Mbunge wa CCM ajiuzulu ubunge


NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Awali Chama Cha Mapinduzi (CCM), lishinda uchaguzi katika jimbo la Konde visiwani Zanzibar, baada ya mgombea wake Sheha Faki kujipatia kura 1,796 na kuwashinda wagombea wenzake 11.

Matokeo ya uchaguzi huo yalitangazwa Julai 19, 2021, ambapo Faki alipata kura 1,796 kati ya kura halali 5,020 zilizopigwa.

Uchaguzi huo mdogo ulifanyika kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kutokea Chama cha ACT-Wazalendo Khatib Said, kufariki dunia Mei 19 mwaka huu.

Hata hivyo, Chama cha Cha Mapinduzi (CCM) kimeelezakuwa kimepokea kwa masikitiko barua ya kujiuzulu kwa Mbunge Mteule wa CCM Jimbo la Konde, Sheha Mpemba Faki leo Agosti 2,2021.

Taarifa iliyotolewa leo na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa,Itikadi na Uenezi CCM,Shaka Hamdu Shaka amesema katika barua yake, Sheha Mpemba Faki ameeleza kwamba amefikia uamuzi huo kutokana na changamoto za kifamilia, jambo ambalo chama hakina uwezo wa kumzuia, hasa ikizingatiwa kwamba ni haki yake ya msingi kama ilivyo kwa haki ya kuomba ridhaa ya kugombea nafasi ndani ya CCM.

Amesema, chama chao kinawaomba wanachama wote kuwa watulivu katika kipindi hiki wakati tukisubiri taratibu nyingine.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news