, 2021, hivyo mwanafunzi ambaye atashindwa kuripoti hadi tarehe 30 Agosti, 2021 atakuwa amepoteza nafasi yake,”amesisitiza Prof . Shemdoe.
Aidha, amewaomba wazazi na walezi waelewe kwamba hakutakuwa na nafasi yoyote ya wanafunzi hawa kubadilishiwa shule kwa kuwa shule walizopangwa ni zile zilizobainika kuwa na nafasi kwa tahasusi husika.