Maliki Apolinary baada ya kumbaka Mwanafunzi alimficha kwenye pipa lililojaa maji chumbani kwake

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Maliki Apolinary (20) mkazi wa Barabara ya Moto wilayani Handeni mkoani Tanga anatuhumiwa kumtendea ubaya mwanafunzi wa shule ya msingi.

Ubaya huo umeenda Sambamba na kumbaka mwanafunzi wa kike anayesoma darasa la nne na kumficha kwenye pipa lililojaa maji chumbani kwake.
Kutokana na tukio hilo la kikatili, Maliki anashikiliwa na Jeshi la Polisi wilayani Handeni mkoani Tanga.

Ni Agosti 25,2021 ya saa nne asubuhi ambapo DIRAMAKINI Blog imeshuhudia Maliki akidakwa kwa kitendo hicho ambacho kimewashangaza wakazi wengi wa mtaa huu.

Hadija Kiula ambaye ni Balozi wa mtaa huo wa Barabara ya Moto amesema, walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa akiwa chumbani na mwanafunzi huyo mwenye miaka 10 huku akijiandaa na mitihani ya darasa la nne ambayo inatarajiwa kuanza hivi karibuni.

"Tumeweza kufuatilia kwa ukaribu maendeleo ya mtoto huyu mpaka tukafanikiwa kubaini kuwa mtoto huyu ameingiliwa kiukweli inaumiza sana, kwa kuwa binti huyu bado ni mdogo sana,"amesema Balozi Hadija Kiula.

Afisa Elimu wa Halmashauri ya Mji wa Handeni, Elizabeth Kilaya amekiri kuwa huyo binti ni mwanafunzi wa darasa la nne shule ya msingi Chanika.

"Binti huyu kweli ni mwanafunzi wa darasa la nne shule ya msingi Chanika na tumesikitishwa na kitendo hiki alichotendewa na tunaliomba sheria ichukue mkondo wake ili kukomesha vitendo vya aina hii,"amesistiza Afisa Elimu huyo.

Baada ya tukio hilo kamati ya ulinzi na usalama ikiongozwa na mkuu wa wilaya ilifanikiwa kufika kwenye eneo la tukio huku mkuu wa wilaya hiyo, Siriel Mchembe akibubujikwa na machozi kwa unyama aliofanyiwa binti huyo.
DC Mchembe alitoa wito kwa wananchi kuendelea kufichua vitendo kama hivyo vya kikatili wanavyofanyiwa watoto wa kike.

"Mbali na kuwa kiongozi mimi ni mama nimesikitishwa na kitendo hiki, huu ni unyama haiwezekani tukayafumbia macho matendo machafu kama haya yanayofanywa na baadhi ya watu, jambo hili litakuwa funzo kwa wengine wenye tabia kama hizi,"amesema.

MUHIMU


UNATAMANI DIRAMAKINI BLOG TUWE HEWANI SAA 24 KUKUPA HABARI ZA KINA KILA DAKIKA, TUNAOMBA UTUUNGE MKONO KWA KUCHANGIA GHARAMA ZA MAWASILIANO NA INTANETI KWA WAANDISHI WETU POPOTE WALIPO NDANI NA NJE YA TANZANIA; TUNAPOKEA MCHANGO WAKO KUPITIA 0719254464 (Tigo Pesa-Godfrey Nnko) AU UKIHITAJI NAMBA YA BENKI TUJULISHE. MUNGU AKUBARIKI SANA KWA SAPOTI YAKO. ASANTE

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news