Mwalimu aliyedhalilisha Watoto apoteza ajira, Waziri atoa msimamo wa Serikali

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Mheshimiwa Simai Mohamed Said ambaye ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar ameagiza kusimamishwa kazi mwalimu,Suleiman Mohamed wa shule binafsi ya Sunni Madressa iliyopo jijini Zanzibar.

Ni kwa tuhuma za kuwapa adhabu za kuwadhalilisha wanafunzi kinyume cha Sheria na Sera ya Elimu nchini.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mheshimiwa Simai Mohammed Said akiangalia kwa makini video zilizonaswa katika CCTV kamera ya Skuli ya Sunni Madressa juu ya udhalilishaji uliofanywa na mwalimu kwa kufanya udhalilishaji.

Mwalimu Mohamed wa shule hiyo ya Msingi iliyopo mjini Unguja jijini Zanzibar anadaiwa kutoa adhabu hiyo ya kuwadhalilisha wanafunzi hao Julai 2021.

Waziri Simai leo Agosti 21,2021 amesema amefikia hatua hiyo baada ya kukutana na watendaji wa shule hiyo Mkunazini Mjini Unguja na kujiridhisha na kuona video za CCTV.

Amesema,kwa misingi ya taratibu na haki za watoto sio vyema kuitoa hadharani video hiyo.

"Sisi kama wizara tulikubaliana na bodi inayosimamia shule hiyo kwamba hatutaitoa nje kwa sababu inaweza kusababisha hali mbaya kwenye jamii,” amesema Mheshimiwa Simai Mohamed Said.

Pia amesema, licha ya kuwepo madai kwamba wizara imeegemea upande wa wazazi si sahihi.

"Kwani sisi tunawabeba wote na tunathamini bidii na kila tukio linapotokezea tunadili nalo kulingana na yule mtu aliyefanya lile jambo,"ameongeza.

Mrajisi wa Elimu na Katibu wa Baraza la Elimu Zanzibar, Zuwena Mataka Hafidhi amesema sheria ya elimu ina miongozo na kanuni zake zinazoelekeza kuhusu adhabu anayotakiwa kupewa mtoto anapokosea.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news