NA MWANDISHI DIRAMAKINI
MBUNGE wa Viti Maalumu kupitia Asasi za Kiraia Tanzania Bara (NGOs) Neema Lugangira ameteuliwa kuwa Balozi wa hamasa dhidi ya mapambano ya virusi vya Corona (COVID-19).
Mheshimiwa Neema Lugangira ameteuliwa Agosti 12,mwaka huu na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mheshimiwa Dkt. Dorothy Gwajima mkoani Dar es Salaam.
Mbunge Neema Lugangira ambaye pia ni Balozi wa Covid-19 akiwa na bango la kuhamasisha uvaaji wa barakoa na wananchi kuhakikisha wanachanja na kuzingatia miongozo mingine ya Afya.
Mbali na Mbunge Neema Lugangira wengine walioteuliwa ni msanii maarufu nchini na Mwenyekiti wa Jukwaa la Mama Ongea na Mwanao, Steven Mengele 'Steve Nyerere' na Mwanaharakati wa Kutetea Haki za Wanawake nchini, Joyce Kiria.
Mbunge wa Neema Lugangira ambaye pia ni Balozi wa Covid-19 wa kwanza kulia akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Afya Maendeleo Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Dorothy Gwajima. Akifuatiwa na Msanii maarufu nchini na Mwenyekiti wa Jukwaa la Mama Ongea na Mwanao, Steven Mengele 'Steve Nyerere' na Mwanaharakati wa Kutetea Haki za Wanawake nchini, Joyce Kiria.
Hatua hii inakuja ikiwa tangu janga la Corona liingie nchini kwenye Wimbi la Kwanza hadi sasa Wimbi la Tatu, Mbunge Neema Lugangira ameonyesha jitihada mbalimbali za kupambana na janga hilo.
Miongoni mwa jitihada hizo ni pamoja na kuelimisha, kutoa mahitaji ya kukabiiana na maambukizi na kuhamasisha Watanzania kujikinga na kuchanja ili kujikinga dhidi ya ugonjwa huo hatari ambao umeathiri maeneo mengi duniani.