NA MWANDISHI DIRAMAKINI
Spika wa Bunge, Job Ndugai ameamuru Wabunge wawili Josephat Gwajima na Jerry Silaa kupelekwa mbele ya Kamati ya Maadili na Madaraka ya Bunge ili kujibu tuhuma mbalimbali ikiwemo kusema uongo na kushusha hadhi na heshima ya Bunge.
Gwajima anatakiwa kufika mbele ya Kamati hiyo Jumatatu Agosti 23,2021 saa saba mchana na Silaa anatakiwa kufika Jumanne Agosti 24,2021.
“Endapo yeyote kati ya Gwajima na Silaa hatofika mbele ya Kamati hiyo kwa siku na muda uliotajwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa;