Na Nteghenjwa Hosseah, Sengerama
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa amesema Serikali itapeleka Shilingi Mil 400 kwenye Kituo cha Afya Kamanga Feri Kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Sengerem Mkoani Mwanza.

Amesema, fedha hizo ni kwa ajili ya kutatua changamoto iliyokuwepo katika Kituo hicho na kupitia fedha hizo Kutajengwa Chumba cha Upasuaji pamoja na Wodi ya Mama na Mtoto.
Akiwa ziarani Wilayani humo mapema leo Tar 14.08.2021 Mhe Ummy alijulishwa changamoto ya kituo hicho kuwa ni kukosekana kwa chumba cha upasuaji, upungufu wa watumishi pamoja na mafuriko pale Ziwa Victoria linapofurika.




Kituo cha Afya Kamanga kinahudunia Wakazi Takribani elf 60 wa Kata za Kamanga, Katunguru, Ngoma B na Kahunulo.