Ndama 'Mtoto ya Ng'ombe' ajinasua jela miaka mitano

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Leo Agosti 2,2021 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyopo jijini Ilala mkoani Dar es Salaam imemhukumu mfanyabiashara Ndama Hussein na Mkemia Yusuph Yusuph, kulipa faini ya sh. milioni 1.5 au kwenda jela miaka mitano baada ya kuwatia hatiani kwa kosa la kujipatia dola za Marekani 75,000 kwa njia ya udanganyifu.

Kiasi hicho walijipatia kutoka kwa raia ya Botswana, Emmanuel Motilhathedi baada ya kumdanganya kwamba wana kampuni ya dhahabu.

Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi Godfrey Isaya, baada ya washitakiwa hao kuandika barua ya kukiri kosa na kisha kuingia makubaliano na Mkurugenzi ya Mashtaka nchini( DPP).

Kabla ya kutolewa kwa adhabu hiyo Wakili wa Serikali Mwandamizi, Ladislaus Komanya, alisoma maelezo ya makubaliano hayo kwamba fidia inakwenda katika akaunti ya mlalamikaji ambaye alitapelewa.

Alidai katika makubaliano tayari mlalamikaji ameshalipwa kiasi cha Dola za Marekani 50,000 katika akaunti yake na kiasi kilichobakia kinalipwa ndani ya miezi minne kuanzia sasa.

Alifafanua kuwa, kuanzia Septemba 31, mwaka huu washitakiwa wanatakiwa kulipa Dola 12,500 na kumalizika kiasi kilichobakia Novemba 31 mwaka huu katika akaunti yake.

Hata hivyo washitakiwa walifanikiwa kulipa faini hiyo na kukwepa adhabu ya jela.

Wakili Komanya, kutokana na ushahidi ulioko washitakiwa walitekeleza kwa pamoja genge la uharifu kujihusisha na biashara ya kuuza madini feki kwa raia wa Botswana ambapo waliweza kumlaghai kuwa Kampuni yao inajihusisha na madini.

Baada ya mawasiliano kwa njia ya simu na barua pepe na raia huyo kabla ya kufika nchini Januari 2021 akishirikiana nao kwa hatua mbalimbali waliwapatia Dola za Marekani 150,000 ili wampatie shehena ya dhahabu kilogramu 500.

Waliendelea kumshawishi mlalamikaji huyo kwamba anatakiwa kutoa fedha kwa ajili ya tozo la vibali ndipo alipowashtukia na kufanya ufuatiliaji kwa wahusika wa madini na kujiridhisha kwamba madini hayo ni feki.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news