NA MWANDISHI DIRAMAKINI
Ni jukumu letu sote kuendelea kuyatunza mazingira ili kuweza kuzikabili changamoto za mabadiliko ya tabianchi.
Pichani ni muonekano wa barafu zilizotokana na mvua ya upepo na barafu iliyonyesha wilayani Biharamulo Mkoa wa Kagera mwishoni mwa wiki.
Mdau ameieleza DIRAMAKINI Blog kuwa mvua hiyo ya saa mbili ilileta taharuki kidogo katika maeneo mbalimbali mjini hapa ikiwemo Lubondo na Lukaragata.(Picha zote na Mdau/Diramakini Blog).