Mbowe, wenzake wasomewa mashitaka sita likiwemo la kutaka kumdhuru Lengai Ole Sabaya

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Freeman Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na wenzake watatu wamesomewa mashitaka sita ikiwemo la kutaka kumdhuru aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai wakati huo, Lengai Ole Sabaya.

Hayo yameelezwa leo Agosti 23, 2021 na upande wa mashtaka ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Nassoro Katuga akisaidiana na Ester Martin, wakati wakiwasomea maelezo ya mashaidi na vielelezo washtakiwa hao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Thomas Simba.

Wamesomewa mashitaka hayo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyopo jijini Ilala mkoani Dar es Salaam.

Aidha, inadaiwa Mbowe alituma kiasi cha shilingi 600,000 kwa washitakiwa wenzake kwa ajili ya kufanya maandalizi ya vitendo vya ugaidi ikiwemo kutaka kulipua vituo vya mafuta, mikusanyiko ya watu, kukata miti na kuisambaza barabarani.

Mbali na Mbowe wengine kwenye kesi hiyo ni waliokuwa Walinzi wake, Halfan Bwire Hassan, Adam Hassan Kasekwa na Mohamed Abdallah Ling'wenya.

Mashtaka hayo ni pamoja na kula njama za kutenda ugaidi ambapo Mbowe anatuhumiwa kufadhili vitendo hivyo vya kulipua vituo vya mafuta kwa kutoa zaidi ya shilingi 600,000.

Piaa watuhumiwa wote wanatuhumiwa kushiriki vikao vya kutenda kosa la ugaidi huku mshtakiwa wa pili anatuhumiwa kumiliki bastola yenye risasi tatu kwa ajili ya kutenda kosa la ugaidi.

Aidha, mshtakiwa wa kwanza anatuhumiwa kumiliki nguo, begi na koti zote za Jeshi la Wananchi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Aidha, mashahidi 24 na vielelezo 19, wanatarajia kutoa ushahidi katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi inayomkabili, Mheshimiwa Mbowe na wenzake watatu.

Miongoni mwa mashahidi hao ni aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai nchini,DCI Robert Boaz.

MUHIMU

UNATAMANI DIRAMAKINI BLOG TUWE HEWANI SAA 24 KUKUPA HABARI ZA KINA KILA DAKIKA, TUNAOMBA UTUUNGE MKONO KWA KUCHANGIA GHARAMA ZA MAWASILIANO NA INTANETI KWA WAANDISHI WETU POPOTE WALIPO NDANI NA NJE YA TANZANIA; TUNAPOKEA MCHANGO WAKO KUPITIA 0719254464 (Tigo Pesa-Godfrey Nnko) AU UKIHITAJI NAMBA YA BENKI TUJULISHE. MUNGU AKUBARIKI SANA KWA SAPOTI YAKO. ASANTE

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news